Ukraine: Serikali na Waasi wanaoungwa mkono na Urusi wabadilishana Wafungwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali ya Ukraine na waasi wanaotaka kujitenga mashariki mwa nchi ambao wanaoungwa mkono na Urusi wameanza kubadilishana wafungwa hii leo.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na wa Ukraine Volodymyr Zelensky kukutana kwa mazungumzo ya ana kwa ana kwa mara ya kwanza mjini Paris mnamo Desemba 9.

Viongozi hao walikubaliana kuchukua hatua za kusitisha vitaa pekee vinavyoendelea barani Ulaya kwa sasa. Bado haijulikani ni watu wangapi waliobadilishana hii leo. Mwakilishi wa waasi wa mji wa mashariki mwa Ukraine wa Donetsk, Daria Morozova, amesema mapema leo kwamba upande wa uasi utarejeshewa wafungwa 87, na wataikabidhi serikali watu wake 55.

Mahusiano kati ya Ukraine na Urusi yaliharibika tangu 2014, Urusi ilipoinyakuwa rasi ya Crimea na kuwasadia waasi wa mashariki mwa Ukraine kuanzisha vuguvugu la kutaka kujitenga.
 
Back
Top Bottom