Kaizer
Platinum Member
- Sep 16, 2008
- 25,320
- 17,822
marhabaaaaaaaa!
Shkamoo!
marhabaaaaaaaa!
Shukran snowhite. Mashallah nipatapo siha njema sifa zikuendee mwalimu wangu, mi bawabu tu ila tende naitia mdomoni hamad imekuwa halua! Alhamdulillah! Pema........ukipema si ........
Ha ha ha, usinifanye nikakopi nikajidai nimetunga mwenyewe
Hili shairi liko kimahaba zaidi, sema watu tumekipuuza kiswahili, nacho kimetuacha
Sasa tunarudi kukilaumu
Sasa hivi kizazi cha leo, hata kuzingatia mizani na vina kwenye ushairi ni ndoto, sababu ya uchache wa misamiati tunayoijua.
chai ya mkandaa ni chai ya mkono mmoja!
Kiswahili ukikijua kinanoga hasa. Na ndo unakuwa kama Dr.Riwa ukiambiwa kwa Kiingereza unaona fake.
Tatizo la siku hizi utandawazi umechukua nafasi ya kila kitu. Watu walikuwa wakitumiana mashairi ya Kiswahili katika kutafutana uchumba, siku hizi tunamtafuta Adele sijui Rhianna!
Watu walikuwa wazuri wa kueleza hisia zao hasa za mapenzi kwenye tungo.......mcheki huyu anaelalamika. Hata ukimaliza kumsikiliza lazima umfikirie namna ya kumkubali maana inaendana na mazingira ya kikwetu zaidi
Si kitu kunipuuza, kwako tamaa sikati
Fikira sitogeuza, moyo wangu madhubuti
Nilani utavyoweza, lakini sikubanduki
Wajua nnakupenda, ndo mana waniringia
Unanifanyia inda, mapenzi kunisusia
Baada ya hichi kidonda, na moto unanitia
Nikimbie japo mwaka, nipo ninakungojea
Ukirudi nakutaka, wala sitoona haya
Kukupenda sitochoka, japo ukinizomea
Kiswahili ukikijua kinanoga hasa. Na ndo unakuwa kama Dr.Riwa ukiambiwa kwa Kiingereza unaona fake.
Tatizo la siku hizi utandawazi umechukua nafasi ya kila kitu. Watu walikuwa wakitumiana mashairi ya Kiswahili katika kutafutana uchumba, siku hizi tunamtafuta Adele sijui Rhianna!
Watu walikuwa wazuri wa kueleza hisia zao hasa za mapenzi kwenye tungo.......mcheki huyu anaelalamika. Hata ukimaliza kumsikiliza lazima umfikirie namna ya kumkubali maana inaendana na mazingira ya kikwetu zaidi
Si kitu kunipuuza, kwako tamaa sikati
Fikira sitogeuza, moyo wangu madhubuti
Nilani utavyoweza, lakini sikubanduki
Wajua nnakupenda, ndo mana waniringia
Unanifanyia inda, mapenzi kunisusia
Baada ya hichi kidonda, na moto unanitia
Nikimbie japo mwaka, nipo ninakungojea
Ukirudi nakutaka, wala sitoona haya
Kukupenda sitochoka, japo ukinizomea
Waoh, nisingefikiria huko kabisa. Duh, asante mwalimu!
So 'mkandaa' maana yake nini exactly, wapi tena naweza tumia hilo neno?
Naweza sema wali wa mkandaa nikimaanisha wali usio na mboga?
Walah, asingekuwa memba wa JF, hii kitu ningeiba (with your permission ofcourse) na kumtumia mupenzi wangu, ningepataje maujiko! LOL
manta khofu!
mahamri ntayatia tui bubu na mkate wa bafta pembeni vipi?utafaa?
kisha ntakuandalia mkekani juu nimefunika kawa yenye rangi ya samawati
halafu nakukosha mikono kisha nikukaribishe ,ukishamaliza ntakupa maji ya sharbat yenye barafu kidogo na limao kuhanikiza hirmu!
Mkandaa kwa maana ya moja kwa moja ni mti aina ya mkoko ambao majani yake yanatumiwa kupikia chai.
Chai yake inakuwa ile watu wengine wanaita "chai ya rangi"......yaani ya kahawia iliyokuwa haijaongezwa maziwa (japo inaweza kuwa imeongezwa viungo kama tangawizi, hiliki, mdalasini)
Kwa hiyo, neno mkandaa ni mahsusi kwa chai na huwezi kulitumia kwa chakula chengine chochote ila unaweza kulitumia wakati unapofananisha vitu vyengine na chai hiyo
Kwa kweli kuna kitu kinatakiwa kufanyika tena kwa jitihada za makusudi
Kiswahili kisipopewa kipaumbele kitakwisha kabisa
Nakumbuka nikiwa darasa la saba ilikuwa tunafundishwa ushairi na kuandika
Sijui kama hii bado ipo shuleni siku hizi
umeona enh!mie tena kwako weye we lete tu nia mie nikufanyie mambo!navopenda kuchagua rangi za harusi mie!shurti chanikiwiti ichanganywe na rangi ya maji ya sharbati ya chungwa pamoja na zambarau au samawati!walahi tutapendezaaaje!Tutaaongea biashara PM, ukinitumia shairi kama 3 hivi piemu lakini; mbona ndoa itakuwa within a month. LOL
Yaani hapo nilicho elewa ni hayo kwenye bold tu, mengine yote ni 0.
Yaani hapo nilicho elewa ni hayo kwenye bold tu, mengine yote ni 0.
ahhhhhhhhh pole maamii!huo ndo utamu wa kiswahili kunako mahaba mwali!
manta khofu ni usiwe na khofu
mahamri ni maandazi
mkate wa bafta huwa ni mlaini hivi una kuwa na ngano yako maalum
nitakuandikia maana yake nitakuandalia
samawati ni rangi ya bluu bahari
maji ya sharbati ni juice
kuhanikiza hirmu ni kukoleza harufu (nzuri)