Ukodishaji wa ndege za serikali, Risiti za Salma Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukodishaji wa ndege za serikali, Risiti za Salma Kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanamayu, Sep 15, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  Bwana Kinana hivi mapato yake yanaonekana kwenye vitabu vya CAG? Au ndio mradi wa watu binafsi? Hivi lengo lake ni kukodishwa tu? Hivi gharama za CCM za mgombea urais hazijazidi kweli? Ndege, helikopta tatu, Nuclear scientist, magari, malori na mabasi ya kubeba wasikilizaji?

  Kwa kweli likizo hii ya X-mass nataka kuikodisha, jamani narudia tena kuomba utaratibu wa kuikodi na bei!
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,356
  Likes Received: 3,123
  Trophy Points: 280
  Haya ndiyo matunda ya kuwa na rais km kikwete mwenye tamaa ya kuongoza wakati anajua hana uwezo.........tuchukue hatua tusimpe kura anachezea sana pesa zetu japo yeye anasema alicheleweshwa kupewa madaraka kwa hiyo tutamkoma ndiyo maana mambo yanapokwenda kombo na amabayo ni ya msingi anakaa kimya km vilke nchi haina rais.......ina rais dhaifu.......hafai.........
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Huipati ng'o.....anaitumia Salima kwa sasa....:confused2:
   
 4. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hivi hii ndo ndege ya rais kwa ndani??? tobaaaaaaaa!!:becky:
   
 5. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  ukishaikodi naomba lift!
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  [​IMG]

  Wakuu kwa hisani ya wavuti.com, Kinana ametoa baadhi ya risiti za kukodi ndege kwa ajili ya mama Salma. Yaani wameingia wenyewe, baada ya kuwa provoked kidogo tu na Dr. Slaa. And now is an open proof that CCM is out of touch! And they deserve to be vote out for good.

  My Take:

  1. Kama huyu mama anatumia $15,000 for only 5 hours flying kumkampenia mumewe what about mumewe tunayeambiwa sasa hivi anatumia helikopta tatu?????????

  2. Mama Salma ni nani kwenye CCM mpaka they dare to go this far? I would have thought Mwinyi, Mkapa wangetumika kwa kampeni of this high standard in Tz terms.

  3. Nyerere angekuwa hai CCM wangethubutu kufanya ujinga huu?

  4. Hizo risiti si "magumashi" kweli???????

  5. Wakuu naomba tujumuishe na zile picha za Tanzania zaidi ya uijuavyo
   
 7. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hey, wakuu.
  Nimegongana na hizi picha ikiwa ni ishara ya SISIEMU kujibu mashambulizi ya Slaa kuhusu safari ya Mama Salma Kikwete ambapo alitumia ndege ya serikali kama ilivyodaiwa na Dr. Slaa hivi karibuni.
  Wataalam vipi hiyo risiti imekaaje au ndo risiti za serikali zinakuwa. Hakuna muhuri wa moto? Poor my country Tanzania.
   

  Attached Files:

 8. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo kila mtu anaweza kukodi ndege ya serikali!! Itabidi nifungue biashara hiyo, nakodi kisha naifanyia biashara kupeleka njugu zangu kule Mtwara.
   
 9. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Huku kutapatapa kunaweza kuwapeleka kubaya sasa. Ina maana serikali inafanya biashara ya kukodisha ndege? Na hizo fedha zinapelekwa kwenye account gani? Namna nyingine ya kujibu mambo inatia mashaka umakini wa hawa watu. Imefikia mahali kuwa nchi hii inaendeshwa kwa matakwa ya mtu na familia yake. Serikali inafanyaje biashara ya kukodisha ndege? Ina maana ikitokea mtu akataka kukodi ile convoy ya magari ya Rais kwa ajili ya harusi inawezekana? Hawaachi kutushangaza kwa kweli...
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mzee wa Meli amechakachua ! Ninaishia kucheka tu na Msomali anavyofanya mambo

   
 11. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu, hilo ni swali zuri sana.
  Kwa kuwa serikali inafanya biashara, then twaweza kukodi hiyo migari just for kupeleka posa ukweli....ahahaha hahaha ahaha:becky:
   
 12. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mbona wameonyesha risiti na ndege peke yake, na ile mishangingi ilitolewa na WAMA au CCM? This time mtaeleza kila kitu.
   
 13. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,424
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Lakini jamani, unawezaji kuruhusu ndege kuruka bila kulipwa, hii ni invoice na pamoja sio mtaalamu wa mahesabu ya fedha, sioni aliyeandikiwa. Na itakuwaje tarehe ya madai yawe ni siku ile ile ya kusafiria. Je viwango vya kukodisha vimepangwa na nani. Mtu mzima anapoamua kudanganya kwa kufoji virisiti na invoice tunaelekea pabaya. Nisingeweza kulala nikijua nimefoji kwa kiasi hicho. Kwa nini wasiseme ndio tumetoa ndege kwa Mama wa Taifa, sidhani Slaa angeweza kumpiku huku ndani ya mahakama. Hii ikienda mahakamani ni rahisi kumshinda!
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hawa jamaa ovyo kabisa! Hivi siku mchungaji nikienda na pesa zangu nataka kutumia viwanja vya Ikulu kufanyia mikutano yangu ya uponyaji nitaruhusiwa!
   
 15. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Ni invoice kwa Katibu Mkuu wa CCM. Kuna matatizo haya:

  (1) Kitengo cha ndege za serikali si cha biashara. Hakina kibali cha kufanya biashara.

  (2)Serikali ya CCM hairuhusiwi kufanya biashara na CCM. Kunakuwepo na conflict of interest.

  (3) Sidhani Mtendaji Mkuu wa hicho kitengo angeandika USD 15,000/=. Hiyo alama" /= " ni kifupisho cha "shilingi".
   
 16. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ama kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza...!!

  Jamani, naomba mtu mwenye namba ya Ndg. Kinana anipatie, ninahitaji kukodisha BMW 3 (X5) za Ikulu kwa ajili ya kipaimara mpwa wangu!!!

  Kama ndege ya serikali imeweza kukodishwa, je kuna vingapi vimesha kodishwa na hatujaambiwa?? Hela zinaenda hazina??

  Mmmmh....Kwa mtindo huu hatuchelewi kukuta hata baadhi ya vyumba vya Ikulu vimepangishwa kama guest house...!!
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hizi risiti zinakuwa forged pale nyuma ya Billicana karibu na Breakpoint. Nadhani hata ofisi za CCM wana uwezo wa kufoji.
   
 18. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mambo ya Ajabu sana haya...

  Hiyo Risiti ukiiangalia kwa makini utagundua ina walakini...

  1. Haisemi imetolewa lini.

  2. Ililipiwa lini

  3. Imelipwa na nani

  4. Je inawezekana kukodisha ndege ya serikali kabla ya malipo maana inaonekana kukodishwa kulifanyika 28/08/2010 na malipo yakafanyika 31/08/2010

  5. Risiti pia haizungumzii ni ndege gani imekodishwa kama ambavyo ilikuwa described na akina slaa inasema air fleight number... sasa kwa wanao fanya kazi airport watakubaliana kwamba fleight number inategemea na siku ndege inaposafiri ndo itajulikana...

  6.Nilifikiri kwamba serikali inapiga marufuku matumizi ya dollar... sasa iweje leo hii malipo hayo yafanyike kwa dollars ... kwa nini sasa they dont practise what they preach?

  7. Usd 15000 Kwa masaa matano? Kwa kazi gani anayofanya huyo mama... hii inaonesha kwamba hawa watu ni anasa tu..Dollar elfu 15 kwa kazi gani anayofanya maana WAMA ni charity tu na sidhani kama sisi wachangiaji wa hiyo charity tungeruhusu matumizi makubwa ya ku-hire private govt jet ya namna hiyo... huu ni mfano mmbaya wa public figures kama hawa... they are setting dangerous examples...hata kama ingelipiwa na CCM... hili pia haliko wazi maana inasema tu Secretary General Chama cha mapinduzi.. sasa sijui ni yeye aliyelipa au ni CCM ... Kama alikuwa analipa wa niaba ya CCM basi tisiti ingeandikwa received from CCM for accounting purposes ndani ya serikali na huko CCM Kwenyewe.

  8. Mwihso Mbona hatujawahi ambiwa kwamba ndege ya serikali ni ruksa kukodi kwa watu binafsi wakiwemo serikali mbadala (wapinzani)?

  Ni hayo tu wakuu... free to make additional observations.
   
 19. K

  Keil JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CCM wanamkodishia ndege Salma Kikwete akiwa kama nani ndani ya chama? Kwa faida gani? Hapo naona changa la macho.

  Kwanini hawakwenda kukodi ndege kwenye kampuni ambazo zinafanya biashara ya usafiri wa anga? Kuna ndege nyingi sana ambazo zinakodishwa na kampuni binafsi.

  Je, serikali ilishawahi kukodisha ndege kwa mtu/taasisi/kampuni nyingine? Wanaweza kutoa ushahidi huo wa kukodisha ndege? Au hii biashara imeanza sasa juzi baada ya Dr. Slaa kuwakomalia?

  Tangu lini serikali imekuwa ikiwatoza wananchi wake malipo in terms of dollars? Maana naona quotation ya bei iko kwenye dollars, na kama ndiyo policy ya wakala wa ndege za serikali, basi risti zake zote zingekuwa zimewekwa sign ya dollar au imeandikwa dollars kwa maneno.

  Hawa jamaa wamekurupuka na wanaji-expose zaidi na kuonyesha utapeli wao kwamba wanajua hata kugushi receipts na proforma invoice.

  Kaazi kweli kweli. Ngoja tuone huyo Mama Kikwete sasa atarudi kwa miguu au watakodi tena ndege ya serikali.
   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wakuu nakubaliana na yote yaliyoandikwa hapa lakini hoja ya kwa nini ndege ya serikali inakodishwa nadhani si nzito sana. Ndege hizo hukodiwa na mtu au kampuni yeyote ile hela yako tu. Nakumbuka nilipokuwa bongo kampuni yetu (Mining exploration Co.) ilikuwa ikikodi ndege kutoka Govt flight Agency mara nyingi tu kwenda na kurudi Mwanza.

  Hivyo basi naomba tustiki kwenye hoja nyingine jamaa wasijecapitalize kwenye hii simple anomaly
   
Loading...