Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,267
- 105,437
Mimi hicho kiswahili cha wasemaga na hakunaga wala sikijui. Nina imani kiswahili changu kinatosha kufahamu yaandikwayo. Sisemi kama ina walakini bali haina ladha au hamasisho kwenye mapenzi nionavyo mimi, Maana kuna lugha nyingine ambazo zipo kimapenzi zaidi yaani yana sweets words kuliko kiswahili hapa simaanishi kizungu.
Kumbe unaongelea mambo ya imani? Kwamba una imani Kiswahili chako kinatosha kufahamu yaandikwayo?
Hata R. Kelly ana imani anaweza kuruka kama ndege, imani si kazi.
Nimekuuliza umesoma tenzi gani ukaiona ina mapungufu ya kukosa ladha? Hujanijibu.
Huwezi kuwa George Bernard Shaw, H.L Mencken au Edmund Wilson au hata mfungakamba za viatu vyao katika fasihi, wa kukisema Kiingereza kama hujasoma vitabu na kuweza kuchambua tenzi na riwaya. Vivo hivyo kwenye Kisahili na magwiji wake.
Nataka kuona hoja inayotokana na uchambuzi wa lugha, si maoni rejareja yanayotoka kwa watu ambaoa inaonekana wazi hata kutaja tenzi moja tu waliyosoma inawawawia vigumu.