Ukomo wa kufikiri wa viongozi wetu

julius mahinya

JF-Expert Member
May 11, 2013
1,152
1,500
Hapa tulipofika viongozi wetu wa serikali za kiafrika wamefikia ukomo wa kufikri. Nikianza na nchi yangu katika mchakato wa kutengeneza katiba mpya watu wanabishana juu ya aina ya kura kati ya siri na wazi mwisho wasiku wanakosa maamzi kamati ya uongozi inakuja na jibu la wazi na siri zitumike huu ni ukomo wa kufikiri kuona kura zote zina manufaa sawa kwamba wazi na siri hazina tofauti!
Tukibakia hapo hapo kwenye bunge la katiba wanang'ang'ania tatu kwa mbili namaanisha serikali kama ilivyokuwa kwa siri na wazi. Mimi nadhani huu ni ukomo wa kufikiri hivi wanaotaka mbili ni kwa manufaa ya nani? na wanaotaka tatu ni kwa manufaa ya nani?
Kama waryoba anasema tatu ni mawazo ya wananchi na wanaotaka mbili hawaamini kama wananchi wanataka tatu si wapige kura ili tuwe na political will juu ya muundo wa serikali?
wananchi munaowasingizia wapo sasa mnarumbana na kuteketeza fedha nyingi wengine wawahonge wajumbe wengine wazunguke nchi nzima si tupige kura ya tatu' mbili na sie wa moja ambao tulikosa support katika bunge la katiba tupate chance ya kutetea hoja zetu kupitia kura ya serikali moja!

Nikirudi Malawi hivi huyu mama J. B mnaomfahamu akili zake ziko sawa au ndio mwisho wa fikira zake umefikia pale? Yaani watu wamemkataa kupitia sanduku la kura lakini analazimisha wamkatae kwa kumpiga mawe ndio afurahie au ndio fikira zetu finyu. Analazimisha kuongoza watu hawakutaki kwa faida ya nani sasa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom