Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,192
- 3,353
Mzungu aliwahi kusema "scarcity is expensive: uhaba wa kitu unaongeza thamani, Ndivyo ilivyo katika soko la ajira, Hapo zamani uhaba wa watu wenye degree uliwapa soko kubwa na walilipwa vizuri na ajira ilikuwa sio tatizo kabisa. Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la watu wenye degree kiasi kwamba huo wingi wa digrii umepunguza thamani ya soko la ajira kwa watu wenye degree.
Baadhi ya wajasiriamali wanatumia mwanya huu kupunnguza gharama za uendeshaji wa biashara kwenye kitemgo cha mishahara kwa kuwalipa wafanyakazi wao mshahara kidogo sana kwa sababu wanajua tayari soko la ajira limekuwa gumu kiasi kwamba wapo wanaojitolea bure na endapo wafanyakazi wao wataleta viburi wala hakuna shida kwa sababu kuna lundo la wahitimu ambao ukitangaza ajira leo basi haipiti hata siku kupata lundo la wahitimu wataongombania nafasi za kazi zinazotangazwa.