Ukombozi wa kifikra kwanza na mtazamamo wa kizalendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukombozi wa kifikra kwanza na mtazamamo wa kizalendo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Oct 22, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Wimbi kubwa la kutojikomboa kifikra limeigubika Tanzania na watu wake hususani wanao ishi maeneo ya vijijini.Zinahitajika juhudi binafsi miongoni mwetu za kuweza kutumia vyema katiba yetu mbovu katika kujikomboa kifikra ikiwa ni pamoja na kutupasa kuongeza ari na uzalendo katika kulinda rasilimali za taifa.

  Uzalendo ninao uzungumzia hapa ni ile hali ya kuthubutu kutumia haki yetu ya kikatiba ya kuwatoa madarakani watawala ambao tumewapa nchi kwa takribani miongo mitano bila kutoa mwanga kwa wananchi wake kujitambua na kujiwezesha kupambana na hali tete ya maisha yao ya kila siku.

  Ukombozi wa kifikra ni ule tu utakaondoa fikra hasi na uoga ndani ya vichwa vya Watanzania na kufanya maamuzi magumu katika kuondoa mfumo mbovu wa kiutawala na kuusimika utawala mwingine ambao utajali zaidi maslahi ya nchi na watu wake kupitia sanduku la kura.

  Tukijitambua na kujikomboa katu hatutokubali kupangiwa bei zetu na kudhalilishwa utu wetu kwa kuuza kipalata cha kupigia kura kwa shilingi elfu tano.Unapouza haki yako kama mzaliwa ni sawa na umeuza utu na heshima yako.Hali hii ya kuuza utu wako hatofautiani sana na utumwa.

  Shime sasa Watanzania tuamke na kuwa walinzi wa haki za kila mmoja kulinda na kuizuia dhuluma ambayo inatumika kuwanyang'anya wananchi ardhi yao na kuwa milikisha wageni.Tukiweza kulitambua hilo hata mawakala(mabalozi) wa ufisadi huo na utumwa mamboleo tukawathibiti tutakuwa tumelikomboa taifa letu dhidi ya utawala wa kimangimeza.


  Viva Tanzania viva,viva haki viva
   
 2. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ninavyo zungumza hivi tayari vitambulisho vya mpiga kura vimeanza kununuliwa kwenye chaguzi za madiwani,uchaguzi unatazamiwa kufanyika jumapili ya 28/10/2012 unao husisha kata 29 nchini kote.Matukio haya yamefanyika na taarifa ziko Polisi lakini hakuna hatua madhubuti zilizoonyeshwa kuchukuliwa.

  Haiwezekani Mtanzania huyu wa daraja la chini(third class) akahujumiwa haki yake ya kuchagua viongozi awatakao kwa udhaifu alionao wa njaa ambayo imesababishwa na sera mbovu za CCM za kushindwa kumpigania mkulima kupata bei nzuri ya mazao.Wanao fanya mchezo huu ni wajumbe wapya wa CCM kutekeleza mpango wao kabambe wa kuhakikisha kamati ya saidia CCM ishinde mwaka 2015.

  Si vibaya kujipanga kimkakati ila tatizo ni mbinu chafu ya makusudi kughilibu wanyonge kutokana na njaa yao na kuamua kupoteza haki zao za kikatiba.Watanzania tukiweza kujitambua na kulikemea hili kwa kauli kali hakika tutaipata Tanzania tuitakayo
   
Loading...