Ukombozi umewadia:Awamu ya 5, Rais Dr Slaa, WM Sitta, Awamu ya 6 Rais Mwakyembe, WM Mbowe

jaman tusichanganye mambo raisi dk slaa waziri mkuu mbowe mambo yanakwenda atuhitaji watu kutoka ccm wa nn sasa?
 
Ngoja nikasari tu, maana uzi huu unaweza ukasababisha nikala ban na pia kuihalifu sabato ya Bwana.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Nawatamani sana S. Sitta na Dr. Mwakyembe, karibuni CHADEMA.

Kuna makubaliano maalum kati ya Chadema na kundi la Sitta. Ilikuwa Sitta agombee urais ila kukatokea matatizo na ndio maana walimwomba Dr Slaa agombee hakuwa ameandaliwa. Mkakati mkubwa ni kuwa kundi la Sitta karibia na uchaguzi 2015 litajiunga na chadema na Dr Slaa atakuwa rais Sitta waziri mkuu. Watatawala kwa kipindi kimoja kipindi kingine anagombea mwakyembe na wm Mbowe. Kwanini inawezekana?
(i) Kundi la Sitta ni wazalendo sawa na ilivyo chadema hivyo wanaweza kufanya kazi pamoja "like-minded"
(ii) CCM hawawezi kukubali kundi la Sitta lichukue power kwani halitakuwa tofauti na chadema- watakamata sana mafisadi na kuibomoa ccm na kuiunda upya tofauti na maslahi ya mafisadi

Ninukuu, nchi itapata ukombozi 2015 na itakuwa salama ndani ya hao niliowataja
 
Sitta kwa hasira na chuki ya kutopata Urais CCM anaweza kwenda CDM kichini chini yaani kuisaidia CDM ichukue nchi huku yeye akibaki mwanachama tu wa CCM. Sitta ni mzalendo, smart na ana uzoefu mkubwa sana ambao wengi hawana na hatoweza vumilia kufanya kazi chini ya Mbowe na Slaa.

Akiisaidia CDM kumshinda pandikiza la kina JK/EL atakua amepress reset button au refresh icon kusaidia kukijenga chama upya..kama CCM ikishindwa 2015 na bado ikaendelea na migogoro yake ya sasa basi CCM B ya Sitta, Mwaky, Mwandosya, etc inazaliwa huku CCM orijino ikifa taratibu.
 
Back
Top Bottom