Ukosefu wa wakalimani katika shughuli za kijamii

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Katika sehemu nyingi za kijamii kama vile makanisani, misikiti, sherehe za harusi na misiba walemavu viziwi huachwa nyuma bila kuwepo huduma za wakalimani.

Mara nyingi makanisa mengi ambayo sio ya viziwi hayajali uwepo wa walemavu Viziwi na hayaweki mkalimani na Wala mchungaji au shehe hatumii lugha za Alama anapoendesha ibada.

Hii imepelekea walemavu viziwi kukosa haki ya kuabudu sehemu za karibu na makazi yao hivyo kulazimika kufunga safari kwenda kutafuta makanisa ambayo ni maalum kwa viziwi ambayo yanakuwepo mbali na sehemu zingine hayapo kabisa.

Hivyo kiziwi kushindwa kupata huduma za kiroho kikamilifu. Katika shughuli za harusi na misiba ‘watu huchukulia poa’ kumuacha kiziwi akiwa anatoa macho tu huku haelewi kinachoendelea.

Hali huwa mbaya zaidi pale kama mfiwa ni kiziwi anashindwa kujua hatma ya urithi wa mali za mfano baba yake ama mama yake ama mume wake.

Walemavu wengi viziwi hudhulumiwa mali zao kutokana na kukosa huduma ya mawasiliano.
 
Umeona mbali kwa darubini Kali

Hapa itabdi lianzishwe somo la alama za vidole mashuleni hii ijumuishe wote

Itasaidia mtu akikutana na kiziwi Basi atakumbukakutumia hizo alama
 
Mada nzuri sana!! Tatizo hao wataalamu wa lugha za alama wanakidhi?
 
Back
Top Bottom