Ukodishaji wa ndege za serikali, Risiti za Salma Kikwete

Wakuu issue ya kukodi ndege hizo inawezekana. Kitu ninaweza kuomba kama Kinana anao ujasiri wa kuonyesha kila kitu in black and white aturuhusu tukague kama ndege hiyo ilitumikaje na kwa safari za lini, kwendas wapi na kwa kipindi gani. Lazima tutagundua kuna kuchakachuliwa tu.
Hizo risti hazionyeshi ni kwa safari za kwenda wapi na wapi maana watumishi wa CCM wamefanya safari nyingi sana mbali na ile ya mama Kikwete.
Tunaomba tuone na hiyo ya choppers hizo tatu zinazozunguka hewani na huyo mgonjwa.
 
uuuwiiii, wanajilia nchi kama hawana akili nzuri, tutafika kweli na wizi huu, yaani zote hizo kwa kilaza huyo?
 
Wakuu tuache ushabiki lakini kwenye hili Kinana inabidi awajibike kwa kuwadanganya watanzania na possibly kufanya forgery. CCM need to immediately come clean on this..............

Inawezekana vp risiti (invoice) iliyotolewa tarehe 31/08/2010 ikawa na serial no. 00868727

na ile iliyotolewa tarehe 14/09/2010 ikawa na serial no. 00867609

Kama kawaida yao kuchukulia mambo rahisi rahisi na kwa utetezi rahisi watasema kuna vitabu vya risiti (invoice) zaidi ya kimoja but why?????? Govt flight agency yenye ndege mbili tu iwe na vitabu viwili? Is that place that busy that much? Hapana hapa Kinana umechakachua tu, na kwa utaratibu wa kibongobongo usikute kuna jamaa alipewa hiyo kazi ya kuafuta risiti (invoice), he got them na no body akagundua upuuzi huu kwa sababu ya desperation. Vile vile by the look of first 4 numbers very likely ni kutoka kitabu kimoja au vinavyoongozana. Sasa iweje the ya mbele iwe ya mwanzo??????

Yaani hata mwalimu wangu in the 80's was smatter than this kugundua forgery za tiketi zan mabasi.

Nimewahi kuona hapo Tz watu wana birth certificate zilizotolewa Dec 25. au May 01, kama ile akaunti ya Tangold ilivyofunguliwa.




Risiti (invoice) iliyotolewa tarehe 14/09/2010




Risiti (invoice) iliyotolewa tarehe 31/08/2010

Note: Mods baadae changanya hii thread na nyingine zinazofanana
 
Stakabadhi za chama na serikali katika malipo ya kigeni (dollar)... halafu watu haohao wanahimiza matumizi ya shillingi kwenye majukwaa??!! Rife hypocrisy!!
 
Nilijua tu watanasa kwenye tundu bovu.
Hawa jamaa wamezoea kuwazungusha watanzania kama magari mabovu na sasa hata hawafanyi kazi kitaalamu. Kinana kafanya makosa kibao sana ila hili la risiti lisipompeleka ukonga basi sijui tena.
 
Nilijua tu watanasa kwenye tundu bovu.
Hawa jamaa wamezoea kuwazungusha watanzania kama magari mabovu na sasa hata hawafanyi kazi kitaalamu. Kinana kafanya makosa kibao sana ila hili la risiti lisipompeleka ukonga basi sijui tena.

Yaani ni makosa ya kipuuzi kumtetea mtu amabaye logically hakutakiwa kabisa kuwa subject ya kampeni!!!!
 
Kinachoshangaza ni kuwa stakabadhi ya zamani ina nambari (serial numbers) mpya na ile stakabadhi mpya ina nambari za zamani.. Hii ina maana kwamba waliruka baadhi ya stakabadhi kutoa ya kwanza? au ndio mchezo ulivyochezwa..
 
stakabadhi za chama na serikali katika malipo ya kigeni (dollar)... Halafu watu haohao wanahimiza matumizi ya shillingi kwenye majukwaa??!! Rife hypocrisy!!


tatizo letu watanzania mambo ya hatari tunayafanyia masihara. Mfumuko wa bei katika miaka mitano ya utawala wa j k kati ya 2005 hadi 2010 ni jambo ambalo limeongeza umaskini na dhiki kwa watanzania wanyonge wengi wao wakiwa wafanyakazi na wakulima, ambapo bei za bidhaa mbali mbali ikiwemo vyakula, bidhaa muhimu, madawa, mafuta n.k vimekuwa vikipanda bei kiholela sambamba na kushuka kwa thamani kwa fedha yetu mbele ya dola ya kimarekani na fedha za nchi zingine.

kila mmoja wetu anakumbuka upandaji wa bei za bidhaa mbali mbali ulivyoweza kudhibitiwa kuwa katika kipindi cha miaka 10 ya ben mkapa. Hivyo hata kama mishahara ya wafanyakazi na bei za mazao ya wakulima havikuwa vya juu lakini wananchi wanyonge kwa kiwango fulani waliweza kumudu maisha.

wataalamu wa uchumi mara kwa mara wamekuwa wakitaja kuwa moja ya sababu kubwa za kuwepo kwa mfumuko wa bei katika utawala wa j k 2005 -2010 ni kushuka kwa thamani ya shilingi ya tanzania kunakosababishwa na mahitaji makubwa ya fedha za kigeni yaliyopo hapa nchini hususan katika maduka ya ya fedha zakigeni yaani buruea de change.

