George Kahangwa
JF-Expert Member
- Oct 18, 2007
- 547
- 147
Kuna mkutano moja wa kimataifa ulifanyika na kuhudhuriwa na wawakilishi wa wizara ya kazi. Jamaa walikuwa wanawakilishi matokeo ya utafiti wao nikawa napigwa butwaa na findings zao. Jumla ya vijana wanaomaliza shule kuanzia primary, secondary na vyuo vikuu only 3% of the population ndio wanaajiriwa kila mwaka. Inamaanisha 97% YA VIJANA HAWANA KAZI Hii figure ni hatari sana na inatisha. Hebu jisomee mwenyewe power point presentation ya watafiti hao katika link hapo chini.
http://info.worldbank.org/etools/docs/library/135839/Tanzania.pdf
Tanzania kazi za kufanya zipo, nafasi za kazi zipo (zipo zinazotumilka na zipo zilizolala tu), nafasi za ajira zipo ila hazifikiki. Kwa hiyo tatizo ni sera, ndio maana kuna ukosefu wa ajira na kazi kwa watanzania wengi vijana. Hapa ndipo pa kutumia akili, hili tatizo linawezekana kabisa kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kama sio kuliondoa kabisa. Bahati mbaya hadi sasa mheshimiwa anasema tu kuna tatizo na halina budi kutatuliwa, labda kwake ni mapema muno kusema litatuliweje (anaficha sera?)