Ukoloni wa Tanganyika kwa Zanzibar kupitia kwa vibaraka wao CCM

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
792
1,144
Mh Spika sasa naomba nizungumzie masuala ya kikatiba yanayohusu Muungano wetu. Kwa wasiofahamu katiba yetu na wanaoweza kuhoji kwa nini tunazungumzia masuala ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar Katika hoja iliyopo mezani. Sura ya nne yote ya katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano inahusu serekali ya mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar, baraza la mapinduzi la Zanzibar na baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Aidha ibara ya 104 ya katiba yetu imewekwa maghsusi kwaajili ya uchaguzi wa kiongozi wa serekali ya mapinduzi Zanzibar. Kwa sababu hizi ni halali kabisa kuzungumzia yaliyotokea Zanzibar katika hoja iliyopo mezani. Mh Spika katika maoni yake juu ya mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya ofisi ya makamo wa rais kwa mwaka wa fedha 2014/15 kambi rasmi ya upinzani ya Bunge lako tukufu baada ya uchambuzi wa kina wa masuala ya fedha za muungano ilisema yafuatayo kuhusu mahusiano kati Tanganyika na Zanzibar tangu Muungano wetu uzaliwe tarehe 26 Aprili 1964.

Kwa vyovyote vile takwimu hizi zinaonesha kwamba kwa sababu ya Muungano huu uhusiano Kati ya Tanganyika na Zanzibar, ni uhusiano wa kinyonyaji kwa sababu hiyo huu ni uhusiano wa kikoloni. Ni uhusiano kati ya himaya ya Tanganyika na koloni lake la Zanzibar. Himaya za kikoloni huwa zinadhibiti masuala yote ya ulinzi na usalama, mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, uraia, kodi, fedha, sarafu na benki kuu ya makoloni yao. Na himaya za kikoloni huwa zinatumia nguvu na udhibiti wao wa masuala haya kuyanyonya makoloni yao kiuchumi, kuyadidimiza kijamii na kuyatawala kisiasa.

Hivi ndivyo ambavyo imekuwa katika mahusiano kati ya Tanganyika na Zanzibar tangu kuzaliwa kwa muungano huu tarehe 26 Aprili 1964. Mh Spika tangu mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 12 Januari 1964 hadi leo hii Tanganyika imeidhibiti Zanzibar kijeshi na kisiasa. Ukweli ni kwamba kama ambavyo Dr Harith Ghassany ameonesha katika kitabu chake "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru" Zanzibar na mapinduzi ya afrabia. Serekali ya Tanganyika ilishiriki kwa kiasi kikubwa katika maandalizi ya mapinduzi, ikiwemo kutoa silaha na mafunzo ya kijeshi katika mashamba ya mkonge ya sakura estates pangani tanga.

Kwa walio pindua serekali ya Waziri Mkuu Mohammed Shamte na Sultan Jemshid bin Abdullah. Aidha siku tatu tu baada ya Mapinduzi hayo serekali ya Tanganyika kupitia waziri wake wa mambo ya nje na ulinzi Oscar Kambona ilipelekea vikosi vya Tanganyika righ force (jeshi la Tanganyika) ili kuidhibiti Zanzibar kijeshi.

Mambo yote haya yamejulikana kwa miaka mingi na wasomi na wanazuoni wa Muungano huu na yamechapishwa katika vitabu na machapisho mengine rasmi ya kitaaluma ndani na nje ya Tanzania. Kwa kutumia udhibiti wake wa kijeshi Tanganyika pia imedhibiti siasa za Zanzibar. Watawala wa Tanganyika ndio wanaoamua nani awe mtawala wa Zanzibar. na wamefanya hivyo tangu mwaka 1964. Alhajj Aboud Jumbe Mwinyi asingekuwa Rais wa Zanzibar baada ya kuuwawa kwa Sheikh Abeid Amani Karume 1972 bila ya ushawishi wa mwalim Nyerere na serekali ya Tanganyika.

Na kama ambavyo wanazuoni wa Muungano huu kama vile Prof. Issa Shivji wameonesha Jumbe asingeng'olewa madarakani mwaka 1984 bila shindikizo la mwalimu Nyerere na watu wake hapa Dodoma. Aidha Rais Mwinyi na marais wengine wote wa Zanzibar waliomfuatia wametengenezewa Dodoma sio Zanzibar. Mh Spika tarehe 20 April 1968 mwalim Nyerere alisema yafuatayo wakati alipokuwa akihojiwa na gazeti la the observer la London Uingereza

"endapo umma wa wananchi wa Zanzibar wataamua bila kurubuniwa kutoka nje na kwa sababu zao wenyewe kwamba Muungano unaathiri kuendelea kuwepo kwao sitaweza kuwalazimisha kwa kuwapiga mabomu, Muungano hautaendelea kuwepo pale ridhaa ya washirika wake itakapo ondolewa"

