Ukizaa na mwenzio au wote ni wazazi usitengeneze mazingira ya chuki na uhasama mnapoachana

Ni mbaya saana...wengi wa watoto wanaokataliwa hupitia maisha magumu saana.

Imagine unaambiwa na mama baba yako alikukataa huku unaona marafiki zako wanachukuliwa na baba zao shule!!

Huyo mdada alifanya vizuri kurudi kwa mara pili kumwonyesha jamaa mtoto wake cha kusikitisha bado mwanaume hakuonyesha ushirikiano.

Unajua faida ya kurudi kwa mara ya pili??
Unaepuka kuwa mbinafsi. Kumbuka unaweza kugombana na mzazi mwenzako wewe binafsi lakini ni haki ya mtoto kumjua mama au baba yake. Hili huwa tunalisahau.

Wengi wanazilisha ego zao kwa kuwakomoa wazazi wenzao lakini literally anayekandamizwa ni mtoto...huu nauita ubinafsi.

Lingine..wanaume tunaokimbia watoto tunadhani wanawake wanahitaji vingiii. Wala sio wengi wenu kikubwa mnachohitaji hata kama hauhufumii asilimia 100 lakini unaonyesha kujali, upendo kwa mama na mtoto na kumweleza mwanamke tulichofanya hatukukosea...inatosha kabisa.

Umenifanya niandike saana.
ni kweli mkuu uwa ni kipindi kigumu sana kwa mama mtoto anakua bila baba na baba yupo hana time nae kuna muda mtu anahitaji ule upendo tu na ukaribu mwanae apate kutoka kwa baba au ndg wa baba sema wanaume wengi wanajua kukumbia kwao wanaepuka matumizi nshaptia hayo yanauma sana
 
Ni mbaya saana...wengi wa watoto wanaokataliwa hupitia maisha magumu saana.

Imagine unaambiwa na mama baba yako alikukataa huku unaona marafiki zako wanachukuliwa na baba zao shule!!

Huyo mdada alifanya vizuri kurudi kwa mara pili kumwonyesha jamaa mtoto wake cha kusikitisha bado mwanaume hakuonyesha ushirikiano.

Unajua faida ya kurudi kwa mara ya pili??
Unaepuka kuwa mbinafsi. Kumbuka unaweza kugombana na mzazi mwenzako wewe binafsi lakini ni haki ya mtoto kumjua mama au baba yake. Hili huwa tunalisahau.

Wengi wanazilisha ego zao kwa kuwakomoa wazazi wenzao lakini literally anayekandamizwa ni mtoto...huu nauita ubinafsi.

Lingine..wanaume tunaokimbia watoto tunadhani wanawake wanahitaji vingiii. Wala sio wengi wenu kikubwa mnachohitaji hata kama hauhufumii asilimia 100 lakini unaonyesha kujali, upendo kwa mama na mtoto na kumweleza mwanamke tulichofanya hatukukosea...inatosha kabisa.

Umenifanya niandike saana.


Nimekusoma barabara baba yeyoo, sasa umefuzu kuwa Laiboni hehehehhee
Hivi Laigunian na Laiboni kipi ni kikubwa kwa mwenzie..?

Hapo kwenye Laigunian najua nimechapia.... Nirekebishe tasavali baba yeyoo...

Ashenaaleek.
 
Nishauri tu kwamba kama wewe ni msichana umezaa na mwanaume ikatokea amekukwaza hakutaka kulea mtoto na mvulana umempa msichana ujauzito usimkimbie na usimfanye ajione kama alikosea kuwa na wewe maana ulipomtongoza na ukamuomba muwe wote mlikuwa mmependana hata kama ni kwa lisaa, mwanamke hawezi kumvulia mwanaume chupi kama hampendi au hajaamua. tuache habari za kubaka na mengine ya shinikizo kuwa utapata chochote ndio maana unaamua kumvulia chupi hapana, hiyo ni story nyingine.

Mwanaume ukimpa mdada ujauzito hata kama umejikuta huna uwezo wa kulea mimba na kumlea mtoto uwe muwazi kwake na umuonyeshe upendo tu inatosha kabisa, kadri siku zinavyokwenda ataelewa na kujua au kupata uhakika kweli huna hela Mwenyezi Mungu atafanya yake. Mdada anapokwambia ana ujauzito wako take it easy usimtukane, usimjibu vibaya, usimrushie maneno makali na ya hovyo, mchukulie kama vile dada yako kakutana na hilo au ndio kapata huo ujauzito na umuheshimu. ukisema alikuwa malaya ana wanaume wengi mimba sio yakwako unakuwa umekosea sana tu, si ungeacha kuingiza mdudu wako ndani au ungeacha kukojoa ndani, kama alikwambia yeye ni mjamzito au hajaona siku zake kwa mwezi huo basi muite mkae myazungumze. mbeleni huko tunakokwenda yani maishani kuna mengi mengine huyajui, kwa hiyo mpe heshima yake na umthamini hata kama ana sura mbaya au ni mbovu wa namna gani mpe heshima yake tu inatosha.

