Tuandamane
JF-Expert Member
- Feb 2, 2008
- 1,220
- 52
KAMPUNI ya Maji safi na Maji Taka mkoa wa Dar es Salaam (Dawasco) jana ilianza tena oparesheni maalum ya kukata maji kwa wadaiwa sugu 112, wakiwemo waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu.
Katika oparesheni hiyo maalum baadhi ya vigogo walioathirika ni Brigedia Jenerali mstaafu Hassan Ngwilizi ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ambaye ana deni la Sh1 milioni.
Katika katakata hiyo, kigogo mwingine aliyajikuta katika mikono ya Dawasco ni aliyewahi kushika nyadhifa za uwaziri kwenye Wizara kadhaa katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Edgar Maokola Majogo.
Katika orodha hiyo, Majogo ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati, Waziri wa Ulinzi na Naibu Waziri wa Ujenzi ananaiwa kiasi cha Sh4.7 milioni.
Kiongozi mwingine aliyewahi kushika wadhifa wa juu serikalini ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi kwa kipindi chote cha Awamu ya Tatu, Marten Lumbanga ambaye anadaiwa zaidi ya Sh3 milioni. Kwa sasa ni Balozi wa Tanzania kwenye Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Uswizi.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Afisa Uhusiano wa Dawasco, Badra Masoud alisema kuwa oparesheni hiyo ilianza jana katika maeneo ya Ada Estate, Masaki, Mikocheni, Regency Estate na Msasani.
Alisema wateja hao 112 ni wadaiwa sugu na wanadaiwa kiasi kikubwa cha fedha kutokana na kutolipa bili za Dawasco kwa vipindi virefu.
�Hii ni Oparesheni endelevu, leo tumaenza na hawa 112 lakini tutaendelea katika sehemu nyingine, tukianzia Manispaa ya Kinondoni,� alisema Badra.
Badra pia aliwataka wateja wao kuhakikisha kuwa wanakwenda kupilia huduma hiyo na kuacha risiti za malipo hayo kwenye makazi yao, ili kuepuka usumbufu wanaoweza kuupata kwa kutolipia madeni hayo.
Tangu kuanza kwa oparesheni hii mwanzoni mwa mwaka huu, Dawasco imekata majini katika maeneo muhimu ambayo yalikuwa wadaiwa sugu, ikiwemo kwenye kambi ya Jeshi la Wananchi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5634