Uko wapi uzalendo wa Tundu Lissu kwa Nchi yake?

Screenshot_20170721-111742.png


try me
 
Mwenyekiti alishawaita wanafiki kama wewe "ng'ombe aliyekatwa mkia" na alikuwa sahihi! Hilo ndio jambo pekee ninalokubaliana na mtakatifu JPM kwa kuwafananisha wanafiki wa design yako na ng'ombe aliyekatwa mkia!
Jpm sio mtakatifu aseeeee unagusa tabaka lingine
 
Asante chief.Ccm imeharibu nchi yetu,imeharibu akili za watu wetu,imeua uzalendo wa watu wetu kwa taifa lao,Ccm imejenga taifa la wàpenda vyama kuliko nchi yao.I hate ccm
Mheshmiwa Mpendazoe, shikamoo!! Kwa sasa nitajikita katika maana ya uzalendo.

Pengine baadae nitarudi kujibu hoja zako zingine. Nimeona msingi wa hoja yako ipo kwenye neno "uzalendo" hadi umehoji uzalendo wa Tundu Lissu (TL) uko wapi.

Nijuavyo mimi uzalendo ni mapenzi ya kujitoa, kuunga mkono na kuilinda nchi yako;utii kwa taifa lako (i.e devoted love, support, and defense of one's country; national loyalty). Hapa hakuna maneno mawili "rais" na "chama cha siasa".

Kwa sababu binfasi, sababu za kisiasa, sababu za kutetea maslahi binafsi, watanzania wengi tena wengi wao ni wasomi wamekuwa wakipotosha maana ya neno "uzalendo". Wao kwenye neon "taifa" au "nchi" wanaweka neon "rais" kwenye definition ya neon uzalendo.

Mark Twain alipata kusema "patriotism is supporting your country all the time, and your government when it deserves it". Pia Edward Abbey alipata kusema "A patriot must always be ready to defend his country against his government".

Hapa utaona utofauti kati ya nini mzalendo anapaswa kutetea; Je ni serikali (including rais) au Je ni nchi/taifa?

Serikali ni watu ambao wapo wema na wabaya lakini nchi/taifa lina misingi na miiko yake ikiwemo demokrasia, utawala wa sheria, umoja, huduma bora za kijamii, amani nk. Je, anayoyafanya TL hata kuhoji uzalendo wake ana-defend nini? Unachofanya wewe Mpendazoe, JPM nk mna-defend nini?

Uzalendo ni "NDIYOOOOO" kwa kila afanyalo Rais hata kama linavunja msingi na mwiko wa taifa letu?

Uzalendo ni kuunga mkono chochote kilicho chema kwa taifa regardless kimefamywa na nani? Kinachopaswa kuungwa mkono ni MTU au KITENDO?
 
Nijuavyo mimi uzalendo ni mapenzi ya kujitoa, kuunga mkono na kuilinda nchi yako;utii kwa taifa lako (i.e devoted love, support, and defense of one's country; national loyalty). Hapa hakuna maneno mawili "rais" na "chama cha siasa".
Nimekuelewa sana!!
 
Wewe ni punguani na una upungufu wa kiakili. Huwezi kumlinganisha mtu mwenye matatizo ya kiakili kama lisu na Yesu Kristu. Tundu Lisu anahitaji msaada wa kiakili kwani alishakula hela za watu sasa anaogopa watamuua iwapo hatajitutumua kuonesha anafanya kazi yao

Jazba ni dalili ya kuumizwa na ukweli. Hata nakubaliana na ww kabisa kwamba Tundu Lisu ni kichaa tena mkubwa sana. Ila hata saa mbovu kuna muda inakuwa na majira sawa. Kwa haya aliyosema na ukichaa wake kapatia mlemle. Huoni ni kichaa lakini hakuna kati yenu anayejibu na kutolea ufafanuzi wa alichokiongea zaidi ya jazba?
 
Wameishiwa hoja wamechanganyikiwa na kutapatapa.