Moja ya njia kuu ambayo wawekezaji na wafanyabiashara huitumia kuhakikisha kuwa thamani ya shilingi ya tanzania inashuka daima ni kudai malipo ya bidhaa wanazouza na huduma mbali mbali wanazotoa hapa nchini kwa fedha za kigeni. Hali hii huwalazamisha wanunuzi wa bidhaa na huduama hizo kukimbilia katika maduuka ya fedha za kigeni kununua dola za kimarekani na fedha zingine za nje na hivyo kuwepo mahitaji makubwa ya fedha za kigeni.

Kwa mujibu wa sheria za fedha za kigeni za tanzania ni makosa kudai fedha za kigeni kwa bidhaa au huduma inayouzwa hapa nchini. Aidha kanuni za kusimamia uchumi nazo zinakataza hali hiyo iwapo serikali makini inataka kudhibiti mfumuko wa bei na kuwafanya wananchi wake waweze kuwa uwezo mkubwa zaidi wa manunuzi (purchasing power). Kwa lugha ya kigeni hali hii inaitwa "dollarisation of the economy"

kwa kuwa ni kinyume cha sheria kudai na fedha za kigeni kwa bidhaa na huduma zinazouzwa nakununuliwa hapa nchini. Kitendo cha serikali ya ccm chini ya jk kuruhusu hali hii kushamiri na kiasi cha ccm yenyewe kushiriki katika ufisadi huu ni kieleelzo dhahiri cha ccm kupoteza uwezo wa kuendelea kusimamia uchumi wa nchi kutokana na kuzingirwa kabisa na ufisadi.

Ni kutokana na wawekezaji na wafanyabisahara kuwa na mahusiano ya karibu na ccm na viongozi wake ndio maana serikali ya ccm chini ya j k inawaruhusu wawekezaji na wafanyabiashara kuwakamua wananchi kwa kuruhusu matumizi ya fedha za kigeni hapa nchini kunakosababisha kushamiri kwa mfumuko wa bei.

Sasa kitendo cha ccm ambayo inatafuta ridhaa kuendelea kutawala kukubali kudaiwa kwa dola za kimarekani kwa huduma ambazo zimetolewa hapa nchini kinyume na sheria za fedha za kigeni na kanuni za uchumi ni kitendo cha kuthibitisha kuwa chama hicho kimegeuzwa kuwa kipofu kutokana na uswahiba katia yake na wawekezaji na wafanyabiashara hapa nchini.

Ni kutokana na ccm kuruhusu mamabio kama haya wafanyabiashara karibu wote hapa nchini wanajitanabaisha na ccm kwa kuvaa fulana, khanga na kubeba mabango na kupandika picha za wagombea wa ccm katika sehemu zao za biashara, magari, makazi n.k.

Naomba wagombea wote wa chadema na vyama vya upinzani wawafafanulie wananchi nchi nzima mahusiano ukiukwaji huu wa sheria za fedha zakigeni na kanuni za uchumi zinazosababisha kuwepo kwa mfumuko wa bei hapa nchini na kuathiri uwezo wa manunuzi wa wananchi wanyonge wakulima na wafanyakazi
.

kwa hali tuliyofika watanzania hakuna tiba ingine zaidi ya hali ni kuinyima ccm na wagombea wake wote kura katika uchaguzi mkuu wa 2010, na kuchagua wapinzani hususan kutoka chama makini chadema ili kiunde serikali na kuongoza bunge ambalo litabadili katiba ya nchi, kupunguza madaraka ya rais, kupunguza ukubwa wa seruikali, kuondoa wakuu wa mikoa na wilaya, kupunguza matumizi ya serikali, na kuthibiti wizi, ubadhirifu na ufisadi wa aina mbali ikiwemo.

Ikiwa mwalimu nyerer aliyeanzisha ccm aliweza kumpa kura mgombea kutoka nccr mwaka 1995 kwa sababu aliyesimamishwa na ccm alikuwa na tuhuma za kufilisi ushirika, ni nini kinwafanya watanzania wengine washindwe kuviamini vyama vya upinzani katika kurekebisha mustakabali wa taifa letu? Tuache kujipumbaza kuwa tanzania haiwezi kuwepo bila ccm; ccm ndio haiwezi kuwepo bila tanzania
 
Wakuu nakubaliana na yote yaliyoandikwa hapa lakini hoja ya kwa nini ndege ya serikali inakodishwa nadhani si nzito sana. Ndege hizo hukodiwa na mtu au kampuni yeyote ile hela yako tu. Nakumbuka nilipokuwa bongo kampuni yetu (Mining exploration Co.) ilikuwa ikikodi ndege kutoka Govt flight Agency mara nyingi tu kwenda na kurudi Mwanza.

Hivyo basi naomba tustiki kwenye hoja nyingine jamaa wasijecapitalize kwenye hii simple anomaly

NYAMBALA-tupe maoni yako kwa CCM kukubali kudaiwa kwa fedha za kigeniin the light of the ever increasing inflation
 
haya sasa mi simo, simo kabisa, risiti za serikari, mbona zina rangi ya njano wadau ,kwani hata baadhi ya agency kama temesa hawatumii hizo risiti, iweje hii agency na ndege ndo watumie hizo, mi simo simo, hadi risiti zinachakachuliwa.
 
Kinachotakiwa Kinana akaonyeshe mahakamani kama risti ni za kweli au kugushi itajulikana si vitabu vitaletwa, na vile vile watuambie walianza lini kukodi ndege za serikali ina maana serikali inafanya biashara ya kukodi. Mimi nafikiri Chadema wasonge mbele tu wapeleke suala hili mahakamani ili waendelee kuwaweka CCM kwenye defensive position wakati wote wa kampeni.
 
Wakuu tuache ushabiki lakini kwenye hili Kinana inabidi awajibike kwa kuwadanganya watanzania na possibly kufanya forgery. CCM need to immediately come clean on this..............

Inawezekana vp risiti iliyotolewa tarehe 31/08/2010 ikawa na serial no. 00868727

na ile iliyotolewa tarehe 14/09/2010 ikawa na serial no. 00867609

Kama kawaida yao kuchukulia mambo rahisi rahisi na kwa utetezi rahisi watasema kuna vitabu vya risiti zaidi ya kimoja but why?????? Govt flight agency yenye ndege mbili tu iwe na vitabu viwili? Is that place that busy that much? Hapana hapa Kinana umechakachua tu, na kwa utaratibu wa kibongobongo usikute kuna jamaa alipewa hiyo kazi ya kuafuta risiti, he got them na no body akagundua upuuzi huu kwa sababu ya desperation. Vile vile by the look of first 4 numbers very likely ni kutoka kitabu kimoja au vinavyoongozana. Sasa iweje the ya mbele iwe ya mwanzo??????

Yaani hata mwalimu wangu in the 80's was smatter than this kugundua forgery za tiketi zan mabasi.

Nimewahi kuona hapo Tz watu wana birth certificate zilizotolewa Dec 25. au May 01, kama ile akaunti ya Tangold ilivyofunguliwa.




Risiti iliyotolewa tarehe 14/09/2010




Risiti iliyotolewa tarehe 31/08/2010

Note: Mods baadae changanya hii thread na nyingine zinazofanana
Hapa mkuu wangu tumeumizwa vibaya sana. haiwezekani risiti ya tarehe 31/8 (00868727) iwe kurasa mbele ya ile ilotolewa baadaye tarehe 28/9 (00867609). Hapa kumefanyika mchezo.
 
Kisha basi kibaya zaidi ni hiyo hiyo serikali inayodai kwamba wananchi wasitumie Dollar kulipa au kupokea malipo!...wao ndio kwanza wanalipa na hata kuonyesha kwa majivuno.
Huu ni mfano gani kwetu?
 
haya sasa mi simo, simo kabisa, risiti za serikari, mbona zina rangi ya njano wadau ,kwani hata baadhi ya agency kama temesa hawatumii hizo risiti, iweje hii agency na ndege ndo watumie hizo, mi simo simo, hadi risiti zinachakachuliwa.
Risiti za serikali karatasi zake ziwe na quality mbovu namna hiyo kama risiti unayopewa unaponunua kilo ya maharage, CCM wamebugi step huo ni uongo wa mchana kweupe.
 
Namshukuru Dr. Slaa kwa uamuzi wake wa kumshaki Mama Salma Kikwete. Hilo limesaidia kufichua uozo mwingine tena wa hawa viongozi wa CCM. Wamezoea kufoji mno? Hawajazoea utawala wa kisheria. Kama hawangekuwa wamefoji, wala malipo hayangekuwa kwenye dola.

Hakuna msomi au accountant ataandika UDS 15,000/=. Hawachanganyi shilingi na dola. Hiyo no forgery ya watu hao hao wanaofoji documents za kuingiza meno ya tembo kwenye meli. Wamezoea.
 
Hapa mkuu wangu tumeumizwa vibaya sana. haiwezekani risiti ya tarehe 31/8 (00868727) iwe kurasa mbele ya ile ilotolewa baadaye tarehe 28/9 (00867609). Hapa kumefanyika mchezo.

Mkuu it is just a big joke!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom