Elections 2010 Ukombozi unakaribia,unacheleweshwa tu.

Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
2,008
1,766
Ukifuatilia kwa makini siasa nchini tangu uchaguzi wa 2005 hadi 2010 utagundua kuwa idadi ya wananchi wengi walioipigia CCM kura mwaka 2005 wameipigia kura CHADEMA mwaka huu.Hii imechangiwa sana na wananchi wengi kufumbuliwa macho na kushuhudia jinsi nchi inavyotafunwa na wachache huku wenyewe wakiendelea kuwa maskini wa kutupwa.Watu wengi walikuwa na imani kubwa na Kikwete kabla hajaingia madarakani mwaka 2005 na kupelekea kumpa ushindi wa kishindo wa 82% ya kura zote halali,huku mpiganaji Freeman Mbowe akipata 5% na wabunge watano tu.Kwa mara ya kwanza wananchi wakashuhudia serikali mbaya zaidi katika historia nchini.Serikali dhaifu,dhalimu,ya kirafiki na ya kifisadi ya raisi Kikwete,huku idadi ya maskini ikiongezeka kwa zaidi ya mil1.5,huku wananchi wakisomewa mafanikio ya kuongeza idadi ya vitu!Ndipo kashfa nyingi zikaibuliwa na hata jina la Dr.Slaa kuzidi kupata mashiko nchini.Tumeshuhudia mwaka huu CHADEMA ikimsimamisha Dr.Slaa kupambana na Kikwete na CCM kupigwa mweleka mkubwa.CHADEMA imeongeza kura za uraisi kutoka 5%mwaka2005 hadi 26%mwaka huu huku CCM ikiporomoka kutoka 82%hadi 61%mwaka huu pamoja na kuchakachua kura nyingi!Hata viti vingi vya ubunge vya CCM vimebebwa na CHADEMA na kufanya idadi ya wabunge wa CHADEMA kufikia 24!Tukirudi kwenye kura za uraisi CCM imeshuka na CHADEMA imepanda kwa kiwango kinachofanana cha 21%!Kama CHADEMA itaendelea kupafom hivihivi na CCM ikaendelea kuboronga hivihivi(kitu ambacho kinategemewa), na tume ya uchaguzi ikaendelea kubaki hiihii isiyokuwa huru na haki,na kuchakachua kukaendelea kwa kiwango hikihiki kikubwa,chadema itaongoza nchi mwaka 2010 kwa kupata kura za uraisi 47%na kufuatiwa na CCM 40%!Kwa hiyo ukombozi unakuja mwananchi,wanauchelewesha tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom