Uko wapi utu wako?

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=1][/h]Written by Stonetown (Kiongozi) // 18/11/2012 // Habari // 15 Comments

dkshein-564x272.jpeg

Dr. Ali Mohammed Shein,
Rais wa Zanzibar
Ofisi ya Rais
P.O.Box 2422
Zanzibar – Tanzania.
Mheshimiwa Rais
Uko Wapi Utu Wako?
Nijambo lililo wazi na lililopo kwenye rekodi kuwa wewe ni mtaalamu mahiri uliyekhitimu katika vyuo vikuu mbali mbali duniani. Kama Wazanzibari ambao hatma ya nchi yetu kwa hivi sasa iko chini ya mikono yako, hatukuandikii kuhusu utaalamu wako; ila dhamira yetu ya kukuandikia ni kuutafuta ubinaadamu au utu wako. Uko wapi utu wako Dr. Shein?
Tunalitilia mkazo suala letu hilo kwa sababu moja kubwa. Nayo ni kwamba hapo mwanzoni ulipopewa madaraka kuna watu waliokubandika utukufu mkubwa. Watu hao walitufahamisha kuwa wewe ni mtu usiyetaka makundi. Aydhan, walitueleza kwamba ukishamaliza salaa zako hutoki nje na kwenda mabarazani. Kwa hivyo, tuna kila sababu ya kutumia vigezo vikali kukutathmini.
Mheshimiwa Rais, historia yako haina mizizi ya ukereketwa. Umeanzia kupanda ngazi za kisiasa kwa kuteuliwa na marais waliopita. Dunia nzima inajuwa kwamba wewe si mtu uliyepikwa kichama. Uongozi umekuteremkia kwa bahati. Ni matokeo ya mazingira ya wakati fulani. Hatudhani kuwa hata kama umewahi kusimamia kiti katika jimbo lolote la uchaguzi. Kama umewahi kufanya hivyo basi hujawahi kufuzu kwani tungelilikumbuka tukio kama hilo.
Tunakumbuka kwamba katika ule uchaguzi uliokupa ushindi wa Urais hujajishughulisha hata kujiandikisha kupiga kura. Siri ya kufanya hivyo unaijua mwenyewe. Mwenye Enzi Mungu akitaka riziki imuangukie mja wake basi ndio hivyo tena hakuna wa kuizuia. Kufumba na kufumbua umekuwa Rais wa Serikali ya Maridhiano inayotambuliwa na wengi kama Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), ambayo kuwepo kwake kumebarikiwa kwa kura ya maoni ya Wazanzibari walio wengi. Kwa muda wa miaka miwili sasa tumekuwa tukijitahidi kuamini kwamba yale mema tuliyoambiwa juu yako yalikuwa si uzushi. Lakini matokeo ya hivi karibuni yametufanya tutokwe na imani hiyo. Tumetokwa na imani hiyo kwa masikitiko makubwa. Jambo ambalo lenye kutusikitisha zaidi ni kuona kwamba wewe Rais wetu mpendwa, tuliyekuamini na kukuthamini umechagua kuwa upande wa wale wasioitakia mema Zanzibar. Ushahidi wa hayo ni vitendo vyako mwenyewe. Miongoni mwa vitendo hivyo vyenye kukatisha tamaa ni:
• Katika hotuba yako ya Eid umetoa pole kwa upande mmoja tu wa waathirika na kuusahau kwa makusudi upande wa pili. Hivyo sivyo inavyotakiwa, ukiwa wewe ni Rais wa nchi.
• Umeamua kukaa kimya huku wananchi wanapigwa, wanakamatwa na wanadhalilishwa kwa kufanyiwa kila aina ya idhilali.
• Wahuni kutoka chama chako (tunaona uzito kutumia neno hili ‘wahuni’ lakini hapana budi) wanahutubia katika majukwaa si matusi tu bali wanatoa matamshi ya kuangamizana raia; matamshi ambayo katika nchi zenye kufuata sheria na kuheshimu misingi ya
haki na demokrasia zingepelekea wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
• Viongozi wa Uamsho wamewekwa vizuizini katika hali isiyokubalika hata kwa sheria zetu sisi wenyewe.
• Tunathubutu kusema kwamba ulionyesha ishara ya kuelemea upande wa wale wenye kuleta fitina pale ulipomtoa katika Baraza la Mawaziri yule kijana aliyefanya kazi kubwa mpaka yakapatikana haya Maridhiano.
Mheshimiwa Rais, unajuwa fika kwamba wengi walishindwa huko nyuma kutufikisha penye utulivu na amani. Kwa kudra ya Mola Wetu na kwa baraka za Rais Mstaafu Amani Abeid Karume pamoja na Maalim Seif Shariff Hamad, Wazanzibari waliweza kuunda Kamati ya Maridhiano chini ya uongozi wa mzee wetu Hassan Nassor Moyo. Naam, Wazanzibari hao wameweza kutupa sote fahari kubwa na kutamka kwa kinywa kipana “Ndio Tumefanya”, “Ndio Tumeweza”. Hapa inabidi tukukumbushe kwamba wewe hukuwamo katika hili. Licha ya hivyo kwa muda mrefu umekuwa ukipokea pongezi kutoka sehemu mbali mbali na kutoka kwa Mabalozi wanaokutembelea.
Mheshimiwa Rais, ikiwa wewe ni mtu muadilifu na mwenye insafu inabidi ujiulize hivi kweli unastahiki pongezi hizo? Ama sisi kwa upande wetu na Wazanzibari walio wengi tunakuuliza nini kinachokuzuia kuienzi na kuitunza Kamati ile? Hivyo wewe kama Mzanzibari mwenye uchungu na nchi yako unaona ni sawa ufanyavyo kuwaachia wahuni wawakashif wajumbe wa Kamati ya Maridhiano, kuchochea chuki na kuleta suitafahamu katika nchi yetu ya Zanzibar?
Mungu akuhidini..
Wazanzibari Wenzako,
Kwa niaba ya Kamati
Hashil Seif Hashil
Zanzibar Committee for Democracy
Gustav Bangs Gade 11st, th
2450 Copenhagen SV
Denmark
17 November, 2012


