Ukombozi wa taifa la tanzania

ramadhani mwendwa

New Member
Nov 23, 2012
1
0
Nimepata kumsikia Rais Thabo Mbeki akilaumu tataizo la wazee kuendelea kutawala kwamba ndicho chanzo cha kukwamisha maendeleo kwa nchi za Afrika.Siko katika lengo la kupinga mawazo yake bali kuyatolea ufanunuzi zaidi kwa lengo la kuboresha.
Napenda kuwakumbusha watanzania wenzangu kwamba siyo kila aliye na umri mkubwa anafaa au hafai kuongoza na pia siyo kila kijana anafaa au hafai kuongoza. Kinachotakiwa leo katika kuongoza Taifa kama Tanzania ni Mtu mwenye dhamira ya kweli ya kuendeleza taifa hili na watu wake bila kutafuta maslahi yake kwanza. Nimeshuhudia Vijana wenye elimu nzuri waliowengi na baadhi yao wakitokea kwenye familia za watu waliowahi kuliongoza Taifa hili na wengine bado wako madarakani wakishindwa kulisaidia Taifa hili kwa kuanza kujinufaisha wao. Ninawaomba watanzania wenzangu kutambua kwamba wakati wa kuchagua viongozi kwa sifa ya chama umepitwa na wakati na hivyo tuhoji sifa za huyo mgombea kwa kile alichofanya kwa nafasi aliyonayo kabla ya kuteuliwa na chama chake. Kitendo cha kutokuwa na sifa ya kusimamia vizuri majukumu yake ndani ya famili na jamii iliyokaribu nae kinaonyesha jinsi mtu wa namna hiyo asivyofaa kuwa kiongozi na hivyo tunapoteza muda pale tunapochagua watu wa namna hiyo kutuongoza. Natoa wito kwa watanzania tuamue sasa na tutambue kuwa viongozi wenye huruma kwa watu waliokwenda kichume na makubaliano na watu wake (SHERIA NA KATIBA) ni mbaya na hatatufikisha popote. Watu wanahitaji kiongozi aliyetayari kwa lolote kwa manufaa ya walio wengi.

Asante na huo ndio mtazamo wangu.


Ramadhani Mwendwa
 
Alikuwa anamaanisha watu wanao kuwa madarakani kwa muda mrefu au uongozi wa chama kwa muda mrefu bila ya kuachia wengine hasa vijana, kwa mfano halisi ni chama cha magamba. Watoto wanazaliwa, wanaoa na kupata watoto bado wanasikia majina yaleyale katika uongozi wa serikali au chama.
 
Mwogope mtu anayeng'ang'ania madaraka kama walivyo viongozi wa ccm kwa Taifa letu leo,ni janga kwa kwetu wanainchi!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom