Ukoo wa mareale wachapana makofi kugombaniaa umangi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukoo wa mareale wachapana makofi kugombaniaa umangi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jun 22, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,613
  Likes Received: 5,782
  Trophy Points: 280
  POLISI wa Kituo Kikuu cha Polisi Himo kilichopo Wilaya ya Moshi vijijini mwishoni mwa wiki walivamia na kuvuruga kikao kilichoandaliwa kwa lengo la maandalizi ya kumsimika Frank Marealle kuwa Mangi wa Wachaga wa Marangu.

  Hatua ya polisi kuvuruga kikao hicho ilifuatia malalamiko kutoka Ofisi ya Kijiji cha Lyamrakana wilayani humo juu ya kuwapo hali ya uvunjifu wa amani endapo kikao hicho kingeruhusiwa kufanyika.

  Taarifa ya Polisi Himo ya Juni 18 mwaka huu, kwenda kamati ya kumsimika Frank Marealle kuwa Mangi wa Marangu ilisema kuwa, pamoja na Serikali ya Kijiji cha Lyamrakana kutokuwa na mamlaka ya kuingilia taratibu za kijadi kwa kabila lolote, lakini polisi wamelazimika kuingilia hali hiyo ili kuleta amani.

  “Kimsingi ofisi hii haipaswi kuingilia utaratibu wa kijadi wa kabila lolote, lakini kwa vile malalamiko haya yameletwa kwetu na kutoa hadhari kwamba kunawezekana kabisa kutokea uvunjifu wa amani katika kikao hicho, tuna kila sababu ya kusitisha kikao hicho kama walinzi wa amani,”ilisema barua hiyo.

  Polisi walitahadharisha kuwa, kama walinzi wa amani hawatopenda kuona kunatokea uvunjifu wa amani na kushauri wanaoendesha kikao hicho kukaa na uongozi wa Serikali ya kijiji ili kutafuta ufumbuzi na kuhusisha pande zote.Hatua ya polisi kufuta kikao hicho, ilifuatia kusambazwa kwa barua za mialiko ya kuhudhuria kikao cha maandalizi ya kumsimika Frank Marealle kuwa Mangi wa wachagga wa Marangu kinyemela licha ya wanaukoo wa Chief Thomas Marealle II O.B.E, kutotambua harakati hizo kwa kuziita ni batili zenye lengo la kuyumbisha mila na desturi za ukoo huo.

  “Somo hapo juu linahusika,hudhuria kikao cha kamati ya Jumapili Juni 19, mwaka huu saa 7.00 mchana, kikao kitafanyika pale kwa Dk Wilfred Marealle saa 7.00 mchana, tafadhali zingitia muda, pia Mangi mtarajiwa Frank L Mlanga atakuwapo hivyo zingatia muda uliopangwa,” inasema barua hiyo iliyosainiwa na Frank Nyaki kama mwenyekiti wa kamati.

  Polisi walizuia kutoendelea kwa kikao hicho kilichokuwa kikifanyika nyumbani kwa Dk Wilfred Marealle katika Kijiji cha Lyamrakana Marangu kikao ambacho hata hivyo kinadaiwa kuandaliwa na watu wasiokuwa wana ukoo wa Marealle kutoka Kijiji cha Marangu Rauya zaidi ya kilometa saba kutoka Kijiji cha Lyamrakana.

  Hivi karibuni baadhi ya wanafamilia wa Ukoo wa Chief Thomas Marealle II, walikutana na kutoa tamko la kutotambua harakati hizo za Frank kujitangaza kuwa Mangi wa Marangu na kumchagua Teddy Marealle kuwa mwenyekiti wa muda wa uko huo hadi Desemba 28, mwaka huu kitakapofanyika kikao cha wanafamilia wote walioko ndani na nje ya nchini.

  Akitoa tamko mbele ya waandishi wa habari na wanafamilia hao Teddy alisema vikao hivyo ni batili na kwamba vina lengo la kuleta mgawanyiko ndani ya ukoo na kuongeza kuwa,taratibu za kumpata mangi wa Marangu kurithi nafasi ya Mangi Augustine Marealle mdogo wake na marehemu ,zitafuata taratibu za kimila na kitamaduni .