[h=4]Related Posts[/h][h=3]Urais una mwisho wake – Dr Shein na Kaumu yako.[/h]

[h=3]Taarifa kwa vyombo vya Habari[/h]

[h=3]Tanzania inahitaji Mabadiliko ya Kilimo – CUF[/h]



[h=3]Dr.Shein atetea muundo wa muungano uliopo ?[/h]
[h=3]DR SHEIN YUKO NJIA PANDA?[/h]











[h=3]15 Comments on "UKO WAPI UTU WAKO?"[/h]


  1. mwanafunzi 18/11/2012 kwa 9:08 mu · Ingia kujibu
    Hongera kwa kupeleka ukumbusho.




  2. zinjibar.asli 18/11/2012 kwa 9:21 mu · Ingia kujibu
    Fantastic Message:
    Kwanza kabisa nikupe shukran nyingi ndugu yetu Hashil Seif Hashil pamoja na Zanzibar Committee for Democracy in Denmark kwa kutayarisha barua hii iliyojaa ukweli, hisia na masikitiko yetu wazanzibari popote tulipo dunaini.
    I feel proud & sad at the same time reading this beautiful letter.
    Proud kwa sababu mumeweza kukaa pamoja na kutusemea (WAZANZIBARI) kwa sauti na uwazi ((loud & clear) exactly yalio moyoni mwangu na kwa hili sina budi kukushkuruni sana ndugu zetu wa Zanzibar Committee for Democracy na namuomba ALLAH atuzidishie umoja, mapenzi na success In Shaa Allah.
    But sad at the same time kwasababu sina uhakika message yetu hii itamfikia huyo bwana mkubwa Dr Shein ambae ndio direct addressee wa hii barua. Kwani traditionally kule nyumbani mtu akishakuwa rais or minister inakua kama Mungu mtu, wanajifanya untouchable and unreachable. Kwani naamini layti hizi messages and comments zinawafika japo through their messengers na makarani basi BIIDHNILLAH zingeleta good and positive impact and hopefully malalamiko yetu yangefika tulipoyakusudia but as I said jamaa are far from people’s reach so let’s make DUA hii barua muhimu na adhimu imfikie DR SHEIN in time aweze kuyazingatia tuliyomueleza.
    ZANZIBAR NEEDS PEOPLE LIKE U WA NDANI NA NJE YA NCHI KWA UMOJA WETU TUINUSURU NA TUIENZI ZANZIBAR YETU KWANI TANGANYIKA & WAHAFIDHUNA ARE DETERMINED TO DO THE OPPOSITE.
    GOD SAVE OUR ZANZIBAR




  3. siri 18/11/2012 kwa 9:37 mu · Ingia kujibu
    AHSANTE Muandishi. Kwaalivyo Shein sasa ndio tunaiona true colour yake kuwa ni mtu MNAFIK anasema asiyo yafanya.. anahubiri amani huku akitia watu jela!! anahubiri watu kusema Masheikh wasiseme!! anahubiri watu kuwa na uhuru wa kuchagua huku anashadidia sera za chama chake!! anakataa dini na kutanguliza CCM mbele !! hajuwi sisi ni waislamu dini kwanza kisha siasa.
    TUNAMUOMBA ALLAH KILA SIKU AMTENGEZENZE MTU HUYU AU AMUANGAMIZE ..(AMINN).




  4. Salali Mana 18/11/2012 kwa 10:40 mu · Ingia kujibu
    Ahsante Ndugu Hashil Seif Hashil kwa kumchambuwa kidogo rais wetu kipenzi, Dk Shein.Yeye aliwataka viongozi wa juu kukumbushana umuhimu wa kujikinga na fitna na kuziepuka taarifa za kubuni! kama tutakumbuka matatizo haya yote yameazia katika jimbo la (BuBuBu)hapo CCM walisema kwamba kabla ya kupelekwa Polisi wanachama wa CUF ni lazima kwanza wanachama wa CCM Vichwa vya Samaki, Mbwa Mwitu, Ubaya Ubaya, na hizo maskani za kachorora, Kisonge, walipewa amri na wakubwa kutoka Tanganyika (Napee), na Zanzibar(Borafya, Seif Idi ili wawashughulikie kwanza ndipo wawapeleke Polisi wale wanachama na wapenzi wa chama cha CUF.Hapo ndipo ikaanza pigapiga, chinjachinja, Uwa Uwa, na wanachama wengi wa CUF kufunguliwa kesi za kubuni, ziko hata picha ambazo askari wa Tanganyika jinsi walivyoshiriki mauwaji ya mwachama wa CUF, halafu mkuu wa Opereshen anasema yule alikuwa mla (UNGA)mwengine mtoto mdogo wa miaka (14)vilevile walimkamata na kumuuliza kwenu wapi akasema kwetu Pemba walimsulubu mpaka wakamuuwa.mbali na hawo waliopatwa na vilema vya maisha.kaset zipo na rais sio kama hayajuwi lakini anayafumbia macho kwani makamo wake wa kwanza kabla ya mambo hayajaharibika aliwasiliana naye kwa sim lakini hakuwa na mda wa kufuatilia matokeyo yake siku ya pili hali ilizidi kuwa mbaya zaid.Hapana taarifa za kubuniwa kama anavyo sema yeye Rais ni hawo viongozi wenzake wenye kutaka kumuharibiya ili baada ya miaka mitatu iwe ndio mwisho wa utawala wake halafu Tanganyika watuchaguliye rais mwingine kama kawaida yao.Hapo ndio atakuja kujuta majuto si mjukuu.Zanzibai kwanza vyama vya siasa, mwisho Tuachwe Tupumuwe.Wasiotaka kupumuwa (Zanzibar) waende Mrima.Tanganyikaaa……..




  5. makame silima 18/11/2012 kwa 11:48 mu · Ingia kujibu
    https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-uchindi-kwa-ukungu-wa-kiza.html#post5052333
    JK, kumbe CCM inategemea polisi ? Kujipatia uchindi kwa ukungu wa kiza.
    Amaliza muda wake kuwashia maaradhi kuyaendeleza.
    Muhariri
    Christopher Nyenyembe
    HIVI leo, Rais Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anapotamka hadharani kuwa CCM waache kutegemea polisi ana maanisha nini?
    Sijui anataka kuwaambia nini Watanzania wa leo kuwa jitihada kubwa za kukijenga chama hicho na nguvu kubwa inayotumiwa na vyombo vya dola wakati wa uchaguzi mkuu, rais alikuwa haoni.
    Sijui anatoa darasa gani kwa wana CCM wenzake kuwa waache tabia ya kuwategemea polisi katika harakati zao za kisiasa akisahau kuwa polisi ndio wanaotumika kuwasambaratisha wafuasi wa vyama vingine vya siasa vinapotekeleza majukumu yao ya kisiasa.
    Kauli ya Rais Kikwete kama ilivyonukuliwa na vyombo vya habari mjini Dodoma wiki hii alipokuwa akifunga mkutano mkuu wa nane wa CCM, moja ya kauli yake ilikuwa kukionya chama anachokiongoza kuwa kisiwategemee polisi katika masuala ya kisiasa, kwa kuwa kufanya hivyo CCM watakuwa wakijidanganya.
    Onyo hilo la rais kama mwenyekiti wa chama cha siasa anachokiongoza linatia shaka kwa kuwa naamini zuio hilo limetolewa muda ambao yeye binafsi anajua fika kuwa hagombei tena urais mwaka 2015.
    Alikuwa wapi kuwazuia polisi waliowapiga mabomu wananchi wa mkoa wa Arusha wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010, waliopigwa mabomu Mwanza, Mbeya, Morogoro, Singida na Dar es Salaam ili watu waogope kwenda kupiga kura.
    Siamini na sidhani kama agizo la mwenyekiti wa chama hicho, ambaye ni kiongozi mkuu wa chama hicho kikongwe cha siasa kuwa ndiyo dhamira ya kweli ya kukitaka chama hicho kiache kutegemea polisi katika masuala yao ya kisiasa.
    Sitaki kujirudisha kwenye maumivu makali ya kisiasa na namna polisi walivyoweza kutumika kuvuruga shughuli za kisiasa zinazoendelea kufanywa na vyama vya upinzani, hususan CHADEMA siku waliyofurumshwa na mabomu kule Nyololo, Mufindi, Mkoa wa Iringa.
    Polisi hao walifanya kazi ya kutuliza vurugu ambazo hazikuwepo na hatimaye kusababisha kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Channel Ten, marehemu Daudi Mwangosi, katika tukio hilo niliamini fika kuwa katika kukemea nguvu kubwa inayotumiwa na polisi katika masuala ya kisiasa, Rais Kikwete angetoa pole kwa familia ya marehemu lakini hakufanya hivyo.
    Nilisema na narudia kusema tena kuwa situmi ombi kwa rais kutaka kumwambia kuwa, watoto wa marehemu Mwangosi wanamlilia, na hata Mwangosi mwenyewe anamlilia anauliza Rais Kikwete uko wapi Mwangosi ninakulilia? Hayo yamepita, leo hii Mwenyekiti wa CCM anakionya chama chake eti kisitegemee polisi.
    Kwa maana hiyo na matukio kadhaa yanayotokea dhidi ya vyama vya upinzani ambapo polisi walioajiriwa na serikali inayoongozwa na CCM kuwa ni kweli wanatumwa na chama hicho ili kuvidhibiti vyama vingine vya siasa vinavyotishia uhai wa CCM.
    Iweje kama nguvu kubwa zimekuwa zikitumika kuvizima vyama pinzani ili kudhoofisha harakati zao za kujijenga, leo hii itawezekana vipi kama rais huyo huyo akiwa Mwenyekiti wa CCM taifa ameirudisha safu mpya iliyokuwa chini ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na kuwataka viongozi hao wasitegemee polisi.
    Yapo maswali ya kujiuliza kuwa enzi za kina Philip Mangula, Abdulrahaman Kinana, Seif Khatib na Mama Zakhia Meghji wakiwa kwenye safu ya Mkapa walikuwa hawategemei polisi ili kuendesha harakati zao za kisiasa na kama walikuwa wanategemea polisi wamerudishwa upya ili waache kutegemea polisi ?
    Nauliza nikiamini kuwa uzoefu wa CCM wa kutegemea polisi katika masuala yake ya kisiasa ulianza lini, ulianza kabla ya mfumo wa vyama vingi vya siasa au ulianza baada ya kuanzishwa kwa siasa za vyama vingi ndipo CCM walipogundua kuwa polisi ni mali yao.
    Na kama miaka yote CCM wanaamini kuwa polisi ni mali ya CCM na vyama vingine vya siasa havina polisi, kauli ya Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho aliyoitoa mkoani Dodoma ya kukionya chama chake kisitegemee polisi anataka kuwaambia nini Watanzania ambao bado wapo usingizini.
    Lakini ni vema ninukuu kwa undani kile alichokisema juu ya CCM na utegemezi wa nguvu za polisi, kuwa kitendo cha wana CCM kuishi katika siasa kwa kutegemea Jeshi la polisi hakipaswi kukubaliwa kwa kuwa kimepitwa na wakati.
    “Mnaishia kulalamika tu kila siku eti wanatukana halafu mnaishia kusema kawaida yao… au utasikia mtu anasema eti serikali haipo!Kazi ya serikali siyo hiyo, hiyo ni kazi ya kisiasa maana hao ndio wenzenu,” alisema Kikwete alipokuwa akifunga mkutano huo.
    “Sasa mnataka wakisema serikali ya CCM haijafanya kitu,polisi wawafuate, au wakisema Kikwete nchi imemshinda, polisi wawakamate ? Kama wakisema hatujafanya kitu, ni kazi yenu kusema kwamba tumefanya kitu, waonyesheni barabara, shule na mambo mengine.
    “Mkijibu kwa hoja wanatulia, siyo polisi. Nakumbuka Mwigulu aliwajibu pale bungeni kuhusu bajeti yao mbadala. Walipoitoa kijana wetu akasimama na kupigilia msumari kweli wakachanganyikiwa sasa hizo ndio kazi zinazotakiwa jamani,” alisisitiza Kikwete.
    Kama, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Kikwete ameamua kukiambia chama chake leo kuwa kisitegemee polisi, alikuwa wapi kukionya mara tu alipoteuliwa kwa mara ya kwanza kutoa kauli hiyo katika mkutano mkuu wa saba alipochukua mikoba iliyoachwa na rais mstaafu Benjamin Mkapa.
    Nini kimetokea ndani ya CCM na safu yake mpya inayoelekea kwenye vuguvugu la uchaguzi wa mwaka 2015 huku kukiwa na zuio kubwa la kukitaka chama hicho kiendeshe masuala yake ya kisiasa bila kutegemea polisi, wameona hasara gani ya kutumia polisi.
    Naamini kuwa mtaji mkubwa wa CCM katika medani ya kisiasa imekuwa ikielekezwa kwenye matumizi ya nguvu za vyombo vya dola siyo polisi pekee yao ambao CCM wanatakiwa waache kuvitumia, waache kabisa kutumia raslimali za nchi kwa lengo la kukijenga chama chao, waache ili serikali iwe salama.
    Kama CCM wanaambiwa hivyo leo, basi Rais Kikwete hakuona alipokuwa akihutubia mkutano huo jinsi watendaji wa serikali walivyokuwa wamejazana Dodoma wakiwa ndani ya ukumbi wa Kizota, huku ni wakuu wa wilaya na mikoa na upande wa pili ni wajumbe wa kamati za siasa za chama hicho.
    Watendaji wengi wa serikali wametumia kwa kiasi kikubwa raslimali za nchi na kulipwa masurufu kwa kazi za chama, mara baada ya mkutano huo kumalizika wamebaki Dodoma kwa kigezo cha kushiriki kwenye mrejesho wa semina elekezi kwa watendaji wa serikali hayo ndio maajabu ya CCM.
    Rais Kikwete anapaswa kusoma alama za nyakati kuwa Watanzania wa leo hawaamini moja kwa moja mawazo ya mtu mmoja ili kuweza kuijenga nchi yenye utawala bora bila kukiuka misingi madhubuti ya haki za binadamu.
    Kwa kuwa haki za binadamu zimekuwa zikikiukwa kwa misingi pengine ya kukibeba chama tawala ili kiendelee kushika dola hata kama wananchi wamechoka, rais alipaswa kuliagiza Jeshi la Polisi kuwa liache kuingilia masuala ya kisiasa na si kukiambia chama chake kuwa kisitegemee polisi, hilo si zuio ni agizo la kiutendaji kwa upande wa pili wa shilingi.
    Naamini kuwa ili nchi iweze kujielekeza kwenye ujenzi wa demokrasia ya kweli ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa, basi kila chama kinapaswa kuheshimu sheria za nchi na taratibu zote za kuendesha vyama vya siasa ili kuepuka vurugu.
    Jeshi la Polisi nao wafanye kazi zao kwa mujibu wa sheria ili chombo hicho kisitafsiriwe kuwa ni mali ya CCM na ili kuondoa dhana hiyo polisi wamesikia, kuwa CCM sasa haitawategemea tena.




