Ukosefu wa ajira Tanzania na mfumo wa elimu yetu

kopundo

Member
Nov 8, 2011
8
0
Wana JF!

Hivi ni kweli kuwa kuwa ukosefu wa ajira hapa kwetu Bongo unasababishwa na mfumo wetu duni wa elimu ambao bado unazingatia na kusisitiza zaidi kazi za kuajiriwa na za ofisini licha ya ukweli kwamba kazi hizo sio rahisi kupata kama zamani?

Mimi nadhani kuna haja ya kubadilisha mitaala yetu ya elimu kuanzi msingi hadi vyuoni ili ufundishaji uweze kufanana na hali halisi ya soko la ajira au iweze kusisitiza zaidi kujiajiri badala ya kuajiriwa.

Je, mnadhani mtisiko wa uchumi unaokumba nchi za Ulaya na USA ndio chanzo cha ukosefu wa ajira hapa kwetu au ni mipango mibovu ya serikali kutokuwa na sera nzuri ya nishati ya uhakika na usimamizi wa sekta ya uzalishaji viwandani na mashambani?

Kwa upande wangu,naamini without reliable source of energy,no nation can flourish in having both industrial production and agricultural development that can stimulate economic development which in turn results into vast employment opportunities?

Do you guys think those in power do not adequately safeguard the employment opportunities we have in the country?Anyone is welcome for comments and suggestion!

Wako,
Desperate job seeker
 
We jamaa una IQ kubwa sana,Tz mtu akihitim elimu hata kujenga kibanda chaa kuku hawezi.Nchi integemea kilimo somo la lazima kusoma GS huu ni ukosefu wa fikra
 
Vijana wengi wa Kitanzania,wanasomea vyeti na sio ujuzi.wanagezea,wanaingia na majibu kwenye vyumba vya mitihani,wananunua paper fake ilimradi wafaulu.Ukweli unabakia palepale kama ujui ujui,matokeo yake wanashindwa intaviews na awawezi ajiriwa!.ukweli cjaona yeyote aliyefauli kiukweli ukweli akitafuta kazi zaidi ya miezi sita!.Wengi wa wanaotafuta kazi muda mrefu ni either ajafauli kiukweli ukweli,au fani aliyosomea wapo wengi sokoni.Utakubaliana na mimi kuwa kuna fani ambazo ajira zake azipo nyingi, SAUT na UDSM zina zalisha watu wa Public Relations zaidi ya 200 kwa mwaka,utakubaliana na mimi kuwa kila kampuni huwa na PR mmoja tu!,je kwa mwaka Tanzania inaanzisha kampuni ngapi,ili hawa 200 wapate ajira?.Kuna mapungufu mengi sana ktk serikali yetu pia,kama unaangalia TBC wakati wa kipindi cha ze komedi kuna matangazo ya shule zaidi ya 4.zote zinatoa kozi za hotel,je hawa wote wanaenda wp?ni hotel ngapi?zinajengwa kwa mwaka?
 
We jamaa una IQ kubwa sana,Tz mtu akihitim elimu hata kujenga kibanda chaa kuku hawezi.Nchi integemea kilimo somo la lazima kusoma GS huu ni ukosefu wa fikra

kipi kinachoshangaza? Huyo mtu alikuwa anajifunza kujenga kibanda cha kuku? Hiyo nayo inahitaji kuwa na degree?
 
Back
Top Bottom