Ukosefu wa bunge makini, ukosefu wa umeme nchini

Nyauba

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
1,098
108
Kukosekana kwa bunge imara lenye maono yakinifu yamepelekea taifa kuingia katika janga la ukosefu wa uhakika wa nishati ya umeme, utendaji mbovu wa TANESCO na kuongeza machungu ya maisha kwa wananchi.

Baada ya kamati teule ya bunge kugundua upungufu wa kampuni ya RICHMOND katika uwezo wake wa kuzalisha umeme kwa TANESCO na kutoa mapendekezo 14 ambayo hayakutekelezwa na serikali na bado bunge likaufunga mjadala ule KIHUNI leo hii yanaoyojiri ni kielelezo cha bunge lisilo makini.

hatimaye DOWANS waliirithi RICHMOND wameshinda kesi dhidi ya Tanesco ya fidia ya mabilioni kwa sababu tuu ya maamuzi ya kisiasa yalizongwa na unafiki zaidi wa wabunge hasa wa chama tawala kwa kuendekeza fitina zaidi na kulindana.

natumai spika alitaambua athari za mkataba huu wa DOWANS na bado akakubalii kihuni kuufunga mjadala ule ndani ya bunge kwa style isiyoelezekaaa sehemu yeyotee. Mh mwakyembe kama mwanasheria natumai pia aliitambua athari za kuvunja mkataba lakini bado hakushauri njia mbadala au kuonyesha msimamo binafsi hata kama serikali haikutaka kukubaliana naye.Nampongeza Mpendazoe aliyepingana na serikali katika mambo yale ya ufisadi likiwemo suala la mjadala wa Richmon.

Lowassa alisema wakati anajiuzulu tatizo lilikuwa uwaziri mkuu, na hilii lilithibitika kwani katika maazimio yale 14 hakuna liliofanyika. huenda kamati ile ya Bunge ilifarijika tuu EL alipoachia ngazi lakini leo athari za mkataba ule bado ni mzigo kwa watanzania wasiokuwa na hatia.

Je Mh sitta leo anaweza kutoa ufafanuzi kuhusu fidiaa hii ya DOWANS waliyoshinda? Je mwakyembe pia analizungumziajee suala hilii hapa lilipofikia? Natumai wao sasa ni sehemu ya serikali na wanatekeleza uwajibikaji wa pamoja. JE NAFASI ZA UWAZIRI NDIZO ZILIKUWAA KILIO CHAO?????

Mahitaji ya utenganishaji wa bunge,serikali na mahakama kwa uwazi unahitajika zaidi hasa kupitia KATIBA MPYAAA.
 
Back
Top Bottom