Ukombozi kwenye media zetu ni MUHIMU kwa TAIFA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukombozi kwenye media zetu ni MUHIMU kwa TAIFA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, May 3, 2012.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nimeipenda hii nimeikuta Facebook, kwa kweli tunahitaji ukombozi kwenye media zetu, ili zitusaidie kukomboa nchi yetu inayokabiliwa na matatizo makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

  "Natumia siku hii ya Mei 3, kuomboleza: Media ni kama kikosi cha uokoaji. Inapotokea gari la zimamoto likawaka moto, inapotokea buldoza linalopaswa kuopoa magari yaliyozama linazama, ujue hali ni MBAYA na ya HATARI zaidi. Nakumbuka siku ya mafuriko Dar es Salaam, kulikua na picha mbili zinazonipa tafakuri nzito! Moja ni ile ya gari la zimamoto na uokoaji kutumbukia katika maji na ile ya katapila lililofika Mbezi Beach kuopoa magari lilipozama. Nikatafakari na sasa naona kama sisi waandishi wa habari wa Tanzania tumezama katika Taifa la watu waliokata tamaa wanaohitaji kuokolewa, nani atawaokoa? Naomboleza nikitoa wito kwa waandishi wa habari kuanzisha mapambano ya kujikomboa kwanza wenyewe ili tuweze kuikomboa nchi".

  Source:

  http://m.facebook.com/story.php?story_fbid=405093316179310&id=100000359340894&ref=pb&_rdr#405099729512002
   
Loading...