Ukomo wa kustaafu upunguzwe uwe miaka 50 kwa lazima

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,879
Wadau nawasalimu.

Ni wakati sahihi kwa sasa sheria ya kustaafu kwa watumishi wa umma iangaliwe.Sheria hii ni ya zamani sana na ilikuwa na sababu ya kuwepo kwani wasomi walikuwa wachache sana.

Hivi sasa nchi yetu ina wasomi wengi sana na uwingi wa wasomi kumesababisha ukosefu mkubwa wa ajira ikiwa ni pamoja na watumishi kukaa ktk utumishi mpaka afikishe miaka 60 ndio astaafu muda ambao ni mrefu sana.

Ushauri wangu ni kuwa serikali irekebisha umri wa kustaafu kutoka miaka 55 kwa hiari iwe miaka 45 na miaka 60 kwa lazima uwe miaka 50 ili kuwapisha wasomi wengine walitumikie taifa na hao wastaafu wakajipumzishe wakiwa na nguvu kuliko sana wanapumzika wakiwa wamechoka sana. Isitoshe itasaidia kupunguza ukosefu wa ajira kwa wasomi wetu.
 
Do you know how pensions work?if the answer is no ,go and look it up,you will understand why most countries are raising the age of retirees na jibu la swali lako utalipata!!!mfn. Britain waliongeza toka 62 kwenda 67 kama sikosei...look up the reasons why!
 
  • Thanks
Reactions: RMC
Kwani lazima uwe employed?Do business and create jobs. Bado kuna kazi zinahitaji hata 70yrs. Let them work
 
Nakubaliana na wewe. Mimi ingewezekana ikifika miaka 50 ning'atuke ila nawaza sheria inasemaje
 
Sijasoma ulicho andika zaidi ya title ila nakuunga mkono ukomo wa kustaafu ushushwe chini.

Wewe umependekeza miaka 50 nami napendekeza 45.

Ipatikane nafasi kwa vijana wetu nao kuajiriwa na kujipatia mitaji ya kujiajiri na kuajiri.
 
Do you know how pensions work?if the answer is no ,go and look it up,you will understand why most countries are raising the age of retirees na jibu la swali lako utalipata!!!mfn. Britain waliongeza toka 62 kwenda 67 kama sikosei...look up the reasons why!
Mkuu wengi hawaelewi how finance and money works. Wanadhani serikali na mifuko inachuma pesa kwenye miti
 
Mifuko ya penshen itakauka kwakua waty wenye uwezo wa kufanya kazi watakua wanastarehe wanakula penshen
 
Nakubaliana na wewe. Mimi ingewezekana ikifika miaka 50 ning'atuke ila nawaza sheria inasemaje
Kwa sasa KUSTAAFU kwa HIARI ni 55 ila unaweza kuomba kwa sababu za kiafya kuja Jamaa ameomba amekubaliwa na Amelipwa
 
Kwa sasa KUSTAAFU kwa HIARI ni 55 ila unaweza kuomba kwa sababu za kiafya kuja Jamaa ameomba amekubaliwa na Amelipwa
Mimi kwa kazi yangu hiari ni 60, lazima ni 65 ila naona ni utumwa tuu. Natamani niwe free lander soon maana nimeshaweka msingi wa maisha yangu nikasake financial freedom.

Nakerwa sana na kukurupushana kila wakati mara unaambiwa bosi anataka hiki mara kile, sometimes anavunja sheria na taratibu lakin kwa sababu ni boss unatakiwa kutii tuu, ukimpinga shida.

haya maisha siyawezi mimi
 
Labda kitu ambacho ulikuwa haukijui au unakijua ni kwamba!

Kustaafu mapema ni hasara kwa serikali, kwa sababu ya kuwahudumia wastaafu na kuwaajiri vijana wapya. Kwa mfano, kwa sheria ya sasa, mtumishi akistaafu atalipwa pensheni kila mwezi mpaka kufa. Sasa akistaafu na miaka 50, atakufa lini? Serikali italazimika kuwalipa wastaafu kwa muda mrefu, pamoja na vijana wapya walioajiriwa.

Ndiyo maana baadhi ya nchi waliongeza muda mpaka miaka 60, ili watumishi waendelee kuitumikia serikali na mtumishi akistaafu anakaa kidogo anakufa. Kumbuka, watumishi wengi wakistaafu kwa mkupuo ni changamoto kwa serikali pia.

Pia, usifikiri watumishi wote wanapenda kutanya kazi mpaka miaka 60. Ukiwa ushule utatamani ufanye kazi miaka mingi, lakini ukishaanza kazi na ukafika miaka 50 hivi unachoka balaaa, unatamani kustaafu lakini sheria inakubana. Hizi kazi zinachosha hasa umri ukiwa umeenda, mara kisukari, presha, mara wajukuu, nk. Labda kazi za wabunge ndiyo hazichoshi mana wao wanalainisha tu!
 
Wazo zuri kinadharia tu lakini siyo practical. Utendaji hautegemei elimu tu, bali experience zaidi. Wewe unaonekana kuthamini elimu kuliko experience.

Ninajua kuna nchi kama marekani wanaongelea kuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 64 kuwa miaka 70! Kwa maoni yako, ina maana huamini kuwa mama SSH ambaye ana miaka 60 hawezi tena kuongoza nchi, awaachie waliotoka chuo!
 
Sijasoma ulicho andika zaidi ya title ila nakuunga mkono ukomo wa kustaafu ushushwe chini.
Wewe umependekeza miaka 50 nami napendekeza 45.
Ipatikane nafasi kwa vijana wetu nao kuajiriwa na kujipatia mitaji ya kujiajiri na kuajiri.
mm napendekeza wasifanye kazi kabisa wakae nyumbani tu wale ugali
 
Wadau Nawasalimu.
Ni wakati sahihi kwa Sasa SHERIA ya KUSTAAFU kwa WATUMISHI wa UMMA iangaliwe.SHERIA hii ni ya ZAMANI sana na ilikuwa na SABABU ya kuwepo kwani WASOMI Walikuwa WACHACHE sana.
Hivi Sasa NCHI yetu ina WASOMI Wengi sana na Uwingi wa WASOMI kumesababisha UKOSEFU MKUBWA wa AJIRA ikiwa ni Pamoja na WATUMISHI kukaa ktk UTUMISHI mpaka Afikishe Miaka 60 ndio ASTAAFU Muda ambao ni MREFU sana
Ushauri wangu ni kuwa SERIKALI irekebisha UMRI wa KUSTAAFU Kutoka MIAKA 55 kwa HIARI iwe MIAKA 45 Na MIAKA 60 kwa LAZIMA uwe MIAKA 50 ili Kuwapisha WASOMI wengine Walitumikie TAIFA na hao WASTAAFU Wakajipumzishe Wakiwa na NGUVU kuliko sana Wanapumzika wakiwa WAMECHOKA SANA. Isitoshe itasaidia KUPUNGUZA Ukosefu wa AJIRA kwa WASOMI wetu.
Chukulia mfano mtu ni dereva wa manispaa unamstaafisha akiwa na miaka 45,hapo watoto wake hata chuo hawajafika,mshahara wake ulikuwa laki tatu,pensheni atakuwa anapokea elfu hamsini kila mwezi,je ataweza kusomesha watoto wake wafike chuo kama wewe!?labda ingekuwa ukistaafu unapewa Kiiunua mgongo chako chote,milioni kama 50,au ikibaki miaka 10 ustaafu unapewa mshiko wako uanze kujiandaa,
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom