Ukraine: Wizara ya Ulinzi yatetea uamuzi wa Wanajeshi wa Kike kuvaa viatu vya mchuchumio

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imetetea uamuzi wake wa kuwavalisha wanajeshi wa kike viatu vya mchuchumio (vyenye visigino virefu) katika gwaride la kusherehekea miaka 30 ya kujitenga na Umoja wa Kisovieti baada ya baadhi ya wabunge kulalamikia uamuzi huo.

Picha za wanajeshi hao zilisambaa katika mitandao ya kijamii, zikiwaonesha wakiwa wamevaa viatu vyenye visigino virefu, wakifanya mazoezi kwa ajili ya tukio hilo la Agusti 24, jambo lililoonekana geni kwa watu wengi nchini humo.

Wabunge wapatao watano walionekana kutopendezwa na jambo hilo, wakilalamikia athari za viatu hivyo kwa afya ya wanajeshi na kuwa haviendani na mahitaji ya kijeshi, na kusaini waraka wa pamoja kusimamia kauli yao. Wabunge hao wanataka viatu hivyo viondolewe, kisha ateuliwe msimamizi wa haki za kijinsia atakayepitisha dodoso kwa wanajeshi wote 57,000 wa nchi hiyo kuwauliza wanavyojisikia kuhusu utendaji wao wa kazi, ikiwamo kuhusu sare.

Wizara ya Ulinzi, hata hivyo, imepuuzia malalamiko hayo ikisema wanajeshi hao watashiriki gwaride wakiwa na viatu vyao vya mchuchumio.

“Ni kazi ngumu kidogo kufanya mazoezi kwa viatu vya mchuchumio kuliko buti za kijeshi, lakini tunajaribu,” Ivanna Medviv, ambaye amekuwa akiwafunza wanajeshi hao kwa mwezi mmoja sasa, aliliambia Gazeti la Kijeshi la Army Inform la nchini Ukraine. Kama sehemu ya kujibu malalamiko hayo, Wizara ya Ulinzi ilichapisha picha za wanajeshi wa kike kutoka majeshi mengine duniani wakiwa wamevaa viatu vya mchuchumio.

Jeshi la Ukraine linaanzisha viwango vya kijeshi vya Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (NATO), vinavyosisitiza usawa wa haki kwa wanajeshi wote bila kujali jinsia.

1625552172686.png


1625552185227.png

Chanzo: CNN
 
Back
Top Bottom