Alichokisema baba wa taifa kwamba hatakifanya. serekali ya Tanganyika imekifanya kwa zaidi ya miaka ishirini sasa. Kabla ya mfumo wa vyama vingi kuruhusiwa mwaka 1992 udhibiti wa Tanganyika kwa siasa za Zanzibar ulifanyika kwa kutumia dhana ya chama kushika hatamu. Katika zama za vyama vingi wananchi wa Zanzibar wamekuwa wapinzani wakubwa wa ukoloni wa Tanganyika kwa nchi yao Kwa sababu hiyo tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 serekali ya Tanganyika imekuwa ikitumia mabavu ya kijeshi ya waziwazi ili kuwaweka madarakani vibaraka wake na kuendelea kiutawala Zanzibar.

Kilele cha matumizi haya ya mabavu ya kijeshi ni uchaguzi mkuu wa mwaka jana (2015). Ambopo vibaraka wa Tanganyika katika Zanzibar walikataliwa kabisa na wananchi wa Zanzibar katika uchaguzi wa urais, wawakilishi na madiwani. Ni jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania tu ndilo ambalo limehakikisha kwamba vibaraka hawa waliokataliwa na wananchi wao wanaendelea kubaki madarakani.

Kwa maoni yetu Mh Spika katika mazingira haya tatizo la msingi la Zanzibar sio Jecha Salim Jecha wala ZEC wala Ali Mohamed Shein. Hawa ni vibaraka tu wasiokuwa na nguvu wala uhalali wowote. Bila ya nguvu ya Tanganyika vibaraka hawa hawawezi kudumu madarakani kwa muda mrefu. Tatizo la msingi ni ukoloni wa Tanganyika kwa Zanzibar ambao umevikwa Joho la Muungano. Bila kulivua Joho hili na kushona jengine badala yake Zanzibar haitakuwa huru na itaendelea kutawaliwa na Tanganyika kisiasa, kiuchumi na kijeshi.

Tundu Lissu.
 
Mlipata nafasi ya kujitawala kwa njia ya kura lakini shein na jecha hawataki muwe huru, kwa hiyo tutaendelea kuwatawala mpaka mjitambue
 
Mh SZpika sasa naomba nizungumzie masuala ya kikatiba yanayohusu Muungano wetu. Kwa wasiofahamu katiba yetu na wanaoweza kuhoji kwa nini tunlazungumzia masuala ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar Katika hoja iliyopo mezani. Sura ya nne yote ya katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano inahusu serekali ya mapinduzZzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar, baraza la mapinduzi la Zanzibar na baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Aidha ibara ya 104 ya katiba yetu imewekwa maghsusi kwaajili ya uchaguzi wa kiongozi wa serekali ya mapinduzi Zanzibar. Kwa sababu hizi ni halali kabisa kuzungumzia yaliyotokea Zanzibar katika hoja iliyopo mezani. Mh Spika katika maoni yake juu ya mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya ofisi ya makamo wa rais kwa mwaka wa fedha 2014/15 kambi rasmi ya upinzani ya Bunge lako tukufu baada ya uchambuzi wa kina wa masuala ya fedha za muungano ilisema yafuatayo kuhusu mahusiano kati Tanganyika na Zanzibar tangu Muungano wetu uzaliwe tarehe 26 Aprili 1964.

Kwa vyovyote vile takwimu hizi zinaonesha kwamba kwa sababu ya Muungano huu uhusiano Kati ya Tanganyika na Zanzibar, ni uhusiano wa kinyonyaji kwa sababu hiyo huu ni uhusiano wa kikoloni. Ni uhusiano kati ya himaya ya Tanganyika na koloni lake la Zanzibar. Himaya za kikoloni huwa zinadhibiti masuala yote ya ulinzi na usalama, mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, uraia, kodi, fedha, sarafu na benki kuu ya makoloni yao. Na himaya za kikoloni huwa zinatumia nguvu na udhibiti wao wa masuala haya kuyanyonya makoloni yao kiuchumi, kuyadidimiza kijamii na kuyatawala kisiasa.

Hivi ndivyo ambavyo imekuwa katika mahusiano kati ya Tanganyika na Zanzibar tangu kuzaliwa kwa muungano huu tarehe 26 Aprili 1964. Mh Spika tangu mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 12 Januari 1964 hadi leo hii Tanganyika imeidhibiti Zanzibar kijeshi na kisiasa. Ukweli ni kwamba kama ambavyo Dr Harith Ghassany ameonesha katika kitabu chake "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru" Zanzibar na mapinduzi ya afrabia. Serekali ya Tanganyika ilishiriki kwa kiasi kikubwa katika maandalizi ya mapinduzi, ikiwemo kutoa silaha na mafunzo ya kijeshi katika mashamba ya mkonge ya sakura estates pangani tanga.

Kwa walio pindua serekali ya Waziri Mkuu Mohammed Shamte na Sultan Jemshid bin Abdullah. Aidha siku tatu tu baada ya Mapinduzi hayo serekali ya Tanganyika kupitia waziri wake wa mambo ya nje na ulinzi Oscar Kambona ilipelekea vikosi vya Tanganyika righ force (jeshi la Tanganyika) ili kuidhibiti Zanzibar kijeshi.

Mambo yote haya yamejulikana kwa miaka mingi na wasomi na wanazuoni wa Muungano huu na yamechapishwa katika vitabu na machapisho mengine rasmi ya kitaaluma ndani na nje ya Tanzania. Kwa kutumia udhibiti wake wa kijeshi Tanganyika pia imedhibiti siasa za Zanzibar. Watawala wa Tanganyika ndio wanaoamua nani awe mtawala wa Zanzibar. na wamefanya hivyo tangu mwaka 1964. Alhajj Aboud Jumbe Mwinyi asingekuwa Rais wa Zanzibar baada ya kuuwawa kwa Sheikh Abeid Amani Karume 1972 bila ya ushawishi wa mwalim Nyerere na serekali ya Tanganyika.

Na kama ambavyo wanazuoni wa Muungano huu kama vile Prof. Issa Shivji wameonesha Jumbe asingeng'olewa madarakani mwaka 1984 bila shindikizo la mwalimu Nyerere na watu wake hapa Dodoma. Aidha Rais Mwinyi na marais wengine wote wa Zanzibar waliomfuatia wametengenezewa Dodoma sio Zanzibar. Mh Spika tarehe 20 April 1968 mwalim Nyerere alisema yafuatayo wakati alipokuwa akihojiwa na gazeti la the observer la London Uingereza

"endapo umma wa wananchi wa Zanzibar wataamua bila kurubuniwa kutoka nje na kwa sababu zao wenyewe kwamba Muungano unaathiri kuendelea kuwepo kwao sitaweza kuwalazimisha kwa kuwapiga mabomu, Muungano hautaendelea kuwepo pale ridhaa ya washirika wake itakapo ondolewa"

Alichokisema baba wa taifa kwamba hatakifanya. serekali ya Tanganyika imekifanya kwa zaidi ya miaka ishirini sasa. Kabla ya mfumo wa vyama vingi kuruhusiwa mwaka 1992 udhibiti wa Tanganyika kwa siasa za Zanzibar ulifanyika kwa kutumia dhana ya chama kushika hatamu. Katika zama za vyama vingi wananchi wa Zanzibar wamekuwa wapinzani wakubwa wa ukoloni wa Tanganyika kwa nchi yao Kwa sababu hiyo tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 serekali ya Tanganyika imekuwa ikitumia mabavu ya kijeshi ya waziwazi ili kuwaweka madarakani vibaraka wake na kuendelea kiutawala Zanzibar.

Kilele cha matumizi haya ya mabavu ya kijeshi ni uchaguzi mkuu wa mwaka jana (2015). Ambopo vibaraka wa Tanganyika katika Zanzibar walikataliwa kabisa na wananchi wa Zanzibar katika uchaguzi wa urais, wawakilishi na madiwani. Ni jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania tu ndilo ambalo limehakikisha kwamba vibaraka hawa waliokataliwa na wananchi wao wanaendelea kubaki madarakani.

Kwa maoni yetu Mh Spika katika mazingira haya tatizo la msingi la Zanzibar sio Jecha Salim Jecha wala ZEC wala Ali Mohamed Shein. Hawa ni vibaraka tu wasiokuwa na nguvu wala uhalali wowote. Bila ya nguvu ya Tanganyika vibaraka hawa hawawezi kudumu madarakani kwa muda mrefu. Tatizo la msingi ni ukoloni wa Tanganyika kwa Zanzibar ambao umevikwa Joho la Muungano. Bila kulivua Joho hili na kushona jengine badala yake Zanzibar haitakuwa huru na itaendelea kutawaliwa na Tanganyika kisiasa, kiuchumi na kijeshi.

Tundu Lissu.
Zanzibar ni nchi huru lakini ikumbukwe hakuna Uhuru usio na mipaka
 
Kama Zanzibar ni koloni piganieni uhuru basi. Ombeni msaada AU na hata UN.

Mnajua mnatawaliwa lakini mmejilaza tu kimwinyi. Basi wengi wenu wanafurahia hicho unaita ukoloni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom