Ukizielewa Siasa za Tanzania huwezi kupata tabu. Hongera Rais Samia kwa kuzielewa vyema Siasa za Tanzania, nasema kazi iendelee

Haujiulizi kwanini uzi wako una comments ishirini tu ndani ya siku mbili? — ambazo kati ya hizo, za kwako tu ni zaidi ya kumi.

Niulize nikujuze.
Nyuzi za kijinga ndizo ambazo watu wanachangia sana kuliko zenye mambo ya msingi.sasa uzi kama huu umejitosheleza unataka watu wachangie nini zaidi ya kuusoma na kuelewa.Mambo yote yako wazi ila kama akili zako ni ndogo utataka kupinga.
 
Nyuzi za kijinga ndizo ambazo watu wanachangia sana kuliko zenye mambo ya msingi.sasa uzi kama huu umejitosheleza unataka watu wachangie nini zaidi ya kuusoma na kuelewa.Mambo yote yako wazi ila kama akili zako ni ndogo utataka kupinga.
Nyuzi zenye akili Kama hizi sio saizi yake yeye na mataga wenzake waliozoea kushikiwa akili na mwendazake
 
Amani iwe nanyi wadau,

Kama nilivyosema kwenye kichwa cha mada yangu hapo juu, Ukizielewa vyema Siasa za Tanzania , huwezi kupata tabu, na kwa siku chache alizokaa madarakani, napenda kusema Mama Samia amezielewa siasa za Tanzania vizuri sana, hivyo napenda kusema wazi, inawezekana kwenye maraisi 6 tuliokuwa nao Kama Tanzania hadi sasa, Samia Suluhu Hassan anaenda kuwa Rais aliyefanikiwa zaidi katika kuipaisha Tanzania kiuchumi, kuliko Marais wote tuliowai kuwa nao.

Kwanini nasema hivi?
Nasema hivi Kwa sababu , Siasa za Tanzania Kwa upande wote wa upinzani hadi Chama tawala, zimejaa chuki dhidi ya matajiri na utajiri, wivu dhidi ya matajiri na utajiri, fitna dhidi ya matajiri na utajiri na mwisho ni siasa ambazo zimejaa propaganda mfu dhidi ya maendeleo ya kweli kulikotokana na watu kuwa na mfumo wa akili unaowaza ujamaa zaidi kuliko ubepari jambo ambalo usipolijua vizuri unaweza kuishia kuwa Kiongozi anayefanya vibaya endapo usipoyajua haya na ukapata nafasi ya kuongoza Tanzania.

Ni kwanini nasema haya?
Tanzania Kama Taifa siku zote imekuwa inapambana na maadui kadhaa ikiwemo ukosefu wa ajira Kwa wananchi wake hasa vijana, umasikini, miondombinu mibaya, huduma mbovu za Afya, mipango miji mibovu na kutokuwepo kwa uwiano mzuri wa Maendeleo pamoja na nchi kukosa mitaji mikubwa na fedha katika kuwahudumia wananchi.

Kwa Matatizo haya makuu Kama Taifa ili kuweza kuyaondoa, tunaitaji 1. Uwekezaji Mkubwa wa Ndani na Nje utakaoleta kodi na ajira wa wananchi wetu( Hii ni Kwa sababu, serikali haiwezi kuajiri watu wote), Mazingira mazuri ya Biashara na uwekezaji ili watu wengi wa ndani na nje washiriki uchumi wetu na kujenga miondombinu, kuleta fedha za kigeni pamoja na teknolojia.

Kwa bahati mbaya sana, pamoja na ukweli kuwa Tanzania inahitaji hivi vitu kama nilivyosema hapo juu, Bado siasa za Tanzania zimegubikwa na chuki dhidi ya matajiri na utajiri, wivu dhidi ya matajiri na utajiri, fitna dhidi ya matajiri na utajiri na mwisho ni siasa ambazo zimejaa propaganda mfu dhidi ya maendeleo ya kweli kulikotokana na watu kuwa na mfumo wa akili unaowaza ujamaa zaidi kuliko ubepari

Mfano wa haya ni kama ifuatavyo!
1. Mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Ukienda Bagamoyo pale kuna sehemu ambayo imepangwa kujengwa Bandari na Viwanda Kwa ajiri way kutengeneza bidhaa, eneo hili tangu nchi upate uhuru halina uwekezaji wowote ule hadi sasa, ni mapori tu na wanyama wanazaliana pale. Huku China na Oman kupitia makampuni yao, wakisema wanataka kuja kujenga Bandari kubwa na ya mfano Kwa pembe hii ya Africa kwa pesa zao ambazo wala sio mkopo kwa Tanzania huku wakijenga Viwanda vitakavyotengeneza mamilioni ya ajira kwa watu wetu, na ikiwa ni Kweli Tanzania tuna Tatizo Pia la ajira linalofanya vijana wetu kugeuka wachuuzi

Bado watu kwa chuki zao tu dhidi ya maendeleo na utajiri wanapinga huu mradi Kwa sababu tele. Ukiwaambia wekeni mkataba wazi hawaweki Ila wanatoa sababu lukuki kama vile Tanzania tuna Bandari za maana sana zinazoweza kututoa vizuri kiuchumi. Bandari ya Bagamoyo ndo itakuwa geti kuu la kiuchumi kwa Africa Mashariki na itaifanya Tanzania kupata mapato mengi na kuwa na ajira nyingi za uhakika kwa watu wake. Ila watu kwa akili zao za kijamaa wanaipinga tu huku nchi ikizidi kuwa masikini na wananchi wanakosa ajira kila kukicha

2. Mradi wa Bomba la Gesi kwenda Kenya
Sasa kuna watu wanajitokeza eti wanadai tunawapa gesi kenya, wanasema haya kama vile iyo gesi Kenya atachukua tu bure wakati huo ni mradi mkubwa sana wa kiuchumi ambao utaliingizia taifa mamilioni ya fedha za kigeni zitakazotumika kufanya miradi mingi mikubwa kama ya ujenzi wa makazi bora kwa wananchi Mf Magomeni Kota. Hawajui fedha hizo za kigeni ndo zitajenga hospitali Bora na shule Bora kwa watoto wetu na kuwafanya wapate elimu Nzuri.

Wao Kwa sababu wana chuki tu na maendeleo ya kweli kazi yao ni kusema tu eti tutumie gesis kwa Viwanda vyetu isiende kenya. Hawajui ikienda kenya ina faida zaidi za kiuchumi?? Hawajui Urusi leo ni Taifa kubwa duniani na silaha yake kubwa inayomlinda kiuchumi ni gesi anayowauzia karibu mataifa yote ya Ulaya?

Mfano wa faida la Bomba la gesi unaonekana kwenye hili bomba litakalopita kutoka Uganda hadi Tanga ambapo Tanzania tutaingiza fedha nyingi za kigeni Kwa maendeleo ya Taifa letu na watu wetu.

3. Chuki dhidi ya Wawekezaji Wazawa (Rostam, Mo, Manji na wengineo)- Hapa Tanzania matajiri wanapigwa vita, wanakopa hela , kuwekeza mitaji yao Tanzania, kutengeneza ajira ila mtu akimuona Rostam tu utasikia huyu mwizi! Hawajui kuwa kodi kubwa za hawa watu ndo zinanunua madawa tunayotumia hospitali, ndo zinalipa mishahara ya watumishi ila wao kila siku ni kuwasema tu eti wezi, wanaliibia Taifa na wanajineemesha wao.

4. Mradi wa LNG Lindi
Sasa kuna watu wamejitokeza kupinga huu mradi, wanadai eti tunakurupuka kufanya huu mradi na miaka Sita ya majadiliano haitoshi tuongeze mingine. Wanadai tuzidi kujadiliana as if dunia itaendelea kutusubiri as if ajira zitaendelea kuwepo tu hata kama mradi utachelewa. Hawajui nchi inapoteza mapato kiasi gani ya kigeni kwa huu mradi kuchelewa, hawajui vijana wetu wanaumia kiasi gani kwa kukosa ajira kwa huu mradi kuchelewa. Hawajui kuwa kati ya miradi itakayoifanya nchi kuwa na uchumi mkubwa ikiwemo kuzidi nchi zote Africa ni huu mradi ila Kwa kutopenda kwao utajiri na kwa kuharibiwa na Sera za kijamaa wanaupinga.

Nimetoa mifano michache tu kuonesha ni jinsi gani Taifa letu limekuwa likirudishwa nyuma kutokana na siasa Za kimasikini na chuki dhidi ya matajiri na utajiri ambazo zimekuwa zikiturudisha nyuma badala ya kutupeleka mbele.

Ninachoshukuru Mungu ni kuwa Kwa tathmini yangu ndogo niliyoifanya, nimegundua kuwa Mama Samia Suluhu Hassan amezigundua hizi siasa za watanzania na amejipanga Kweli kuzipuuza kwa maendeleo ya kweli ya Tanzania. Anafanya vitu Kwa kuangalia maendeleo ya Tanzania ya kweli na sio kwa kusikiliza kelele za watu wenye fikra za ki masikini zisizolisaidia Taifa.

Hongera tena mama Samia. Umeanza vizuri sana.
Hivi Mwendazake alikuwa anatufokea kwa nini jamani? mbona mambo mengi hayajakaa sawa?
 
Back
Top Bottom