Ukosefu wa 'Kichwa' Katika Diplomasia ya Tanzania

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,586
1,678
Leo nataka nizungumzie diplomasia ya Tanzania, au kama kitu kama hicho kipo! Sijui ni uvivu wa kufikiri au ni ukosefu wa taaluma, niambieni.
Katika miaka ya sitini, sabini na themanini Tanzania ilikuwa kiongozi wa nchi za msitari wa mbele wa mapambano dhidi ya ukoloni na apartheid. Msimamo huo uliigharimu Tanzania, nchi maskini, mabilioni ya dola na raia wake kuendelea kuteseka ili 'kuwaokoa' ndugu zetu. Mwisho wa mapambano hayo ulifika na zaidi ya sifa tele tele sijui kama Tanzania iliambulia kitu. Sababu kubwa kwa maoni yangu ni kuwa hakukuwa na mtu katika diplomasia yetu mwenye 'kichwa' cha kupanga na kuwalea allies'wandani' wetu katika mfumo mpya. Matokeo yake hatukuambulia chochote kiuchumi na hata kisiasa.
Basi afadhali zama hizo kulikuw na hata waliokuewa na aina ya mipango ya mbele ingawaje hawakuendela na kushirikisha uchumi na uongozi wa mustakabali. Hivi sasa ni vurugu mechi tu, hakuna diplomasia yeyote: tumekosa fursa nzuri ya ushawishi huko Sudan ya Kusini na mpaka sasa sijui kama tuna ubalozi huko. Fananisha na Kenya ambayo inavuna mabilioni kiuchumi na kisiasa kutokana na kuwekeza kwake huko na kuwa na mipango ya mustakbali.
Angalia Somalia. Tuna nini huko? Sasa ngojea jinsi Kenya itakavyohodhi biashara na siasa za Somalia.
Kwa kweli kwa kusafiri kwangu katika maeneo yanayozunguka Afrika Mashariki, hakuna nchi inayopendwa zaidi kama Tanzania kutokana na siasa zake za miaka ya 60, 70. Kila viongozi niliokutana nao watakusimulia wanavyomheshimu 'mwalimu' na mchango wa Tanzania.....halafu watakuuliza, kweli rais wa sasa ni nani vile....?
 
Watawala wa leo wako busy kuiba na kutafuta wapi pa kuficha,muda wa kujenga Tanzania yenye heshima ndani na nje ya bara la Afrika hakuna,watawala wanaamini ili kuendelea lazima uwekeze kwenye kuomba misaada,lazima ujipendekeze kwa watu weupe ndipo uonekane una maana.
Wakati wenzetu wakitumia mwanya wa diplomasia kukuza uchumi wa nchi zao WaTZ tuna tumia mwanya huo huo wa kidiplomasia kuomba na kujenga mazingira ya kuibiwa na wageni.Imefika wakati hata wanaotuibia wanashangaa how cheap wa are.
Bado tumepoteza dira,hatujielewi tulipo na wapi tungependa kwenda.Tumeshindwa kujenga uchumi kwa mlango wa diplomasia na sijui tuna tatizo gani hasa katika eneo hili japo jibu la haraka ni Watawala wetu tatizo la kwanza.Viongozi wetu wamekuwa na mwenendo usio pendeza kabisa maana wapo kwa kimaslahi binafsi zaidi kuliko vinginevyo,wao wakisikia kwamba kuna chochote watapata basi akili zinapoa,wanajivua ufahamu na kujitoa utu wao na pengine kusahau hata kusahau wajibu wao tulowapa kama viongozi.
Ushauri ni kwamba we need to overhaul the whole system then tujenge mfumo ambao katiba yetu itatuelekeza kufanya.
 
Back
Top Bottom