Ukomo wa kufungua shauri la ardhi katika mahakama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukomo wa kufungua shauri la ardhi katika mahakama

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Dec 12, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Ukomo wa kufungua shauri la ardhi katika mahakama
  Thursday, 09 December 2010 21:59

  KATIKA kuhakikisha inatekeleza haki za walalamikaji kwa wakati na kupunguza mrundikano wa kesi, Mahakama Kuu ya Tanzania imejigawa katika divisheni mbalimbali ambazo huchukua na kuamua aina fulani za kesi tu. Divisheni hizo ni pamoja na Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, Kitengo cha Biashara na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi.


  Kimsingi kila mahakama hupokea na kuamua kesi zinazohusu aina ya mgogoro unaohusika nayo na kwa maana hiyo haitakubalika na mahakama husika kusikiliza shauri ambalo kimsingi lilipaswa kusikilizwa na divisheni nyingine ya Mahakama Kuu. Hivi karibuni kumefanyika mabadiliko kadhaa katika Sheria ya Ardhi yanayotoa fursa na uwezo kwa Mahakama Kuu kusikiliza mashauri ya ardhi bila kuathiri utaratibu wa kisheria.

  Hii imefanyika kwa kuzingatia sababu ileile ya mrundikano wa kesi, kitengo cha ardhi kimeonekana kuzidiwa na wingi wa kesi kulinganisha na idadi ya majaji waliopo katika mahakama hiyo.


  Mashauri yote yahusuyo migogoro ya ardhi hufunguliwa, kusikilizwa na kuamuliwa na Mahakama ya Ardhi ama moja kwa moja kufunguuliwa katika mahakama hiyo endapo thamani ya mgogoro (pecuniary jurisdiction) hairuhusu mabaraza ya kata kusikiliza, au wakati mwingine kupokea kama rufaa kutoka katika mabaraza ya kata na yale ya ardhi na nyumba ya wilaya ambayo pia kwa mujibu wa mabadiliko hayo, yanaweza kufunguliwa kwa Mahakama Kuu ya Tanzania.

  Katika kuwajibika juu ya utatuzi wa migogoro hiyo mbele yake, mahakama na mabaraza hayo huongozwa na sheria mbalimbali miongoni mwazo ni ile yenye dhamana ya masuala ya ardhi, Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 na Sheria ya Ukomo (The Law of Limitation Act) sura ya 89 ya mwaka 1971.
  Sheria hii ya ukomo hutumika katika kusimamia ufunguzi wa mashauri yote ya asili ya madai kama vile mikataba, ardhi, madhara na mengine yote yenye asili ya madai. Sheria hiyo ya ukomo inatoa fursa ya kuwasilisha mashauri yenye asili ya migogoro ya ardhi katika mahakama na mabaraza yenye uwezo katika kipindi cha 12 tangu kutokea kwa mgogoro. Maana ya msimamo huu wa kisheria ni kwamba malalamiko yoyote yahusuyo ardhi yaliyoibuka ndani ya kipindi cha miaka hiyo hayatakuwa na haki ya kusikilizwa na kuamuliwa kama ilivyo kwa mashauri mengine.

  Labda inaweza kuzua swali la msingi kwamba ni wakati gani muda huu wa kisheria huanza kuhesabiwa rasmi. Tarehe na siku ambayo mgogoro husika uliibuka kwa mara ya kwanza ndiyo huchukuliwa kama ni chanzo cha mgogoro, hivyo kutokea hapo hesabu zake zitaishia tarehe ya mbele inayotimiza miaka 12.
  Ifahamike tu kwamba si kazi ya mahakama kuibua hoja kwamba shauri husika limepitwa na wakati, hii ni kazi ya kimsingi kwa upande wa mlalamikiwa au walalamikiwa, ama kwa mlalamikaji binafsi au wakili wake kuwasilisha kwa njia ya pingamizi na kuithibitisha hoja hiyo mbele ya mahakama sambamba na kuiomba kulifutilia mbali shauri husika. Uthibitisho huo ambao huwasilishwa kisheria na kihistoria ndiyo unaotumika kuiomba mahakama kukubali au kukataa maombi husika kutegemea na uzito wa hoja zilizowasilishwa na pande zote katika kesi.

