Ukoloni wa miamala haukubaliki; wananchi tukiwa na msimamo tunaweza kuupinga kwa nguvu utapeli huu; Kapu la VAT 18% linatosha wagawane huko

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,252
21,345
Baadhi ya mambo ukiyatafakali yanadhihilisha wazi baina yetu bado tuna imani za kikoloni kichwani!

Elimu haijatukomboa kabisa, hatuna ubunifu kichwani kabisa! Ni bure kabisa!

Hivi kazi ya VAT ni nini? Na matumizi ya fedha hiyo ni yepi?

Hivi kuna sababu gani ya mimi kukatwa 18%ya VAT, Halafu tena nikatwe na takataka zingine?

Mfano!
Ninunue umeme wangu kwa ajili yangu mwenyewe ambapo nitakatwa 18% VAT!
Halafu mimi huyuhuyu Inakuwaje tena unikate hizi takataka za 3% ya REA, 1% ya EWURA?

Kwanini hizo takataka wasinge gawana hukohuko kwenye 18% ya VAT? (Yaani mfano wagegawana hivi 1% mamlaka za mashirika-regualatories, 2% Manunuzi ya machine/magari, 2% mafuta,2%REA, 5% mishahara,2% ujenzi, 2% madawa , 2% elimu etc )
Na kama Pesa haiwatoshi! Wapunguze mashirika yanayojiendesha kwa hasara!

Gharama za mashirika zingefutwa zote, zikaitwa kuwa Regulatory authority ili kuepusha mashirika kuendelea kuitia hasara serikali pasipo ubunifu.

Mfano, Tanesco wabaki kuwa wasimamizi (power authority) halafu makambuni ndiyo yasambaze umeme n.k

Hii itapunguza mzigo wa kuendesha serikali na kuongeza uwajibikaji kwasababu makampuni yatafanya kazi hiyo!

Hii ni mifano tu na kama hiyo VAT itaonekana ni ndogo au kubwa basi inaweza kuboreshwa ili iwe kapu moja la kodi!

Lakini hii ya kukatana TOZO kila kona ni utapeli wa kimamlaka kabisa!

VAT NI SAWA NA MAHARI YA POSA !

Unapotaka kuoa unatajiwa mahari (package) yenye mnyambuliko wooote ndani Mfano 4% mkaja wa bibi,7 kanzu ya bamkwe, 2% beberu la mjomba, 3% kitenge cha mama, 4%posa n.k JUMLA KIASI FULANI ni TOTAL VAT UNALIPA!

Sasa baada kulipa mahari sitarajii tena twende kununua gauni la bi-harusi halafu usewe bei ya gauni laki tatu lakini pia kuna TOZO ya laki moja ya beberu la mjomba! huu NI UTAPELI

Haya tukiachana na hizo takataka kujirudia!

Kuna kosa jingine la kodi kuingilia bajeti ya mlaji (CONSUMER BUDGET)

MFANO Tuliambiwa kuwa LUKU maana yake ni TUMIA KADRI UNAVYOTUMIA!

sasa inakuwaje mimi mwenye bajeti yangu ya elfu 20000/= tena nawasha taa kwa machale ili umeme usiishe, unanibebeshaje tena mzigo Mwingine wa 5000 wa REA, EWURA n.k? WHY? yananihusu nn mimi!?

HAYA YOTE TISA! Nyumba hazifanani thamani, wa huko mjini ananyumba ya milioni 100, kwenye kiwanja chenye bei ya mamilioni, inakuwaje unawalipisha kodi bei moja ya jengo SAWA na mtu wa kijijini mwenye nyumba ya udongo?

Hii kodi ya jengo unayokusanya kwa fratrate je kuna utaalamu gani hapo wewe kama msomi umeutumia kuamua hawa wawili walipe kodi SAWA? Kodi ya jengo mjini inafananaje na kijijini huku?

Kodi ya jengo unapoibandika kwenye LUKU Pasipo kufanya USAJILI MAALUM!

Maana yake Unakwenda kuwatoza kodi ya jengo hadi wajasiliamali walio na vibanda vingi stendi na masokoni ili nao walipe kodi hiyo sawa na yule wa masaki?

Tengenezeni kodi zenu pasipo kuingilia faragha za watu?
Kitendo cha kumfuata mtu kwenye LUKU pasipo utaratibu nikuingilia UHURU WA BAJETI YA MTU!

Wekeni utaratibu wa kuyasajili kwanza majengo yote, ili pale mwenye nyumba asipolipa kwa mwaka, mpate haki ya kumbebesha hata penalty kwasabu ndiyo mlengwa!

Mnaweza hata ku- Link hizo nyumba(mita namba na TRA) ili pale mwenye nyumba asipolipa LUKU Igome kununulika UMEME hadi pale atapoleta clearance na malipo kutoka TRA!

EPUKENI KODI ZA KITAPELI!

Halafu kama mtakumbuka vizuri moja ya sababu ya kufuta ile monthly service charge kwenye LUKU mwaka 2015 ilikuwa na lengo zuri la kuipa hadhi LUKU

Sababu ilikuwakumfanya mtumiaji ajisikie raha KULIPIA UMEME KADRI ANAVYOTUMIA! yaani kutokumzonga zonga kwenye bajeti yake ya lazima, umeme ni kama unga wa kula, kwamba mtu anabajeti ya unga robo, na wewe unaukata unga huo huo je unataka AFE?

Na sijui TLS huwa mnafaida gani kama tunafanyiwa utapeli huu na nyie mpo!
 
Wapunguze pia mlolongo wa viongozi angalia mkoa mmoja unautitiri wa viongozi mara rdd mkurugenz etc
 
Sas mm nauliza na wale ambao tayar wameshalipa kodi ya pango je bado tena wanatakatwa kwenye luku?
 
Umenyambua vizuri sana, ila kweli hawa TLS kazi yao hasa ni nini tofauti na kugombana na wanasiasa
TLS yenyewe inaongozwa na mstaafu, tena mwenye itikadi za kiccm! Halafu tutegemee maajabu!! Labda ingekuwa ile TLS ya akina Tundu Lissu.
 
Sasa inafaida gani kwetu watanzania
Kwa sasa na yenyewe ni tawi tu la ccm kama ilivyo kwa vyama vya wafanyakazi! Kote huko wameweka vibaraka wao. Hivyo haina faida yoyote ile.

Na kama huamini, subiri uone kama watatoa hata tamko tu la kulaani huu uhuni tunao fanyiwa Watanzania.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom