Ukondefu unaninyima amani nifanyeje ili nipate walau vinyama kidogo

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,225
3,507
HABARI WAKUU.
Wakubwa kwa Wadogo salamu kwenu
Mimi ni kijana mwenye 28 years..!

Tatzo langu ni uwembamba uliopitiliza natamani walau na mimi niwe na vinyama kidogo. Nakumbuka mwaka jana niliwahi kupima uzito wangu nikawa 48kg uzito wa Jogoo la kienyeji iliniuma sana nilikaa wiki zima nikitafakari hatma ya afya yangu hadi hapo nilipoenda kupima magonjwa yote nikakutwa nipo smart sina tatzo la kiafya!

Nikaamua kujianzishia Dozi ya kula matunda kila baada ya chakula na mara kwa mara hali ambayo ilikuwa inanigalimu kila siku kutumia galama zaidi ya elfu kumi 10,000 kwa ajili ya Kuimalisha Afya yangu pia nilipata ushauri wa kula kitimoto na Bia moja kila siku! Hali ambayo sikuona shida nilikuwa nafanya hivyo hadi kujikuta nakuwa mlevi wa bia, Maana nilikuwa nakunywa bia moja kwa ajili ya Afya ila hatmae nikajikuta nakunywa bia zaidi ya 5 kwa siku maana tabia ya Bia nilikuwa nikinywa moja natamani kuongeza nyingine na nyingine hadi nikajikuta nakuwa mlevi pasipo kukusudia hali hii ilikuwa inanipelekea kukosana na watu wanaonizunguka kila nikinywa pombe nawatambia majirani zangu kuwa hawana hela na kusababisha fujo hadi nyumbani kwangu! Ikabidi nijishauri mwenyewe nakuacha dozi hii kwa sasa situmii tena.

Ila katika kumbukumbu zangu kipindi nafanya haya walau nilianza kuona mabadiliko kidogo ya afya mwilini mwangu nikaanza kutokeza kakitambi kwa mbali na kunenepa shavu na nilipopimwa uzito nilikuwa nimefikisha 60Kg hadi watu walianza kuniambia nimenenepa pasipokujua hiyo hali inaniingiza galama kiasi gani!

Nilikuwa nimeanza kunyanyua kakibanda kangu ila nilisimamisha shughuli ya ujenzi, pesa yote niliokuwa napata katika mihangaiko yangu ikawa inatumika kwa ajili ya kufanyia kile ninachokitamani, baada ya kuacha tena dozi hii kwa sasa nimepururuka vibaya mno jana nimepima uzito nakuta 52kg tu na kila kukicha nazidi kukonda tena!

Nimeamua kuja hapa ili wataalamu mnipe namna ambayo itakuwa si ghali sana ambayo nitatumia ili ninenepe huu ukondefu unaninyima michongo mingi sana!
Atakaeweza kunisaidia nipo tayari kumlipa!
 
Nyama ni chakula chenye kuongeza uzito haraka, kila mlo wako kula nyama na ikiwezekana nunua nyama ya kidari.

Kula chakula na kilevi iwe wine au beer.

Baada ya siku 28 type mrejesho.
Asante mkuu nimedandia huu ushauri, mi mwenyewe ni mwembamba hadi naogopa kupima uzito ingawa nachukulia poa tu sijawai kujishughurisha na hilo, ila ushauri wako nitaufanyia kazi na mimi nione.
 
Nyama ni chakula chenye kuongeza uzito haraka, kila mlo wako kula nyama na ikiwezekana nunua nyama ya kidari.

Kula chakula na kilevi iwe wine au beer.

Baada ya siku 28 utupe mrejesho.

Hapo kwenye nyama haijalishi imeandaliwaje !?
Kukaangwa,michemsho,kuchoma au rost
 
Asante mkuu nimedandia huu ushauri, mi mwenyewe ni mwembamba hadi naogopa kupima uzito ingawa nachukulia poa tu sijawai kujishughurisha na hilo, ila ushauri wako nitaufanyia kazi na mimi nione.
Ukitaka kupungua uzito ukitoa pombe na nyama kwenye ratiba yako umefanikiwa
 
Kwa kuwa kazi unayofanya inakuingizia kipato,na kwa kuwa unayo nia ya dhati kuwa chibonge basi nakushauri udundulize hela na kujiepusha na matumizi yasiyo na ulazima ili kiasi unachookoe ukitumie kama nauli ya kuruka hapo China Chap kule kuna karakana za kutosha kutatua tatizo linalokukabili! Makalio na sehemu za ndoa utaonyezwa tu kama ofa ya huduma!
 
Yani unashindilia nyama na bia on a daily basis hunenepi? Kweli binadamu tunatofautiana.

Watu tuna 130kgs hapa. Hatukutumia mwezi kufika hapa. Inabidi ule heavily na ule vizuri (NYAMA) kila siku ya maisha yako. Hata kilo 200 utafika. Pia gonga sana sugary foods, soda, keki, mavitu ya supermarket yenye sukari.

Always kunenepa au kukonda hakutakiwi temporay adjustment in meal habits ila permanent one.
 
Kwa kuwa kazi unayofanya inakuingizia kipato,na kwa kuwa unayo nia ya dhati kuwa chibonge basi nakushauri udundulize hela na kujiepusha na matumizi yasiyo na ulazima ili kiasi unachookoe ukitumie kama nauli ya kuruka hapo China Chap kule kuna karakana za kutosha kutatua tatizo linalokukabili! Makalio na sehemu za ndoa utaonyezwa tu kama ofa ya huduma!
Oy mi mwanaume makalio ya nini sasa mbona unaleta mizaha katika issue seteous ndugu
 
Mkuu umeelewa post yangu "samahani"

Ninamaanisha nilikuwa nakunywa bia moja ila bia huwa ina tabia ukinywa moja ikiisha unataman kuongeza tena natena na tena.........hapo ndio inakuja addiction na ulevi
kuwa na msimamo usiwe kama v money
 
Back
Top Bottom