  Mangi wa Marangu alikuwa ni Augustine Marealle ambaye alizaliwa Januari Mosi mwaka 1921 na alifariki dunia Novemba 26 mwaka 2006 wakati huo kaka yake, Chief Thomas Marealle II O.B.E, alikuwa mangi Mkuu wa wachagga wote enzi za utawala wa ki-chief. Tamko hilo la Ukoo wa Mangi Marealle lilitolewa mbele ya viongozi wa serikali ya Kijiji cha Lyamrakana wakiongozwa na Ofisa mtendaji wake, David Mkusu, mwenyekiti wa kitongoji cha Lyamrakana, Albert Mtui, mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama na mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji, Daudi Lyamuya.

  Wajumbe wengine wa Serikali ya Kijiji cha Lyamrakana waliofuatana na mwenyekiti wao ni Ernest Tilia Dresfori Kessy na Robson Kitali ambao waliunga mkono tamko la mwenyekiti wao la kutotambua uwapo wa makundi mawili katika ukoo wa Marealle.

  Kwa upande Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho,alisema Serikali ya kijiji chake haitakubali kutokea kwa uvunjifu wa amani katika kijiji hicho kutokana na watu wachache kuendesha shughuli za siri bila kuhusisha Serikali ya kijiji.
   
 2. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  badala watu watwangane kwa mambo ya maana, eti uchifu wa kikabila....bullshit.
   
 3. babuwaloliondo

  babuwaloliondo JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Waanjoooooooooo bwana wanamambo ya kizamani sana,
   
 4. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,971
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  this is just another family feud being publicized
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Msihusishe CHADEMA na huu uchagga tafadhali
   
 6. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Duuh...nawajua wote hawa, wamenikumbusha 'mn'denyi'! Lakini of all people Frank Marealle awe mangi wa Marangu? Huni lile limejaa jeuri na kiburi hakuna kila biashara yake inabuma...Kibo Hotel inakufa, Embassy Hotel imekufa, Wami bar chali...sijui hotel gani tena Moshi mjini hamna kitu! Hata ndugu zake hawamkubali ndio itakuwa waMarangu?!
   
 7. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Ukitaka kujua mtu amefilisika utamwona anaanza kutafuta vi-TITLE vya ajabu ajabu ili kumaintain
   
 8. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Is Tanzania still practising Chiefdom? sasa kama ipo si iruhusiwe tu ijulikane kama inavyofanyika Uganda...wenzetu wanayo na wanahold powers over Museveni,kama ni mazuri basi tuyarudishe kwa mpango maalum

  Mwenyekiti amepanga tarehe nyeti kabisa make Desemba is also a statistical month to these comrades..big up!
   
 9. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Patakuwa hapatoshi...maana Dar na Arusha yote huwa inajaa hapo Marangu, watahitaji FFU kama kutakuwa na upuuzi upuuzi!
   
 10. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,136
  Likes Received: 6,630
  Trophy Points: 280
  kila kitu kina posho yake na ndiyo maana wanazipiga.
   
 11. L

  LAT JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  hvawa ni vishoiya
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Hivi Mbowe si Marangu! Wachagga wanapenda vyeo sana sijui kwa nini, ata ukiangalia wenyeviti wengi wa vyama vya siasa ni Wachagga
   
 13. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mbowe ni machame acha kubahatisha
  hawa jamaa wana wazimu,wanaamini watapata heshima kwenye kizazi hiki?
  wamekosa kazi ya kufanya
   
 14. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... big up Mkuu Camaraderie, uhafidhina wa hawa jamaa kugombea ile ngozi ya chui na kichwa chake usiwapake tope wengine ndani ya nguvu ya umma. By the way, kuna jungu moja chafu sana kuhusu huyoo anayetaka umangi. Manake kama ni yule mwenye property pale maili sita, basi tangu lini mangi akawa wa jinsia tofauti na ...? Mmh kama ni kweli aibu tupu!
   
 15. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  tena si kidogo ati!!
   
 16. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,697
  Likes Received: 429
  Trophy Points: 180
  Hawezi kuwa Mangi wa Wachaga, labda awe Mangi wa ukoo wa Marreale's family. Tujaribu kutofautisha mkuu wa ukoo na Mangi wa wachaga...
   
 17. M

  Marbomu Member

  #17
  Jun 22, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamaa ameona disemba ni mbali sana kusubiria
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  this is crap.... kesho tutakuja ambiwa shirima na mkewe wamegombana, wakaita babu na polisi kuamuli

  we have more serious things to deal with and not this family matter
   
 19. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #19
  Jun 22, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 522
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  heri kuongozwa na chief Frank kuliko kuongozwa na mhuni a.k.a mzee wa kuchekacheka
   
 20. pitbull

  pitbull JF-Expert Member

  #20
  Apr 8, 2013
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 45
  :rockon:
   
Loading...