  6. kitabukidogo 18/11/2012 kwa 11:48 mu · Ingia kujibu
    MUANDISHI HONGERA KWA UJUMBE MARIDHAWA , LAKINI INAFAA KUJIULIZA NI KWELI HUYU RAIS WETU YUPO HADHI INAKUWAJE ANAKUWA NA MANENO YA SIO KUA NA BUSARA KATIKA HOTUBA ZAKE KWA JINSI ANAVYO KURUPUKA INAONEKANA HANA WA KUMUANDALIA WA HAJIANDAI NI KITU GANI ANATAKA KUONGEA NA WANANCHI AMA ANAHISI WANANCHI NI WAPUMBAVU FULANI TU.
    KWA KAULI ZAKE ZA HIVI KARIBUNI NA JANA NDO KAZUA KUBWA LA KUSHANGAZA ATI HAKUNA MUUNGANO BORA DUNIANI KULIKO HUU MUUNGANO WETU. MIMI NAHISI WAJIBU WETU KUMTUMIA UJUMBE KAMA ALIVYOFANYA MUANDISHI LAKINI TUJIULIZE JEE UJUMBE UNAMFIKA ? NA KIMTAZAMO ANAESHAURIWA NDIEE? ISIJE IKAWA TUNAMPIGIA GITAA MBUZI ?
    MUUNGANO WETU NI BORA KULIKO MIUNGANO YOTE DUNIANI by Dr Ali Mohd Shein 17/11/2012




