Ukizitambua njia hizi sahihi za kupita utatimiza ndoto zako

Chu joe

New Member
Jul 15, 2021
3
45
Na Chu Joe

Habari za muda huu watanzania wenzangu natumaini nyote mko salama, leo napanda jukwaani nikieleza kwa uchache mambo unayotakiwa kuyafanya kijana ili uweze kutimiza ndoto zako au malengo yako iwe ni katika biashara, kazi, nasomo, nk.

1. Muombe Mungu na umshirikishe unachotaka kukifanya, kwa kiasi kikubwa binadamu tunamtegemea Mungu katika kila kitu kwenye maisha yetu, hivyo kama utahitaji kufanikiwa katika biashara, au masomo ni vyema ukimuomba Mungu aweze kukusaidia.

2. Fanya unachokipenda na unachokiweza, hii itakusaidia kulifanya jambo kwa ufasaha na ubora wa hali ya juu kwasababu utakachokuwa unakifanya utakuwa umejipima kama unakiweza na pia utakuwa unakipenda.

3. Zingatia ushauri wa watu lakini usibadili malengo, kitu kingine unachotakiwa kufanya ni kusikiliza ushauri unaopewa na watu, lakini hupaswi kubadili malengo kwasababu unachokifanya unakijua na unakuweza ndio maana ukaamua kukifanya.

4. Tenga muda wa kupigania unachotaka, tunafahamu ya kuwa ili ufanikiwe katika jambo lolote lile ni lazima utenge muda na uitoe akili yako katika kile unachokitafuta kwahiyo hilo ni jambo la kuzingatia pia.

5. Kuwa na nidhamu ya kazi, ili uweze kupata matokeo chanya katika jambo unalofanya unapaswa kuweka nidhamu mbele ili kila unachofanya uweze kukifanya kwa mpango maalumu kama kujali muda na kutunza kumbukumbu.

6. Usikubali kukata tamaa, katika kila jambo utakalolifanya lazima changamoto ziwepo hivyo basi ili ufanikiwe kutimiza ndoto yako unapaswa kukabiliana na matatizo yote yanayojitokeza bila kukata tamaa.

7. Punguza kufanya starehe, tunafahamu kuwa binadamu wengi tunapenda starehe na wakati mwingine tunafanya wakati hatuna hata uhakika wa kula kesho, kwahiyo ili ufanikiwe ni lazima upunguze au kuacha kabisa kufanya starehe kama kujirusha viwanja vya muziki, kutumua pombe kupita kiasi, nk.
 

mzushi flani

JF-Expert Member
Jan 20, 2020
1,630
2,000
maisha hayana kanuni! ndo maana wasio na mungu pia wanafanikiwa bila kumtanguliza kama ulivosema hapo juu!

kanuni zote zingine zinaingia kwenye "law of course and effect"

chochote unachokifanya kitaleta matokeo sambamba na ulichokifanya! isipotokea hivyo basi jua kuna sehemu ulikosea ndo maana hujapata matokeo stahiki! fanya kazi kwa bidii na bidiii yako italipa, fanya starehe kwa sana na majibu yake utayapata!

zingatia! bahati hutokea pale ambapo maandalizi yamekutana na fursa katika muda husika! huwezi kushinda biko kama hukucheza biko

mwisho nakwambia! acha u motivational speaker!

kwaheri!
 

Chu joe

New Member
Jul 15, 2021
3
45
Maisha hayana kanuni kweli lakini ukizingatia hayo mambo kwa kiasi chake utafika unapotaka ila sijakulazimisha kuamini wew simamia unachoamini na mimi hicho ndio nakiamin
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom