Ukombozi wa tanzania 2015; chadema nataka kusikia hili.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukombozi wa tanzania 2015; chadema nataka kusikia hili....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mharakati, Jul 13, 2012.

 1. m

  mharakati JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  M4C, MAGWANDA, na pilika pilika zote hizi zinaonyesha kitu kimoja kua CDM imedhamiria kuleta mabadiliko ya kweli ya jinsi taifa hili limekua likiendeshwa hii ikiwemo na kufukia kabisa wale watawala wabaya waliopita. Wale waliotuweka gizani bila sababu, wale waliokwapua mabilioni ya wananchi bila aibu, wale waliotorosha wanyama wetu nje, wale waliotuingiza kwenye madeni hewa ya kitaifa n.k

  Sasa tatizo CDM na sekretariet yake sijasikia wakisema wakichukua nchi kama mwizi a, mwizi b, mwizi c wataenda mahakamani (zaidi ya Mkapa ambaye kwa kauli binafsi za muasisi wa CDM mzee mtei ataondolewa kinga ya mashitaka na kupandishwa mahakani kwa matumizi mabaya ya mamlaka ya Urais)

  Sijakisia CDM wakisema mabillioni yetu yaliyokwapuliwa kua yatarudishwa serikalini (nakumbuka kuna wakati aliyekua gavana wa benki kuu Dr Idris Rashid alipata kusema Tz ina zaidi ya $8bil nje katika akaunti binafsi za watu na hii ni miaka zaidi ya 15 imepita wakati deni letu la taifa likiwa haliko mbali sana na kiasi hicho cha fedha..unaweza kujiuliza sasa hivi zimefika ngapi huko nje zilizokwapuliwa kwa njia isiyo halali)

  Vile vile kuhusu mali zilizopo hapa ndani ya nchi ambazo zimepatikana kwa njia za kuhujumu uchumi sijasikia CDM wakisema watazitaifisha kwa manufaa ya umma..sijasikia zile nyumba zilizouzwa kiholela kule maeneo ya zamani ya kiserikali kama Ada estate, oysterbay, masaki n.k kama zitarudishwa wizara ya miundombinu kupunguza matumizi ya serikali kukodi makazi kwa watumishi wake.

  Hili linaweza kua ni jambo moja muhimu katika mengi muhimu, lakini kumbuka wananchi wana kiu ya mabadiliko kutokana na uongozi mbovu wa CCM na wala siyo sera murua za CDM. Watu wanataka huu udhaifu wa kuchekeana na wezi ukiwa haupo tena na hii ni sababu kuu ya madai na shauku kubwa ya mabadiliko nchini na ndiyo imekua theme na political capital kubwa ya CDM na wapinzani kwa ujumla.

  Kufanyika kwa haya yote ndiyo ishara na dhihiriko kuonyesha dhamira ya mabadiliko ya kweli na kamili katika uongozi wa taifa hili. Bila ya kufukia kwa haki na kurekebisha uozo wote uliopita CDM itapata shida kutengeneza tamaduni yake mpya ya uongozi kukiwa uzozo uliofanyika nyuma bado unatoa harufu kwa jamii huku athari zake zikiwa bado zinaisakama jamii na kufanya kazi yeyote ya watawala wapya ngumu zaidi ya inayotakiwa iwe.

  Mageuzi ya kweli ya kimfumo na kiuongozi yataletwa na hatua na maamuzi thabiti ya kuwachukulia hatua za kinidhamu wale viongozi wahalifu wote na uhalifu wao ili serikali ya kimageuzi iweze kufanya kazi yake vizuri na kwa ufanisi na kusimika yale mageuzi kwa vizazi vingi vijavyo.


  (CDM kumbukeni hata mr dhaifu alipoingia aliingia na kesi zake kwa akina mramba, yona, mgonja n.k ikiwa ni maamuzi ya kuondokana na uchafu wa Mkapa katika ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya..japokua haikufanya kazi kwa sababu ya wezi wengi waliombeba kuupata Urais, lakini ilikua ni dhamira nzuri)

  wananchi tunataka kusikia hili  Mharakati,
   
Loading...