Uko Wapi Mkakati wa Viongozi wa CHADEMA Kama Chama Mbadala Katika Kushika Dola 2015?

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
Gazeti la Mwananchi la tarehe 12 November, 2012 lilimnukuu Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh Freeman Mbowe akisema, "Tumeanza mkakati wa kuhakikisha tunawafikia wananchi kila mahali. Tunataka kusikiliza matatizo yao, na hata pale ambako kuna shida ya usafiri, kwa pikipiki tutafika,” maelezo haya yanatoa picha kuwa, kwa sasa chama ndiyo kiko kwenye mchakato wa kuwafikia wananchi ili kuyajua matatizo yao. Maelezo haya yanapelekea kupatwa na wasiwasi juu ya mikakati ya chama kukabiliana na muda, misukosuko ya kiutendaji ili kujiandaa kushika dola na kukizi matakwa ya wananchi walio na kiu ya mabadiliko kutokana na kukosa kimbilio la uhakika baada ya CCM kuonekana kuwasahau au kuwatupa.

Inashangaza kuona pamoja na kuwa nchi imebakiwa na miaka miwili na nusu hivi kuingia kwenye uchaguzi mkuu, chama bado kiko kwenye mchakato wa kuyajua matatizo ya wananchi achilia mbali kujua safu ya uongozi wake itakayokipeleka kwenye chaguzi kuu.

CCM kwa sasa wanajipanga kuelekea uchaguzi mkuu baada ya kufanya chaguzi zao za ndani mapema ambazo zitawapa muda wa kujua wapi palipo na kikwazo ili kutafuta suruhisho mapema.

Historia inaonyesha kuwa chaguzi zozote na mara nyingi hasa katika vyama vyenye 'mashiko' (individual vested interest) huzaa makundi na inahitaji muda na hekima wa kuyakutanisha kwa ajiri ya mstakabali na ustawi wa chama. Ndiyo maana CCM wakaamua katika katiba yao kuwa na chaguzi mapema ili kutibu majeraha yatokanayo na makundi kabla ya chaguzi zake.


Dokezo za kisiasa zinaonyesha kuna uwezekano CHADEMA itakumbwa pia na hili 'gonjwa' la makundi hasimu katika chaguzi zake kwa sababu mpaka sasa hakibainisha hata utaratibu mbadala wa kuwapata watakao kuwa wagombea. Kama ubinafsi utatawala, basi kuna uwezekano wa chama kuelekea kwenye uchaguzi mkuu kikiwa bado na majeraha ambayo kwa kiwango kikubwa yatachangia kukidhoofisha. Ni wenye kuangalia mambo kwa jicho moja tu ambao watapingana na dokezo hili.

Maelezo ya Mwenyekiti yanajenga wingu la wasiwasi kiutendaji na ikumbukwe kuwa Oktoba 2015 kinadharia inaweza kuonekana ni mbali sana lakini ukiainisha muda na mikakati inayobainishwa na chama, inatoa sura ya wasiwasi kama kitaweza kuisukuma CCM nje ya madaraka ya nchi baada ya uchaguzi mkuu, Oktoba 2015.

Viongozi wa CHADEMA bado hawajajua kuwa mwaka 2015 kwa CHADEMA itakuwa ni 'do or die'.


Ninawasilisha...
 
Back
Top Bottom