Ukubwa Wa Baraza La Mawaziri Ni Ufisadi Mkubwa


Freetown

Freetown

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2008
Messages
887
Likes
17
Points
35
Freetown

Freetown

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2008
887 17 35
Ukubwa wa baraza la mawaziri ni ufisadi mkubwa sana, nasema hivi kwa sababu nchi zilizoendelea tena zinazochangia bajeti yetu zina baraza dogo la mawaziri kuliko TZ. Kenya nchi ambayo hakuna ubishi imetuzidi sana kiuchumi ina baraza la mawaziri 40 ambalo pia limepigiwa kelele sana na wananchi wa nchi hiyo mpaka walifanya maanadamano ambayo mwanamama aliye wahi kuwa mshindi wa Noble alipokea maanamamno hayo na kuelezea juu ya ubaya wa kuwa na baraza kubwa la mawaziri kuwa ni mzigo kwa wananchi.
Sasa kwa nchi yetu hata pale Rais alipounda baraza la mawaziri 60 halikupingwa waziwazi. umefika wakati katiba ileeze wazi kuwa tunatakiwa kuwa na baraza la mawaziri wasiozidi 20 ili kupunguza mzigo kwa wananchi ambao hali zao zinazidi kuwa mbaya kila kukicha. Najua wabunge wengine hawatafurahi kwa sababu udogo wa baraza la mawaziri utawanyima ndoto yao ya kuwa mawaziri
Tujaribu kulipia kelele hili swala jamani!!!!!!!!!!!!!!
 

Forum statistics

Threads 1,235,534
Members 474,641
Posts 29,225,844