"Ukosefu wa Fedha Unakwamisha Maendeleo" Lakini za Posho Zipo!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Ukosefu wa Fedha Unakwamisha Maendeleo" Lakini za Posho Zipo!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sizinga, Jun 22, 2011.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Sio siri kwamba Rais Jakaya Kikwete anapenda sana kusafiri.Kuna vijimikutano vya kimataifa mbavyo kwa hakika visihitaji Tanzania iwakilishwe na Rais na badala yake akaenda Waziri Mkuu au kwa stahili kabisa Waziri wa wizara husika.Lakini asipokwenda yeye,watajuaje kama Kikwete ndiye Rais wa Tanzania?


  Tuweke hilo kando.Tatizo jingine la Kikwete ni kutoa kauli ambazo yayumkinika kuamini kuwa hazijafanyiwa tafakuri ya kutosha.Huku nyuma,alishawahi kusema haelewi kwanini Tanzania ni masikini,na Waziri Mkuu wake,Mizengo Pinda, akaakisi kauli hiyohiyo.Sasa kama Rais hajui chanzo cha umasikini wa nchi anayoongoza,anafanya nini hapo Ikulu?


  Safari hii kaibuka na madai kwamba kinachokwaza maendeleo yetu ni ukosefu wa fedha.Fedha zipi hizo?Mbona yeye kiguu na njia huku safari zake zikilibebesha taifa mzigo mkubwa wa gharama?Na fedha zipi anazozungumzia ilhali wabunge wetu wanalipwa mamilioni ya posho kwa "ku-rubber stamp" kila kinachowasilishwa kwao na serikali huku jitihada kubwa zaidi wanayofanya ni kubamiza meza (pongezi) kama sio kuwazomea wabunge wa upinzani na kulala wakati wa bunge(Wassira)?

  Sasa cha kushangaza baada ya KUB kudai ziandaliwe form 2 za kusigh posho na mahudhurio, sasa Waziri Mkuu anataka kuambatanisha Posho kwenye mishahara yao-kukata mzizi wa fitna!!

  From Chahali
   
Loading...