  Kushindwa kuwasilisha malalamiko au kuripoti mgogoro katika mamlaka yenye uwezo wa kusikiliza shauri, humaanisha kupoteza haki ya msingi na kikatiba huku ukiona kwa macho yako. Kwa upande wa waweka pingamizi ambao walalamikiwa au wadaiwa katika kesi ya msingi hujipatia umiliki halali wa ardhi bila ya kujali kama ni kweli ardhi hiyo si yao na malalamiko ya mdai yalikuwa na msingi ndani yake na bila ya shaka kama yangesikilizwa ni wazi mahakama husika ingeamuru mdai kurejeshewa ardhi yake.

  Lakini kutokana na kutokidhi haja ya sheria ya ukomo pekee, inatoisha kwa mahakama kukubali kutosikiliza malalamiko ya mdai. Kipindi cha miaka 12 ni kirefu kutosha kukidhi haja ya kufungua na kufuatilia kesi husika mahakamani, ni kipindi kinachoshuhudia mabadiliko mengi katika ardhi husika na ni kwa ajili hiyo ili kuondoa usumbufu na kuhamasisha wamiliki wa ardhi kuwajibika na ardhi zao ndipo iliwekwa sheria hii kwa makusudi kusaidia na kuchochea kutilia maanani na kujali miongoni mwa raia.

  Hivyo ni vyema kufuatilia mara kwa mara vipande vya ardhi tulivyomilikishwa kihalali ili kuepuka adha ya kuvamiwa na kukaliwa na watu wengine kwa muda mrefu kiasi cha kusababisha mgogoro ambao hatimaye huishia kupoteza umiliki wa ardhi ambayo ndiyo chanzo kikuu cha uchumi miongoni mwa Watanzania wengi.
   
 2. mzee74

  mzee74 JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2016
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 5,440
  Likes Received: 3,806
  Trophy Points: 280
  Asante kwa makala nzuri.
  Naomba kuuliza kuhusu uuzwaji wa ardhi mara mbili.
  Nilinunua ardhi mwaka 2005 na kupata hati ya serikali ya mtaa.Baadae alieniuzia akauza tena kwa mtu mwingine mwaka 2006.
  Baraza la ardhi baada ya kusikiliza shauri likampa umiliki yule mnunuzi wa pili kwa vile yule muuzaji alisema yeye ndio mnunuaji halali.
   
 3. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2016
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  Rutashubanyuma nisaidie. Hopefully wewe ni mwanasheria. Nimestaafu kwa mujibu wa sheria. Nilikuwa na madai yangu ambayo wakati nastaafu nilikuwa sijalipwa. Sasa muda wa ukomo wa kudai haki hiyo ni upi. Nasema hivyo kwa kuwa nimstaafu, hapakuwa na labour dispute. Sasa time limitation katika hali kama hii ni ipi?
   
 4. sajo

  sajo JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2016
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 365
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Ulistaafu mwaka gani na nini majibu kuhusiana na malipo yako hayo pindi ulipoyafuatilia?
   
 5. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2016
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  Nimestaafu July 2015. Sijapata vitu kama acting allowances nilizokuwa nadai kabla ya kustaafu, awards mbali mbali ambazo shirika linazitoaga kwa utumishi wa muda mrefu. Zito kwenye standing orders za shirika .
  Walinipa barua kuwa wakipata fedha watanilipa.-commitment letter
   
 6. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2016
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  Rutashubanyuma, nikikaa kwenye ardhi yenye granted right of occupancy kwa miaka 12 na zaidi bila kubugudhiwa na mwenye, Je sheria ya ukomo wa miaka 12 inahusika hata kwenye ardhi yenye granted right of occupancy?
   
 7. joshydama

  joshydama JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2016
  Joined: May 10, 2016
  Messages: 2,612
  Likes Received: 1,933
  Trophy Points: 280
  Sheria inasema ukitumia ardhi ndani ya miaka 12 na zaidi bila ya kubugudhiwa hiyo ardhi inakuwa yako na unaweza kwenda kuomba hati miliki (title deeds).

  Pia una haki sawa kabisa na yule ambaye alipewa right of occupancy.

  Hivyo basi yule ambae alikuwa mmiliki wa Mara ya kwanza atapoteza hiyo haki ya umiliki kwa kushindwa kuindeleza ardhi Kwa muda unaofaa kulingana na maelezo anayopewa.
   
 8. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2016
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  sante sana rafiki. Nina issue kama hiyo inanihusu. Nice for your confirmation.
   
 9. joshydama

  joshydama JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2016
  Joined: May 10, 2016
  Messages: 2,612
  Likes Received: 1,933
  Trophy Points: 280
  Wahi sasa ukaombe hati miliki Mkuu.

  Ili upate kunufaika vizuri na hiyo ardhi.
   
Loading...