Ukodishaji wa ndege za serikali, Risiti za Salma Kikwete

Nilimwambia wifey nyumbani wakati tunaangalia news kuwa hakuna risit pale

Ukiangalia kwa makini utagundua wino hauna siku tatu nyuma. new and fresh invoice.
Wanatuibia hawa.

Kama wanasema kuwa viongozi wa serikali ndo wanajipendekeza kwenye msafara wa mama Salma. basi tuwaunganishe kwenye kesi ya msingi ya kutumia rasilimali za umma kisiasa. pamoja na uzembe ukiambatana na matumizi mabaya ya ofisi ya umma.
 
Wakuu

Nimewasoma ila naomba niwakumbushe mambo machache ambayo wengi wenu vijana hamyafahamu na ni kwa sisi wazee tunaweza dadafua:

Kwa kifupi Wakala wa Ndege za Serikali, ilizinduliwa mwezi Mei, 2002 kutoka kilichokuwa Kitengo cha Ndege za Serikali na ina majukumu yafuatayo:

1.Kumhudumia Mhe. Rais na Viongozi Wakuu wa Serikali.

2.Kusimamia, kutunza, kuendesha na kuendeleza ndege za Serikali pamoja na karakana yake.

3.Kutumia nafasi ya ziada kwa kutoa huduma kwa umma kwa msingi wa biashara.

4.Kutoa ushauri kwa Serikali juu ya mafunzo ya wafanyakazi wake na shughuli za usafiri wa ndege kwa jumla.

Baada ya kusema hayo naomba kuchangia mjadala huu

1.CCM wako sahihi kabisa kukodi ndege ya serikali kutokana na kifungu cha tatu hapo juu na yeyote yule anaweza kufuata utaratibu wa kukodi ndege za serikali.

2.Sifahamu ni gharama zipi ambazo mtu anatakiwa kulipa ili kukodi ndege hizi kwa sasa ila nitafuatilia na kuwapa majibu baadaye

3.Dr. Slaa anatakiwa ajenge hoja nyingine za kuleta mapinduzi na hili ndiyo jukumu kubwa alkilokabidhiwa na watanzania.

4.Asipoachana na kukurupukia hoja za mafisadi na kuendelea kuwaambia wananchi mambo ambayo hayawagusi kila siku basi wapinzani wataendelea kushindwa vibaya.

5.Mkuu Mwanakijiji utakubaliana na mimi tatizo la wagombea wa upinzani ni kukosa 'focus' katika kunadi sera zao na siku zote hubebwa kirahisi na propaganda za chama cha mapinduzi(CCM).

6.Wananchi wa vijijini wanapenda kusikia utawaletea maji,umeme utajenga shule na siku zote CCM imekuwa inashinda kwa kufanya hivi ila tatizo la wananchi wanashindwa kuchagua watu watakaoleta mabadiliko.kwa sasa kuna CDF ambao kama ukitumiwa vizuri basi unaweza kuleta mabadiliko madogo madogo kwanza katika kila jimbo.

7.Suala la risiti siyo hoja sababu wana uwezo wa kulijibu.CHADEMA wajipange zaidi kuwaleza wananchi nini wanaweza kuwafanyia na kwa kipindi gani

8.siku zote maendeleo yatakuja pale viongozi watakapoweza kuwajibishwa kwa kushindwa kutekeleza kile ambacho huwa wanakihaidi.kuwepo adhabu kali kama kunyongwa,kutolewa macho ama kukatwa mdomo na koromeo ili watu wajue uongozi si lelemama!

Wenu Mkuu Gembe!
Gembe

Toka nianze kukusoma sijawahi kuona unakuja na hoja dhaifu kama leo,
Kwanza umeonyesha udhaifu kwa kufikiri Mwanakijiji tu ndiye mwenye mawazo mazuri hadi akubaliane nawe je asipokubaliana utafanyaje.
Pili kinachozungumzwa hapa si biashara ya ndege za serikali tu je mazingira ya biashara yenyewe yakoje.
Tatu unasema wananchi wa vijijini wanapenda wasikie utawaletea umeme nk, je hawapendi kusikia mali ya umma inatumikaje? crap.
8.siku zote maendeleo yatakuja pale viongozi watakapoweza kuwajibishwa kwa kushindwa kutekeleza kile ambacho huwa wanakihaidi.kuwepo adhabu kali kama kunyongwa,kutolewa macho ama kukatwa mdomo na koromeo ili watu wajue uongozi si lelemama!
Unaweza kuyatolea maelezo haya ukirejea uliyozungumza awali.
 
Kachanganyikiwa Msomali wa watu yaani propaganda hata sehemu ambayo haitakiwi duh shame on him


8082869.jpg
 
Luteni taratibu basi umesahau kuwa bado una kadi yao? ebanaeee.. Marando ujiko huooo kiulainiiiiiiiiiiiii kama kumsukuma mlevi
Sitarajii kuwa na kadi ya CCM maishani chama chenyewe kinajifia kama si mwaka huu mwaka kesho, hata hivyo kadi ya chama cha siasa ni mali ya mwanachama tofauti na kadi za kikazi.
 
