Ukosefu wa ajira na yaliyonipata.

Hyungnim

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
301
500
Habari za wakati huu watanzania wenzangu.

Jana nilifanikiwa kupata rekodi ya sauti juu ya kilichozungumzwa na 'mkuu' akiwa ziarani Bukoba kuwaona waathirika wa tetemeko.Sio siri nilikumbwa na hofu,kihoro na mwisho huzuni ikanivaa."Hakuna chakula cha msaada,mkuu wa wilaya mimi sileti chakula hapa....".Kama binadamu nilisikitika mno.Kutamka vile inahitaji ujasiri na moyo mgumu sana.Ila ujasiri wa ajabu ni wa wale wananchi waliokuwa wanacheka,kupiga makofi na kushanhilia maneno makali yale yasiyotia tumaini!lipi la kuchekesha?kwamba sitawajengea nyumba?au neno mwafwa?jamani mbona hayachekeshi?na vile yalivyokosa usanaa ndani yake na kutamkwa kwa ukali na vitisho nadhani watu walipaswa kukimbia kwa hofu!.

Nilizifuta haraka zile rekodi zs sauti(za mkuu) kisha nikajigeukia upande wangu.Nikaumba taswira yake akiwa anahutubia umati mkubwa wa wahitimu wa ualimu ngazi ya cheti,stashahada na shahada masomo ya sanaa.Ndani ya umati huo nipo mimi nikiwa nimevalia mavazi kuukuu(suruali imejazwa viraka makalioni ambavyo pia vimekosa adabu.Eti kwa kejeli huamkiana shikamoo kiraka.cha kalio la kushoto kikimsabahi sahibu yake wa kalio la kulia).Viatu vilivyokwisha upande na shati la mikono mifupi rangi ya mauamaua lililopambwa picha za njiwa lililosopekwa kwenye suruali njiwa yangu .Uso umechakaa kwa kujazilizwa na ndefu nyingi,zilizosokotana mithili ya brashi isuguayo sakafu ya vyoo vya uma!

Taswira ya mkuu inaendelea kurandaranda kichwani mwangu,namuona akiyageuza maneno ya Bukoba ili yatulenge sisi.Kwa ukali anang'aka "hakuna ajira za waalimu wa masomo ya sanaa!waziri wa elimu hakuna ajira!serikali haina ajira!kuna watu wamehitimu tushahada twao tudogo tena TWA masomo ya sanaa wabasubiria ajira,nawaambia mwafwaa....kufikia hapo mapigo ya moyo yananifukuta,macho nayatoa pima na kutahamaki watu wanakimbia kwa hofu,nami naanza kuzichanga hatua za miguu 1,2,3....miguu inagota kisogoni.Kihoro.Anaogofya.

Ghafla najikuta nipo peke yangu nje ya kajumba kangu ka mianzi kalikoezekwa kwa mianzi.Kumbe ulikuwa ni mzugo wa fikara tu!lakini ukweli mchungu haufutiki,ajira hakuna.Kiwahili na historia ni masomo ya sanaa,ingawa ktk baadhi ya kozi za kiswahili nimefunzwa sayansi ya lugha(Isimu) lakini Waziri wa elimu hakuitaja!Alitaka zile sayansi pyua(pure) zenye makemikali na ukokotozi ndanu yake.

Nikiendelea kubung'aabung'aa mithili ya zuzu ghafla anakatiza Shani binti Mwamanyeghesi.Kaloa na mvua,hana mwanvuli hivyo anasogea ajibanze upenuni pangu.Kaloa chapachapa.Mavazi mepesi mafupi aloyatinga yanagandamana mwilini mwake.Na lile umbile nene lenye shibe,umbile la kinyakyusa ananihamasisha kutenda uovu.Haraka sana mawazo ya ukosefy wa ajira yanapotea.Yaani kwa mda ule ningeulizwa kitenzi kisaidizi ni nini ningejibu sahani!tayari nilishakuwa Zuzu.

Ananijia kwa kunesanesa tena kinyumenyume kanipa mgongo na kuacha nifaidi kuangalia rasilimali makalio yake.Ananesanesa na kuyayumbisha makalio yake kwa nguvu.Naam makalio makubwa yaliyovirigwa mfanowe wa tufe!mviringo makini,sio pembetatu.

Kitu mfanowe wa mzizi wa mmea wa kisamvu kinamea taratibu na kuchomoza maungoni.Sasa ni dhahiri nimehamanika!utimamu wa akiki umeyeyuka.Ubongo hauchakati mambo kwa usahihi.Ninaanza kutamka maneno ambayo kwa muktadha ule hayana maana!Naam muktadha wa kutamani kumlaza Shani kwenye chano.Nimtie na saladi,kitunguu maji,asali,tambuu na bagia nimfaidi.Naanza kutamka "mzuri...kivumishi,...sentensi....faru....waarabu....kamusi.Nikidhani nipo kufundisha kiswahili kidato cha tatu.

Shani ananifikia na kunibamiza na makalio yake maungoni.Kijasho chembamba kinachuruzika kwapani,maungoni na kwenye meno na kutoa harufu ya kuudhi.Anatoka upenuni kisha anautikisa mwili wake kwa nguvu.Ananisonya kwa dharau na kudokeza "...tafuta hela unifaidi.Ila ukipata ajira tuu ntahamia hata kwako".Anaondoka kwa mbwembwe huku kaniacha nikiyakereza meno kwa utamu wa haja.

Akiisha kutokomea ndipo utimamu wa akili unarejea.Naanza kujuta.Najutia kuropoka neno faru kipindi nilipochafukwa .Hofu inanitawala,nisijeitwa mchochezi.Kwa haraka nafuta mawazo hayo kwani Subira Mwamambolesi kaja 'geto' kwangu nimfundishe kiswahili. Najiweka sawa asijeona maungo yalivyochemka....
 

Hyungnim

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
301
500
ok. kajiajiri ndo suluhisho
si Nazi rahisi na ya ghaflaghafla!inahitaji mazingira rafiki ya muda mrefu.Hao kina jafo,simbachawene,ndalichako,na wabunge wengine wamejiajiri?wote si waajiriwa?kama wamejiajiri basi mitaji na channels za kujiajiri wamepatia serikalini.
 

mdau mpya

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
452
1,000
si Nazi rahisi na ya ghaflaghafla!inahitaji mazingira rafiki ya muda mrefu.Hao kina jafo,simbachawene,ndalichako,na wabunge wengine wamejiajiri?wote si waajiriwa?kama wamejiajiri basi mitaji na channels za kujiajiri wamepatia serikalini.
labda subiri tu 2020
 

Jics

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
234
500
siyo 2020 bali ni 2019 ili tumpe ridhaa ya kurudi tena
nb:usikate tamaa naye ni binadamu anaweza kuingiwa na moyo wa huruma na kuwaajiri wote
si unaamini miujiza amini chochote chaweza kutukea
 

Kashindi

JF-Expert Member
Oct 28, 2011
347
250
ffirst to reply. uandishi mzuri, uchaguzi wa maneno na misamiati ni mzur pia. hongera mwalimu. lakini ndo hata hauhitajiki.
 

laki si pesa.

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
10,020
2,000
Ajira za nini wewe jiajiri acha uvivu wenye ajira nchi hii hawafiki hata milioni moja wakati Watanzania wako milioni 40.....jiajiri acha uvivu
 

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
13,998
2,000
Hata mkipiga kura ya kumkataa hapo 2020 na ili hali hakuna tume huru ya uchaguz ni kazi bure

Immagine chairman of electoral commission kateuliwa na yeye na jeshi lote lipo chin yake kuna nin hapo?

Mwafwaaa kweli kweli.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom