Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 27,520
- 34,823
Yaani tuna Majaji vilaza ?Wanabodi, hili ni bandiko la kitambo, hoja yake ni uwezo mdogo wa baadhi ya majaji na mahakimu wetu kuwa na jicho la tatu, jicho la ndani, jicho la roho kubaini haki.
Hoja hii inathibitishwa na kinachoendelea ndani ya mhimili wa Mahakama sasa. Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma, ametimiza umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria tangu Juni 15, lakini kufuatia kukoseana majaji Rufaa wenye uwezo wa kushika nafasi ya Jaji Mkuu, imebidi Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma aongezewe muda kidogo wakati wa kumuandaa mrithi wake.
Hivyo hoja yangu hii inapata nguvu!, yaani licha ya kuwepo majaji kibao wenye sifa za kuwa Jaji Mkuu, lakini bado hawatoshi, hali inayopelekea Jaji Mkuu aliyemaliza muda wake, kuongezewa muda mpaka mrithi muafaka apatikane.
Kuongezewa muda huku, kukamuibua Jaji Stella Mugasha Profesa Ibrahim Juma kuendelea kuwa Jaji Mkuu, Rais Samia anavunja Katiba ya JMT? hivyo na mimi nikashauri Jaji Mugasha Apewe Maua Yake Kupinga Uvunjifu wa Katiba Ukomo wa CJ, ila Mbona Hili ni Dogo Tuu, Kubwa ni Katiba Yetu Imenajisiwa! Why Wako Kimya?!.
Kuna vitu watu tunasema humu, wana wanapinga!. Majaji Rufani wenye sifa za kuwa Jaji Mkuu, wangekuwepo wa kutosha, kusingelikuwa na need kumuongezea muda CJ aliyemaliza muda wake!.
P