Ukosefu wa ruzuku CUF Tanzania bara mtaji mkubwa wa kisiasa kwa Hamad Rashid | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukosefu wa ruzuku CUF Tanzania bara mtaji mkubwa wa kisiasa kwa Hamad Rashid

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DT125, Dec 19, 2011.

 1. D

  DT125 JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Ni wazi kuwa mgogoro wa madaraka kati ya Maalim Seif na Hamad Rashid, unaonekana kuigawa CUF pande mbili za Bara na Visiwani na usiposhughulikiwa vizuri utakuja kuwa mgogoro mkubwa utakao kuja kujenga chuki kwa wazanzibari wa CUF kuuchukia Muungano kama walivyo Wazanzibari wa CCM kwenye kumpata mgombea wa Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo kura za wajumbe wengi wa Bara hupitisha mgombea Urais wa Zanzibar. Vikao visivyo rasmi vya viongozi wa CUF wa wilaya na mikoa ya Tanzania Bara vinavyoendelea Dodoma visivyofahamika nani mfadhiri wake, wajumbe wanaonekana kumuunga mkono Hamad Rashid. Kuungwa mkono kwa Hamad Rashid kunatokana na chama hicho kushindwa kupeleka ruzuku katika baadhi ya mikoa kutokana na kupungua kwa ruzuku yake ukilinganisha na uchaguzi 2005. Kama kikao cha maamuzi ya mwisho kwenye chama hicho kitakuwa na wajumbe wengi wa Bara ni wazi kuwa Hamad Rashid hayatampata yaliyompata Kafulila na hii itaibua mgogoro kati ya wanachama wa Bara na wa visiwani ambao utakuwa hatari kubwa kwa ustawi wa CUF. Wakijieleza katika mahojiano yao na Star Tv leo wameonekana kutoridhika na matumizi ya fedha zilizo tumika kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo wa Igunga, tuhuma inayomwangukia Julius Mtatiro ambaye amejiingiza kwenye mgogoro wa wawili hao kwa kumshambulia HR na kutoa picha kuwa adui wa HR ni adui wa viongozi wa Bara.
   
Loading...