sosoliso
JF-Expert Member
- May 6, 2009
- 8,539
- 9,462
Mwanamke aliefahamika kwa jina la Monika Mapoli (22), mkazi wa kijiji cha isima wilayani Geita, amekutwa amejinyonga juzi kwa kutumia kipande cha nguo karibu na Ofisi ya Mganga mkuu Wilaya ya Geita.
Taarifa ya mashuhuda wa tukio hilo zilisema kuwa Mapoli alichukua uamuzi huo baada ya kufiwa na mtoto wake Jumanne Philimo (2) aliekuwa amelazwa wodi namba moja katika Hospitali ya Wilaya ya Geita akipatiwa matibabu.
Ilielezwa kuwa baada ya mtoto kufariki dunia, mama huyo alitoweka wodini na kwenda kusikojulikana hadi alipokutwa amejining'iniza kwenye mti uliopo jirani na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dk. Omary Dihenga.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio Petro Majiasi aliekuwa kwenye wodi hiyo alisema chanzo cha kifo cha mtoto huyo ni huduma duni za matibabu zinazotolewa hospitalini hapo ambapo tangu mtoto huyo alipolazwa hakupatiwa matibabu hadi mauti yalipomkuta.
Akizungumzia tukio hilo, Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr. Nelson Bukuru, alithibitisha kumpokea mtoto huyo saa 7 mchana juzi akisumbuliwa na homa ya mapafu lakini kutokana na uhaba wa dawa za kutibu ugonjwa huo walilazimika kumlaza wodi ya watoto ili taratibu za kupata dawa za kutibu ugonjwa huo zikifanyika. Alisema kabla ya kupatikana kwa dawa hizo mgonjwa alifariki dunia akiwa amelazwa wodini chini ya uangalizi wa wazazi wake na katika hali ya kusikitisha kulipopambazuka walikuta mwanamke huyo akiwa amejinyonga na kuning'inia juu ya mti ulio ndani ya Hospitali hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Jeshi la Polisi bado linaendelea na uchunguzi..
Source: Mwananchi
Mytake..
Moja ya sababu za msingi za madaktari kugoma ni ukosefu wa vitendea kazi na dawa mahospitalini.. Mgonjwa mmoja zaidi amefariki kutokana na kukosekana dawa na kupelekea mzazi wake mwenye uchungu kuamua kujinyonga.. Hawa ni wawili tu kati ya wagonjwa wengi wanaopoteza maisha kutokana na siasa kuingiliana na utendaji.. Mungu awapumzishe kwa amani huko waliko..