Ukoo - CCM walivua gamba la Nyerere, Nape kaongelea CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukoo - CCM walivua gamba la Nyerere, Nape kaongelea CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, May 14, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  CCM walivua gamba la unyerere na kuvaa lao ambalo linakitesa chama na kwa kweli halivuliki kirahisi. Ukiangalia historia ya familia ya Nyerere hakupenda kuwaingiza watoto wake kwenye siasa au serikalini kwa mgongo wake, na hivyo heshima yake ilisheheni na kupevuka.

  CCM ya leo na viongozi wao ni tofauti na itikadi za mtazamo wa Nyerere, na ukiangalia safu ya uongozi utaona ni kile alichokisema Nape chama cha ukoo na viongozi wa ukoo kinyume na alivyoelekeza mashambulizi dhidi ya Chadema. Baba kabla hajang'atuka anamwandaa mwanawe kushika hatamu, na anapong'atuka ameshamtarisha na mwendelezo unakuwa wa mfumo wa kitemi. Haya yapo tunayaona kila siku lakini leo Nape anaelekeza kombora kwa Chadema wakati hakumbuki baba yake Moses Mnauye alikuwa kiongozi mwandamizi huko aliko.

  Mwingine ambaye huna mkubwa katika serikali na chama cha CCM vigumu mno kupenya maana huko inategemea jina la mtangulizi wako katika siasa au chama, vinginevyo utaishia kuwa msindikizaji.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Makamba anapong'atuliwa alishamwandaa mwanae na ameshika sehemu nyeti ya secretarieti, Mwinyi mwanae ni waziri, Nape baba yake alikuwa kiongozi mwandamizi, Kikwete mwanae kiongozi umoja wa vijana nk. huu ndio uongozi wa ukoo anaotakiwa Nape auongelee na una mizizi miaka mingi kulilko kuhangaikia chama ambacho hata hakijashika dola.
   
 3. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hili ulilolitoa ni angalizo zuri sana hasa kwa vile mwenendo huu unazaa dynasty ambayo ni hatari kwa ustawi wa taifa lolote. Hata hivyo siyo wote ambao ni watoto wa vigogo wamepata grooming na kuandaliwa kuwarithi. Wakati mwingine athari za kuishi maisha ya kukulia katika siasa huwa yanazaa interest kwa watoto na hatimaye unakuta na wenyewe wamekuwa wanasiasa. Hili lipo katika CCM na limepigiwa kelele muda mrefu sana. Sasa hivi hili limeanza kuwa tatizo kubwa ndani ya CDM na hasa ukizingatia kwamba chama hiki bado ni kichanga lakini kinachobeba matumaini ya baadhi ya watu. Kinachoonekana humu ni juhudi za makusudi za kuhakikisha kwamba wanafamilia siyo tu kwamba wanashiriki siasa, lakini wanapewa nafasi za juu za uongozi na kuwa sauti muhimu ya maamuzi katika chama. Mfano wa uteuzi wa viti maalum wa ubunge katika CDM yametoa picha hiyo kwamba watu wenye nasaba na wakubwa ndiyo wanaopewa vipaumbele. Hali hii ingekuwa na athari kimaamuzi CCM basi Nape, Kipi na wengine kadhaa wangepita kwa four wheel katika mchujo wa kura za maoni lakini wapi!

  CDM inahitaji kujitazama maana malalamiko haya yanazidi kukua na kuenea na kwa kiasi fulani yanatia hofu juu ya fursa za wengine ambao hawana god fathers.
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  kikwete wanae hawaishii kuongoza umoja wa vijana tu wanashuka hadi kwenye chipukizi wa ccm, ambao ni watoto. sasa sijui hii imekaaje watoto kufanya shughuli za siasa hebu wanasheria wa haki za watoto hapo tudadavulieni kidogo
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa mtazamo wangu Vyama vya upinzani bado vichanga sana, na pengine ni wachache ambao wamekuwa karibu na viongozi ndio wanaopewa nafasi, lakini hata hivyo vyama vichanga vina nafasi zaidi katika kuwapa wengi nafasi kuliko chama kikuukuu cha CCM ambacho kushika madaraka ya juu ni reserved for watoto wa vizito. Afadhali tuanze kunyoosha kidole kwa wale ambao wanazuia kabisa nafasi ya wengine kupenya. Nadhani ni rahisi kupenya chama cha upinzani kwenye uongozi kuliko ilivyo CCM kupenya ni sawa na ngamia kupenya tuntu la sindano
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Siri moja ya watu kukufahamu vizuri kiongozi ni hii. Uwafikie hao waongozwa huko waliko katika mazingira na maisha yao ya kila siku ndipo utakapojua vema matatizo na mtindo wa maisha yao. Kwa utaratibu huu watakuelewa na kuwa huru kueleza matatizo yao. Ukiweka ukingo kati yako na wao ni vigumu kuwapata na itawawia vigumu kukufahamu. Unatakiwa kiongozi usiwe juu yao, ila teremka uwafikie walipo.
   
 7. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #7
  May 14, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sasa hii imeingiaje humu kwenye mjadala huu wa watoto wa vigogo au kurithishana kwa nafasi za uongozi? Hivi unadhani pale Laela hata angetaka chakula kilicho bora na mazingira bora angepata wapi wakati hiyo ndiyo "hoteli yenye hadhi ya nyota tano"? It may also be a populist apporach which is very common to politicians. Bottom line ni kwamba vyama hivi viendeshe siasa above board na viongozi wake waache kujifikiria wao na familia zao tu!
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  May 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Mwaka huu tutashuhudia mengi maana tulijisahau na kuanza kuishi peponi bila kuwajali wavuja jasho. Namwona Kepten Chilingati kaamua kunyanya sululu kuteremkia mtaroni kwa ajili ya kupata picha ya kujinadi kwamba naye yumu.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  May 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Laela ni kituo kikubwa ambacho huwezi kukosa sehemu ya kupata sahani ya wali na samaki wa kutoka Ziwa Rukwa. Na hata ungeniambia kule Mpui bado ni sawa na Laela kwani hata ile hoteli ya Bismilah hotel ingali, sasa unashangaa nini yakhe? Wa Kuchagua wangeamua kuendelea na safari hadi njia Panda ya Kaengeza wapate mchiko wa uhakika.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  May 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Kuiga ngoma ya wanayaturu hivyo ndo kuvua gamba ati mjomba? Mwaka huu makubwa, mmmmhhhhhh.
  Halafu wahudhuriaji wengi ni toto ya shule, kwani hao ni wa kufuata maelekezo, wakishakua na bongo zao kuanza kuwa independence watakugeuka na kujutia walivyodanganywa.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  May 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Naomba sana maisha yangu yasimame katika kujitegemea kwa njia ya kawaida, lakini kujiingiza katika siasa ni jinamizi nisiloweza, maana kuna wakati inabidi nibadili kufanya mambo kinyume cha tabia na mazoea yangu.
   
Loading...