Ukuaji uchumi wa Tanzania waikuna IMF

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Patricia Kimelemeta na Newstar Rwechungura

SHIRIKA la Fedha la Duniani (IMF), limetoa tathmini ya ukuaji uchumi kipindi cha nusu mwaka, huku ikionyesha hadi sasa uchumi imeimarika.


Akizungumza Dar es Salaam juzi, Kiongozi wa tathmini hiyo kutoka IMF, Paolo Mauro alisema tathmini hiyo ilifanywa chini ya Mpango wa Ushauri wa Sera za Uchumi (PSI), ambao umeonyesha pato la taifa linatarajiwa kukua kati ya asilimia 6.5 hadi 7.


Mauro alisema ukuaji huo unatokana na serikali kusimamia vizuri suala la ukusanyaji mapato, kupunguza gharama za matumizi, kulinda matumizi ya huduma za jamii na utoaji fursa ya uwekezaji katika miundombinu muhimu.


Alisema kutokana na hali hiyo, serikali imesimamia mikopo ya biashara kutoka nje ili iendane na deni la taifa, jambo ambalo linaweza kuleta maendeleo ya kuridhisha katika utekelezaji wa malengo ya mfumo chini ya mpango maalum, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.


“Katika kipindi cha nusu mwaka, serikali ya Tanzania imesimamia kwa umakini ukusanyaji kodi ya mapato, uwekezaji na kuboresha miundombinu mbalimbali inayochochea ukuaji uchumi, jambo ambalo limesaidia kupunguza ukubwa wa deni la taifa,” alisema Mauro.


Aliongeza kuwa ili kuongeza ufanisi zaidi, wanapaswa kuhakikisha wanasimamia kwa umakini ulinganifu wa hesabu, ili kuongeza mapato katika nyanja mbalimbali ikiwamo biashara, huduma, mapato ya uchumi na uhamisho wa mali za nje ya nchi.


Alisema kutokana na hali hiyo, serikali inapaswa kupunguza gharama za uagizaji mafuta ambayo kwa kiasi kikubwa yamechangia kupanda kwa gharama za maisha, kuboresha miundombinu ya gesi asilia ili iweze kutumika kwa shughuli mbalimbali.


“Iwapo Tanzania itasimamia kwa umakini matumizi ya gesi asilia na kuingiza kwenye gridi ya taifa ili kuzalisha 2,500 za umeme, gharama za maisha zinaweza kupungua kwa asiliamia kubwa,” alisema.


Pia, alisema gesi hiyo itaweza kutumia viwandani na majumbani, jambo ambalo linaweza kuongeza uzalishaji bidhaa na ajira.

Waziri wa Fedha na Uchumi, William Mgimwa alisema kutokana na tathmini hiyo, serikali imepanga kusimamia mfumko wa bei ili kupunguza gharama za maisha kwa wananchi.
Dk Mgimwa alisema mazao ambayo yamepanda zaidi ni mchele, sukari na mahindi.

Ukuaji uchumi wa Tanzania waikuna IMF
 
Sawa wamesimamia vizuri ukusanyaji wa mapato, so called kumkamua ng'ombe Mwananchi..... nani anawasimamia wao katika matumizi ya mapato yaliyokusanywa? Efficiency iko wapi hapa kama hakuna mlinganyo?
Inflation iko 18% na ukuaji wa uchumi 6.9% to 7% mnatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
watu wanazidi kuwa masikini kila siku, govt haina hata hela za kulipa mishahara ya mwezi mmoja na miradi inazidi kusimama kwa kukosa hela halafu wewe unakuja na title "Ukuaji uchumi wa Tanzania waikuna IMF"!
 
Back
Top Bottom