JPM muarobaini wa wapinzani:D.
Moarobaini? Angejibu hoja badala ya kurusha ngumi! Mngekuwa na hoja tungekuwa mbali, hoja yenu kuu ni Kamata weka ndani! Mna hoja gani zaidi ya vihoja? Mtu mwenye Akili hatumii mabavu, hutumia Akili! Hii ndiyo tofauti yetu nanyi, kila kitu mnakimbilia Dolla! Hopeless kabisa! Msingekuwa waoga mngejibu hoja, mngewaruhusu wenzenu wafanye Siasa kama mnavyofanya nyie!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
uzalendo huanza kwenye kuheshimu katiba na sheria za nchi..
yule anayezinajisi hana uzalendo na taifa ni sawa na kuchukia maneno ya baba eti unayempenda..
kudai asilimia mbili huko ni kuhitaji tu hela ili kujenga airport porini..
 
Patriotism siyo kusema ndiyo kwa kila atakalo raisi
Uzalendo unaweza kuonekana kupitia matendo mengi
Ikiwemo kupigania freedom of speech kwa nchi yako,kupigania Demokrasia ,Kupigania uwazi,Equity and Equality na mifumo bora ya utawala wa nchi
Uzalendo ina definition pana na definition mliyonayo nyinyi watawala ni ile inayowapendeza nyinyi tu.
 
Hapo sasa, tena nashukuru Chademakwanza hawakuchukuwa nchi, hawa jamaa hawangekuwa madikteta, wangekuwa kama kina Museveni kama siyo kina Mugabe, wakibisha wewe angalia wanavyoendesha chama chao, kuanzia mwenyekiti wa kudumu, jinsi wanavyochaguwa wabunge wa kuteuliwa uendeshaji wa chama, mapato na matumizi n.k. n.k.
 
Nadhani kuna wanasiasa wa ccm wengi wanaamini na kuaminisha Watu uzalendo ni kumuunga mkono kiongozi kwa kila alifanyalo liwe baya au zuri kwa nchi huo sio uzalendo ni unafiki Wewe uliitwa ngombe aliyekatika mkia je kweli wewe umekatika mkia acha kusema lisu sio mzalendo ametaja majina na nafasi zao na undugu au ukabila wao wewe kanusha unakuja na hekaya zako ili upate uongozi
 
Kwa taarifa yako, huyu mnafiki kwa sasa anachukiwa sana na watanzania, kila mtanzania anajua jinsi anavyotumika na wazungu.
Hii propaganda haiuzi hata kwa Bei ya Tshs 4! Sema CCM mnamchukia, na hii ni kwa sababu from top to bottom uwezo wenu wa kuona ni mwisho wa pua na matumbo yenu! For those who thinks of 1000 years ahead mnawaona vituko! Poleni saaana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikuzote nasema nikisikia neno uzalendo likitumiwa na wanasiasa ujue kuna mtu ata kaangwa na bahati mbaya wengi wao hawajui au wanajifanya kutokujua maana ya uzalendo. Zama hizi usipomuunga mkono mheshimiwa basi wewe si mzalendo, umelipwa na "mabwana" zako, una abudu wazungu etc, halafu hao hao mabwana, wazungu, ndotunawalilia watusaidie kila siku kwa hili na lile. Wazalendo ni wale wanaotaka mtu atawale daima, kwa jina la Tanzania (wenyewe wanaita nia njema)-afanye atakalo (the end justifies the means).
 
Itisha Pres conference na wewe au umtumie Tundu Lisu kama unajiona unaweza kupambana nae
 
Sikuzote nasema nikisikia neno uzalendo likitumiwa na wanasiasa ujue kuna mtu ata kaangwa na bahati mbaya wengi wao hawajui au wanajifanya kutokujua maana ya uzalendo. Zama hizi usipomuunga mkono mheshimiwa basi wewe si mzalendo, umelipwa na "mabwana" zako, una abudu wazungu etc, halafu hao hao mabwana, wazungu, ndotunawalilia watusaidie kila siku kwa hili na lile. Wazalendo ni wale wanaotaka mtu atawale daima, kwa jina la Tanzania (wenyewe wanaita nia njema)-afanye atakalo (the end justifies the means).
Nadhani hii post yako inaweza kabisa kuhitimisha huu mjadala wa uzalendo. Umeeleweka mkuu.
 
Back
Top Bottom