Hizi siyo risiti, watuonyeshe risiti na walilipa lini, je wamelipa baada ya kuumbuliwa? Invoice (Hati ya Madai) ni ya mwezi wa August kwa hiyo tunatarajia wawe wamelipa hadi kufikia sasa.
 
wapendwa haki anayo huyo mama swala libaki kwenye risiti tu

AOC Holder
spacer.gif
Home › Operator › AOC Holder › Aircraft Operating Certificate Detail
print_icon2.gif


Aircraft Operating Certificate DetailsAOC Number:CAA/AOC/053Name :GOVERNMENT FLIGHT AGENCYBase Address:P.O.BOX 1493 DAR ES SALAAM. ceo@tgf.co.tzApproved Maintenance Base:Engineers:0 Pilots:0 Type of Aircraft / Registration:F-50,PA-31Base / Area of operation:PUBLIC TRANSPORT,AIR CHARTER WITHIN TANZANIA AND AType of Operation:COMMERCIAL AIR TRANSPORTIssue Date:04/03/2010Expiry Date: 05/03/2011

Hivi ndivyo bill za kukodisha ndege zinavyoonekana, zikijieleza wazi kabisa kama ni Charter, je ni humu nchini au ni nje, flight nk kama ilivyoonyeshwa hapa.....LAKINI KINANA ANAFOJI, tena kitoto kabisa. Tena anasahau kwamba huduma imeshatolewa na usingetegemea taasisi ya serkali hata siku moja itoe kibali bila malipo kufanywa hata kama ni First Lady.

Na sidhani kama hao wahasibu wa wakala hawa ni mambumbu kiasi hicho washindwe kutofautisha Proforma Invoice, Tax Invoice na GRN!

Mh Dr Slaa, please badilisha mashitaka, ongeza la forgery, ushahidi huu hapa tele.
 
So what is your point mdau? risiti au invoice what is the different? Hoja ni kwamba where are the funds for thee ndege are coming from. Invoice inaonyesha kwamba CCM wanadaiwa na sio sirikali. Au nimekosea?
 
Hatudanganyiki! Kinana Aonyeshe STAKABADHI YA SERIKALI (EXCHEQUER RECEIPT) au Pay-in slip ya Benki. Siyo Hati ya Madi iliyoandikwa kwa Broken English. Hivi kule Old Moshi Sekondari hakusoma Kiingereza?
 
Wakuu najua hii issue imejadiliwa kwenye post nyingine. Nimeiangalia kwa umakini mkubwa nimeona kinana ameonyesha hati ya madai a.k.a bili, ankara - INVOICE na siyo risiti ya malipo.


154cdtv.jpg


Nilitegemea kuwa kwa kuwa ni ndege za serikali, risiti ilipaswa kuwa ya njano. Ni wazi kuwa hakuna malipo yaliyofanyika ndiyo maana hakuna risiti. Wametumia ubabe tu kuchukue hiyo ndege.

Halafu haina ''approved by'' na ''authorised by''....pia kulipaswa kuwa na makataba...unapo ''hire'' kitu ni muhimu kuwa na mkataba:eyebrows:
 
So what is your point mdau? risiti au invoice what is the different? Hoja ni kwamba where are the funds for thee ndege are coming from. Invoice inaonyesha kwamba CCM wanadaiwa na sio sirikali. Au nimekosea?

Mkuu mwongo hunaswa kwa vitu vidogo mno, kwa kuwa hata source of fund hawawezi kusema though we know ni hazina ya taifa. Ili wasiendelee kubanwa kwa kukurupuka kinana anatuonyesha invoice badala ya kutuonyesha risit kuwa wamelipa.
and that invoice siamini kuwa imetolewa na government agency, it is too local. Hiyo lugha kwenye maelezo yake ni mushkeli mtupu-being cost of hiring charges.

Kuazima assets za serikali ndiyo kunafanyika hovyo hovyo hivi kama kununua laptop kariakoo??
 
Hehehehe
Nilisema ngoma bado ipo LELE
ngoja mwangwi uanze kusikika.

Pamoja na kulindwa na wanaUSALAMA waliojazana ktk idara za serikali lakini wameshindwa kufahamu kuwa ndani ya nchi kuna wananchi wenye kuipenda nchi bila hata ya KIAPO cha utii
 
Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli,iwafae maishani"

.... "Kama mnataka mali, mtayapata shambani"


Sijui wamekwisha lisahau hili shairi?
 
Wakulu, nina maswali mawili matatu hivi::confused2:

1: Kwanini CCM wamkodie ndege mke wa mgombea?
2: Hivi NGOs zinaruhusiwa kujihusisha na siasa?
3: Hivi WAMA (NGO) ina-budget ya uchaguzi wa CCM?

Ni hayo tu.
 
Kinachosikisha zaidi waTZ anaoweza kudadavua mambo kama haya wapo wachache sana,wengine wote wadanganyika hawaelewi hata maana ya invoice ni nini..

na hao wachace wanaoweza kudadavua mambo, hawachukui hatua yoyote zaidi ya kulalamika na kuuzunika.
 
Hivi hiyo ukodishaji wa ndege ipo kwenye bajeti yao ya uchaguzi?
Na yale magari wanayotumia wakuu wa wilaya ktk kampeni za ccm yamekodishwa kwa risiti feki kama hizi au ndo ile Boss yupo right hata akikosea yupo right
 
Kinachosikisha zaidi waTZ anaoweza kudadavua mambo kama haya wapo wachache sana,wengine wote wadanganyika hawaelewi hata maana ya invoice ni nini..

Na hichi ndicho CCM inategemea kushinda -- yaani umbumbumbu wa Watz ambao umeletwa na miaka 50 ya CCM. Imeshindwa kuwaelimisha, haitaki kuwaelimisha kwani wakielimikma kuna sikum watawatimua madarakani.
 
Back
Top Bottom