Ukizingatia Kanuni hizi, basi ufugaji wa kuku utakunyanyua kiuchumi

farmersdesk

Senior Member
May 26, 2012
164
120
@farmersdesk_tanzania
KABLA UJANZA KUFUGA KUKU TAMBUA MBEGU BORA YA KUFUGA🐓
MBEGU BORA YA KUKU
KABLA hujaanzisha mradi wa ufugaji kuku, ni lazima utafute aina ya mbegu bora itakayo kuongezea kipato.
Kumbuka kuna aina nyingi za kuku na ni aina zuri zote. Ila kila mfugaji huwa na malengo sasa hayo malengo yako ndio yatakayo kufanya utambue ni aina gani ya kuku unaetakiwa kumfuga ili utimize malengo yako.

Kumbuka kabla hujaanza kufuga kitu cha kwanza Fanya uchunguzi sehemu ulipo ni nini kina nunulika Zaidi.
Kwa mfano kama mayai yana soko Zaidi basi hapo unatakiwa ufuge kuku watakao kupatia mayai mengi KUROILER , na kama nyama ya kuku inanunulika Zaidi Basi hapo unatakiwa ufuge kuku wenye sifa ya kukuwa kwa haraka , wenye maumbo makubwa na nyama nyingi Ambapo Pia Kuroiler wataufaa zaidi.

Huo uchunguzi utakufanya wakati wa kuuza kuku au mayai usihangaike sana kuhusu soko.

SIFA ZA MBEGU BORA🌀

- Utoaji wa mayai kwa mwaka uwe mzuri
-Umbile la mwili na njisi aonekanavyo
-Uwezo wa kukua haraka
-Uwezo wa kuotesha manyoya haraka
-Uwezo Mkubwa mwilini wa kutengeneza chakula kuwa mayai au nyama
-Ulaji wa chakuka uwe mdogo ukilinganisha na uzalishaji wake
-Utagaji uwe wa muda mrefu kabla ya kupumzika
- Uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga wengi (Hii ni kwa kuku wa kienyeji)

FAIDA ZA MBEGU BORA🌀

Faida zipo nyingi hizi ni baadhi tu!!

👉Faida moja wapo ni kuwa mbegu bora ya kuku hukua kwa haraka , basi hiko kitendo cha kukuwa haraka kitakufanya wewe usitumie gharama nyingi kwenye kuwatunza; na hivyo utapata faida nyingi utakapo wauza

👉Faida ya pili ni wana muonekano mzuri kutokana na maumbo makubwa, hiyo itafanya wanunuzi kuvutiwa na kuku wako.

👉Kutokana na ukuwaji / utagaji bora itakuongezea kipato.
Ungana na familia ya wafugaji kupitia
 
Hongera sana hizi post ndo vijana tuzipendazo ili tuendelee kiuchumi


Kupitia uzi huu ntaacha kuwatapeli wanaume wa mikoani pale sokoni karume
Nitaanza kufuga kuku
 
Umesema kanuni hizi
Halafu umetaja moja Tu mbegu..
Ndo imeisha??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom