MADAM T
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,210
- 2,389
Sijakuelewa ndugu yangu wazazi umewaingizaje hapo? kwani wao ndio waliotaka kuoana? wenyewe si walishapendana kabla na kuona wanafaa kuwa mume na mke sasa.. sherehe ya kukamilisha tu tena huwa mwishoni baada ya kutoka kanisani ndio iwe tatizo..!Mwanajamvi mwenzangu mimi nahisi matatizo ya ndoa huanzia kwenye maandalizi ya ndoa zenyewe... Vijana wanakuwa wamependana vizuri kwa jinsi walivo na wamelidhika kwa uwezo wao, ndoa wazee wanataka kuonesha wana uwezo kiasi gani, hivi ina maana gani mtu mwenye kipato kidogo cha chini kumfanyia harusi ya gharama si bora kama wazazi wana hela wawape watoto za kuanzia maisha..... Tutakapofika pale kila mtu atakapokuwa na uweza kujiamini na kuishi kwa kadiri ya uwezo wake ndoa zitadumu, sababu tatizo kubwa linalopelekea kuachana ni tamaa na instability ya kipato katika familia changa!! Watu wasipojitambua vikao vya usuluhishi vitakuwa vingi sana!!