  7. Makame Ame 18/11/2012 kwa 12:29 um · Ingia kujibu
    Ahsante sana ndugu yetu Hashil Seif. Na sisi wengine tungependelea kuongeza waadhi huo kwa Mh Rais wetu Dr Shein.
    Tunamwona mara kwa mara pale msikitini kwa Boko akija kusali Ijumaa. Hili pamoja na ukweli kwamba anayo historia ya kutojifunga na magenge na kwamba ni hivi juzi tu amerudi kutekeleza nguzo ya Hija ina tupa imani kwamba mwenzetu anao moyo wa kumwogopa Muumba Wetu SWT.
    Hakuna aliyetimilia ila Yeye tu SWT na sote hupitia mitelezi ya kidunia. Na kwa hali hii ni wajibu wetu kukumbushana tukiona tunateleza au mwenzetu anaelekea kuliko siko (kubaya)
    Tafadhali rejea aya ya 93 ya Surati-Nnisaa:
    ومن يقتل مؤمنا متعمدا فجزاؤه جهنم خالدا فيها وغضب الله عليه ولعنه واعد له عذابا عظيما
    Whoso slayeth a believer of set purpose, his reward is hell for ever. Allah is wroth against him and He hath cursed him and prepared for him an awful doom
    Hii aya haina mchezo. INATISHA! Moto wa Jahannam si wa kumwombea mwenzio kuingia! Ghadhab za MwenyeziMngu hazichukuliki na Laana Yake si jambo la kuliomba!
    InshaaLlah hii aya isikuguse ndugu yetu. Lakini askari wako na vijana wa chama chako mbali ya kudhalilisha watu wasio na hatia wamefika pia kutoa roho za watu bila ya sababu zinazokubalika kidini (kisheria). Yachunguze vyema haya kwa kutumia ‘neutral’ sources. Wewe ukiwa kama ni jamadari wa vikosi hivyo unahisi au unafikiri huna mas’uuliya yoyote juu ya haya? Utakwenda kujibu nini Siku ya Siku. Umejitayarishaje kwa hili?
    Kwa hali na mambo yanavyokwenda haioneshi kwamba hili jambo umelichukulia hatua yoyote…ikiwa una uwezo huo. La huna, basi hatuna la kusema na pengine utaweza kujitetea mbele ya SWT. Kwetu ni kunasihiana.
    Tusighurike na sera za kidunia (kichama) ambazo asli yake ni ushetani. Fanya utafiti mzuri kwa vile wewe ni msomi utaliona hili. Na badala yake tutumie Mwongozo wa SWT, Sera za Mtume SAW, na akili zetu katika kutimiza majukumu yetu tuliyotwishwa au tuliojitwisha.
    Tunakunasih mwenzetu pamoja na nafsi zetu tujitahidi kufanya na kuamrishana mema, na kuepukana na kukatazana mabaya ili tupate radhi za MwenyeziMngu, tuweze kujenga mujtamaa wetu wa Wazanzibari (iitisaam) kwa hali ya kupendana ili dunia yetu na akhera yetu viwe vyenye manufaa nasi.




  8. Suleiman Bakar 18/11/2012 kwa 1:56 um · Ingia kujibu
    dah,, yan yanaihiataj kufikiriwa,, hasa kwa kukumbuka,, wako wapi walokua na nguvu na mamlaka makubwa leo hii?,, jibu hawapo,, lakini ndio wameishia tu hawapo au wapo lkn wamemelikiwa na yule mwenye mamlaka juu yao,, tafakari.




  9. Abdul 18/11/2012 kwa 2:14 um · Ingia kujibu
    mungu msambe sheni yeyena firauna wale wote wanao cheza sataili ya aina yake




  10. Bakar Faki 18/11/2012 kwa 3:30 um · Ingia kujibu
    Mtume (s.a.w) amesema " litakapo wekwa jambo kwa mtu asiyekua mwenyewe, basi subirini kiamatu" kwa maana hakuna litakalo kuwa.
    Wzanzibar tumeichukua serikali yetu ya umoja wa kitaifa tukamuachia mtu ambae hana uchungu na maridhiano, leo tunayaona hata wale waliotoa mchango mkubwa katika kuleta hayo maridhiano leo hawathamini.
    Lengo kuu la wananchi wa zanzibar kukubali maridhiano ni kuacha tofauti zao kuungana pamoja katika kutetea maslahi ya nchi yao. Je! sasa kama wale waliofanya jitihada kubwa katika kuleta haya maridhiano leo Dr. Shein anawatupa nje ya uongozi, kweli atkuwa anayathamini mariano au anayadharau?
    Kama tuliungana ili kupigania mamlaka ya nchi yetu, inapofika mahali wale wanaopaza sauti zao kuitetea zanzibar Dr. Shein anawasulubu, nani atasimama kututetea?
    Wazanzibari tukubali kwamba tulikosea kumkabidhi mamlaka ya serikali mtu ambae hakutoka jasho hata kidogo katika kuleta maridhiano zanzibar. Nina wasiwasi hata ile kura ya maoni sijui kama yeye alishiriki, na kama alishiriki basi itakuwa alipiga kura ya hapani, isingekuwa hivi anavyofanya. Lakini Mungu hafichi mnafiq tusubiri tutajuwatu, inshallah.




  11. mwanahalisi 18/11/2012 kwa 4:59 um · Ingia kujibu
    JAMANI HUYU DAKTARI SHEIN ALIKUWA MZIGO KULE SMT KWA VILE HAJUWI KUONGOZA NA NDIO AKAPELEKWA SUK ZANZIBAR NA KWA VILE YEYE ETI NI MPEMBA WAKIJUWA KUWA NA HUKU ATABORONGA TU KWA VILE HANA UWEZO UONGOZI SIO FANI YAKE,NA AKISHINDWA SI IONEKANE KWAMBA UNAONA MPEMBA HAWEZI KUONGOZA BWANA SI UMEONA,HIYO NDIYO MIPANGO YAO KWAMANTIKI HIYO ITAKUWA NI SABABU TOSHA KWAO HATA AWE NANI KWAKUWA NI MPEMBA BASI HAFAI KUONGOZA.NDIO MANA YEYE ANAKUWA REMOTED ALL THE TIME NAHISI AKIENDELEA HIVI ATASHINDWA TU.




  12. kijini 18/11/2012 kwa 5:33 um · Ingia kujibu
    kila rais anaye kuja anasifa zake aliye jiita komandoo alinadikuembea paa paa paa M/mungu kamtakabali nainshaall amuongezee karumbe alijitahidi kujikusanyia mmh wenyewa mnajuwa huyu SHUWAIN kaja na lake nayeye kututanulia puwa inshaall M/mungu nayeye amuongezee




  13. makame silima 18/11/2012 kwa 5:34 um · Ingia kujibu
    Katika watu waliokula Hasara Mmoja ni huyu Shein.
    Huyu jamaa juu ya kuwa nyeye mwenyewe hujita ni Mumuni wa dini ya kislamu lakini vile vile kasahau kuwa ni kiongozi wa nchi na watu anaowaongoza bila kujali mtu mwenye chama au asie na chama ,nijukumu na zimaa mbele ya Allah alio mumba na kumpa uwezo.
    Kiburi chake na makeke yake ya kujiona yeye ni yeye lakini anaonekana anavuka mipaka hivi sasa hata ya utu na ubinadamu wa kuwahurumia waislamu wa Zanzibar,Hivi sasa kiburi cha Uluwa kimezidi kwa uroho wa madaraka.
    Yupo tayari kuona waislamu wa Zanzibar (Masheikh wa Uamsho)wanaangamia Gerezani kwa propaganda za udini na ili wao waendelee kubaki madarakani huku mikono yao ikiwa inanuka harufu ya damu za waliowaangamiza kwa kauli zao.
    Wazanzibar katika mapambano ya kutafuta haki mambo mengi yanaweza yakasemwa kwa wale wanaoonekana kuwa ni tishio kwa utawala ulioko madarakani.
    Hivi sasa hatuna budi kutafuta mbinu yoyote ile ili kuwanusuru na kuwatetea ndugu zetu na Masheikh wetu ambao chini ya amri ya tunae mjuwa kuwa ni kiongozi wa nchi hii Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh Shein.
    Hivi sasa viongozi wetu wanaangamia na mateso vitendo vya ufezuli wanavyofanyiwa kama vile nchi hii % kubwa sio waslamu na wala hawana shembe ya ubinadamu.
    Hii leo inaonekana Mh Shein kafurutu mipaka na kuiongoza nchi hii kwa misingi ya ubaguzi na ubabe na kusahau kuwa yeye ni kiongozi wa wananchi wote wa Zanzibar walio mchaguwa na wasio mchaguwa, wenye vyama na wasio na vyama.
    Lakini Rais wetu kopoteza muelekeo huo yeye kawa ni Rais wa chama zaidi kuliko wa nchi na wananchi wake, sina haja ya kutowa mifano ,lakini mifano iko mingi tu yakuonyesha hivyo.
    Matokeo mengi tu na haya ya hivi karibuni mtoto wa miaka 14 kupigwa risasi na jeshi lake la Polisi na vitendo vyengine vya unyanyasaji wa watu wasio na hatia Rais kashindwa kutowa mkono wa pole kwa walengwa wote bali , rambirambi tuliziona ni kwa Kuliwa Koplo Said Abrahamani na kuvunjwa Maaskani za ccm Kisonge na Kachororo.
    Jee huyu kweli sio mbaguzi mwenye kuiongoza nchi kimatabaka ?
    Jee hawa wengine akiwemo huyu mtoto wa miaka 14 sio raia wake wenye kuhitaji haki na kuheshimiwa utu wake kama mzanzibar yoyote?
    Huyu Shein sie tayari tumetengezewa Balaa nyingine kuja kuendeleza maovu kwa jamii ya watu wa Zanzibar, lakini Ishaallah M/mungu tuko pamoja na wewe na hatuko pamoja na viongozi kama hawa wasio hata na chembe ya Ubinadamu.




  14. Rachid Abas 18/11/2012 kwa 7:53 um · Ingia kujibu
    Asante Hashil kwa barua yako hii kumkumbusha Dr, kama ni muungwana atakufahamu. Siku nyingine Hashil tuulize unapotaka kuandika kwa sisitulioko Zanzibar tuna mengi tunayofanyiwa na wahuni wa JESHI LA POLISI. Kila siku wahuni hao hutufata ucku wa saa 4 kutuvizia kutupiga ila ALLAH pekee ndie anaye tunusuru.




  15. Zakariya Nyange 19/11/2012 kwa 6:24 mu · Ingia kujibu
    asante kwa makala yako ambayo hakika ni nzuuri, ila m nina masuala ambayo hata sijui nimuulize nani na kwa sababu sijui upana wa mtandao huu ila nauliza 1.hizi habari ambazo zina andikwa humu kwenye blog zinawafikia walengwa kwa kiasi gani? 2.haya mawazo ni michanhgo ambayo yanatumika yanakuwa yanapewa kipaumbele au ni kutoa na hatimae siku kuiwa zinakwenda mbele? mwisho natoa mchango wangu: me nahisi ni bra kuwe hakuna uchanguzi ili watu wajiweke wenyewe kwenye madaraka kwa sababu mtu hujiona kama kajiweka mwenyewe hana habari ya wale ambao wamemchagua na kumuweka pale ni bora tuu tuachiwe na watu waongoze watakvyo tusihangaishane bure na LIENDE LENDAVYO KWANI SOTE C TUKO HUMU HUMU LIKIZAMA TUNAZAMA SOTE! KUUMIZA KICHWA KWA NN YAANI UJINGA TUU AH!

 
Back
Top Bottom