Ukombozi wetu utakuja pale tu tutakapoanza kuheshimu mawazo ya kila mtu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukombozi wetu utakuja pale tu tutakapoanza kuheshimu mawazo ya kila mtu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dijovisonjn, Mar 15, 2012.

 1. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ukombozi wa mtanzania utakuja pale kila mtu atakapoheshimu mawazo ya mwenzake na kuyakubali au kuyapinga kwa hoja na si kwa matusi.

  Ni vigumu sana kwa mwanachama na shabiki wa CHADEMA kukubaliana na mawazo ya shabiki au mwanachama wa CCM vivyo hivyo pia ni vigumu kwa shabiki na mwanachama wa CCM kukubaliana na mawazo ya shabiki au mwanachama wa CHADEMA au chama chochote kile cha upinzani, hii hali inakubalika na wala sio mbaya lakini tatizo, badala ya HOJA KUPINGWA KWA HOJA, hapa kwetu hoja inapingwa kwa MATUSI NA KASHFA zisizo za uhakika.
  Ndugu zangu matusi hayatujengi wala kutupa faida yeyote zaidi ya kushusha hadhi ya utu wetu.
  Hebu kwa pamoja kwa wale wote wenye nia njema na Tanzania tujifunze kuheshimu mawazo ya wale wenye imani au itikadi tofauti na sisi na kama ni kupinga hoja zao basi tuzipinge kwa hoja na sio kwa matusi.
   
Loading...