Ukosoaji wa Awamu ya Tano ni Woga wa wapinzani

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,982
45,901
Kwa sasa kuna uelekeo wa wapinzani kujaribu kukosoa kila jambo ambalo serikali ya awamu ya tano imekua ikilifanya.

Uhalisia sio kwamba ni kweli kua awamu ya tano inakosea.

Siwezi kukataa kua kuna makosa, ya kibinadamu, lakini lililowazi ni kua upinzani haupendi kuona yale Magufuli na awamu ya tano wanayoyafanya.

Ukweli ni kwamba, kuna woga wa kukosa nafasi chaguzi zijazo.

Kwanini wana woga, kwakua mpaka kufikia uchaguzi ujao, asilimia kubwa ya yale ambayo upinzani umekua ukiyataka kuyafanya Magufuli atakua ameyafanya kwa kiwango kikubwa na kwa weledi.

Hivyo vilio vyao vinanipa faraja na kuona kua sasa CCm ipo pazuri na tunafanya yale yanayogusa nyoyo za watanzania wengi.
 
Walianza na "Magufuli anatekeleza sera za UKAWA". Wakaona hawaoni pa kushikiria, wakageuka kupingana naye kuwa hafuati sheria.

Cha msingi, watafute pa kushikiria na watafute vijana wenye ueledi wajenge chama upya, hasa CHADEMA. Waliokijenga wameondoka. Sasa wanashindwa hata kufikiria pekee yao.

Akili na shule viko pamoja.
 
Ujinga walio nao sasa
Wanaishi kwa kufuata upepo
Wakiona jambo wananchi wana lipongeza sana
Wanasema Serikali inatekeleza Ilani ya (UPAWA)
kesho utawasikia CCM ni ileile!!

Kiukweli Unatakiwa Akili zako ziingiliwe NA Sisimizi ili uwashabikie hawa watu.

Hoja ya Zanzibar imebuma
Kwasasa wapowapo kama vifaranga vilivyo kosa mlezi

AKILI NDOGO KUONGOZA AKILI KUBWA NDIO MATOKEO YA UKAWA KUWA UPAWA
 
ndio siasa hizo nyie mnataka asifiwe tu hata kwa madudu,tatizo ccm hamjielewi mlimsifia mkwere alipotoka mkamuona takataka JPM naye akitoka mtamuona ovyo acheni unafiki,kosoa akikosea msijitie upofu,kazi ya upinzanini watchdog wa serikali hata akikosea kufunga kifungo cha shati ni kosa
 
Unapo penda kukosoa
Kubari NA wewe kukosolewa

Nawakosoa Nyie Hamna mwenyekiti MNA Msweta
 
Kwa sasa kuna uelekeo wa wapinzani kujaribu kukosoa kila jambo ambalo serikali ya awamu ya tano imekua ikilifanya.

Uhalisia sio kwamba ni kweli kua awamu ya tano inakosea.

Siwezi kukataa kua kuna makosa, ya kibinadamu, lakini lililowazi ni kua upinzani haupendi kuona yale Magufuli na awamu ya tano wanayoyafanya.

Ukweli ni kwamba, kuna woga wa kukosa nafasi chaguzi zijazo.

Kwanini wana woga, kwakua mpaka kufikia uchaguzi ujao, asilimia kubwa ya yale ambayo upinzani umekua ukiyataka kuyafanya Magufuli atakua ameyafanya kwa kiwango kikubwa na kwa weledi.

Hivyo vilio vyao vinanipa faraja na kuona kua sasa CCm ipo pazuri na tunafanya yale yanayogusa nyoyo za watanzania wengi.

Unachoongea ni vichekesho vya mchana kweupe, kwani miaka yote hiyo mnayofanya vibaya mmekubali kuachia madaraka hata mnapoonekana kushindwa dhahiri? Ni hivi ccm itaendelea kutawala mpaka pale wananchi watakapoamua kufanya machafuko na wala sio kushinda kwa ubora wa matendo. Kwa hiyo hilo unalosema wapinzani wanaogopa kushindwa ni kama unatuona sisi ni watoto wadogo. Toa maoni yako kuhusu hicho kinachoendelea uchaguzi wa meya oanisha na huo utoto wako ulioandika hapa. Halafu malizia na uhuni uliofanyika znz.
 
Kwa taarifa yako Messi ni mchezaji nguli wa timu ya Barcelona, lakini hata akiondoka hakuna uwezekano wa timu hiyo kufa. Kwa hiyo kuondoka kwa mwanachama yoyote katika chama sio mwisho wa chama husika zaidi ya kuacha pengo fulani.
 
Binafsi sioni dhambi kwa chama/vyama vya upinzani kukosoa serikali isipokuwa tatizo linakuja kwenye jambo linalokosolewa.
Tukubali kwamba hakuna serikali imara pasipo na upinzani imara, kwani mara nyingi waliopo kwenye vyama tawala ni ngumu sana kukosoa mifumo na matendo ya vyama vyao kwa hofu ya kukidhoofisha machoni mwa wapiga kura au kujitafutia nafasi katika serikali.
 
kumekwisha tolewa madai mara kadhaa kuwa Magufuli anafanya kazi kwa kutumia Ilani ya vyama vya upinzani
kwa maana hiyo wapinzani hawana cha kuikosoa serikali iliyoko madarakani
 
Mleta mada utakuwa na homa ya manjano, kama hayo unayo yasema ndio mwisho wa upeo wako basi leo hii huko USA kusingekuwa na pilikapilika za uchaguzi.
 
ndio siasa hizo nyie mnataka asifiwe tu hata kwa madudu,tatizo ccm hamjielewi mlimsifia mkwere alipotoka mkamuona takataka JPM naye akitoka mtamuona ovyo acheni unafiki,kosoa akikosea msijitie upofu,kazi ya upinzanini watchdog wa serikali hata akikosea kufunga kifungo cha shati ni kosa
Mbwa anyebweka hata bila ya adui, huyo mbwa anapaswa kuwa mlinzi wako kweli?
 
Miaka 55 tangu nchi iwe huru, hatujawah kupigana wenyewe kwa wenyewe au mauwaji ya kimbari, au baa la njaa la kutisha. Nchi tulizokuwa almost sawa miaka hiyo saiv ziko mbali, sie maji umeme yan social services tu hakuna. Halafu wanakuja wazee yan watu wazima na mvi zao, na vijana wao wote ukiunganisha na vyombo vya ulinzi hakuna strategy yoyote waliyonayo zaidi ya kuwaza UKAWA tu. Kweli Mungu akunyime vyote lakin asikunyime akili.
 
Back
Top Bottom