Mwanamke anapobaini kuwa ni mjamzito wewe mwanaume uwe na uvuilivu flan ambao utakuzuia kutorusha maneno, mwanaume akikataa sio yakwake na hata akikurushia maneno usipanik kwa kuanza kumjibu au kumtukana take it easy, haya maneno ya hovyo machafu na mabaya huwa tunakutana nayo huko mbeleni mwisho wa siku tunakutana na matatizo mengi yatokanayo na maneno mabaya tuliyo yatoa. Wengine huomba msaamaa yakisha wakuta wengine huvumilia na kuwatafuta wanaume wengine na kuwapa mzigo kuwa ni wakwao hadi mwanaume atakapo stuka yote haya ni kujisaidia ili upate sehem ya msaada hadi hapo utakapo jifungua.

Ninachotaka kushauri tu ni kitu kimoja
1. Mwanaume mtoto wa mwenzio ni kama wakwako au kama dada yako, tusiwatendee hao tunaweza tukatendewa kwa mabinti zetu pia au dada zetu, je tutafurahi au tutakuwa tayari kuyapokea kwa mikono miwili?

2. Kina dada tuache tabia ya kurusha maneno makali na machafu kwa wanaume tunapobaini kuna tatizo, si tunajua hatukufanya tafiti na kujiridhisha kuwa huyu mwanaume hafai, tunajua hilo hayo ni makosa basi tutafute namna pasiwepo na bifu au uhasama maana mwisho wake ni mbaya na ni mateso ambayo yanaweza yakakurudisha kule kule kwa huyo mwanaume.

3. Wanaume tuache kuwazalisha watoto wa watu, wanawake tumieni kinga mara zote hadi hapo mtakapo jiridhisha kuwa huyu anafaa kuzaa naye, maisha yasiwafanye mkawa chip hadi ukamuachia.

4. Lazima ifike mhala tuheshimiane, kama tumezaa mtoto tusiwape watoto sumu kuwa mama yako mbaya au baba yako mbaya hafai.

Kuna mdada nimezaa naye aliwahi kunambia siku nitadai mtoto wangu hakuna rangi nitaacha kuiona, mdada alikuwa mkali sana, hayo yalitokea tu ghafla maana sijaona nilipo mkosea nilimuandikia email nyingi za kuomba msamaha huenda kuna sehem nilikosea bado aliendelea kusema achana na mimi, kuna mwanaume alimwambia atamuoa na atamlea mtoto wangu basi akanikana. Hekima niliyoitumia nilikaa kimya sikumsemesha nilienda kumlipia mtoto ada ya sh Mil 1. laki 5 kwa mwaka, nikampa namba ya simu nikampa na mtoto hela ya kula huko shuleni, mama mtoto alivyosikia hivyo akawaambia waalimu wasiruhusu mtu yeyote kuja kumuona mtoto tena akachukua namba akatupa ili mtoto asiwasiliane na mm.

Niseme tu kwamba yule mwanaume alimuacha anabaki anazunguka na mtoto, jinsi ya kurudi kwangu imekuwa ngumu maana anajua matusi makubwa aliyoyatoa na kwa ndugu zangu hatukumjibu. amejipendekeza kukaa na wanaume zaidi ya 3 sasa wote anawaita ni malaya haoni wa kuishi naye na kila mwanaume amekaa naye kwa zaidi ya miezi 4 kama mke na mume, akitoka kwa huyu anahamia kwa huyu akijua huenda kuna unafuu kumbe hamna kitu, mwisho wa siku sasa hivi alirudi kwa kaka yake ndipo anapoishi sasa.

Bado ni mkimya nasubiri mwisho wake niuone maana maneno yake sijui nisemeje ila yanamtesa kwa sasa.

Lazima sote tujifunze hapa yeye ajifunze kwa upande wake na mimi nijifunze kwa upande wangu tujue nani kakosea na nani kafanya vizuri.

Hayo ndio maisha.
Hii ni elimu tosha, ila ushauri wangu kaa uzungumze naye atakua na mengi amejifunza ikiwezekana mpe nafasi tena anaweza aje kuwa mke bora sana kwako , dunia ni chuo ila kwa hawa viumbe wa kike huwa hawahitimu mpaka yawakute
 
Mwanaume kukataa mimba wakati ulikojolea ndani ni ufala.

Mwanamke kumsingizia mtu mimba ni upumbavu wa hali ya juu.

...........................................................................................


Usikatae mimba kataa mtoto.


Niliwahi kataa mtoto hivihivi na jamii ilinielewa. Sababu bila hata ya DNA yule hakuwa damu yangu.
Bahati nzuri nilifuma picha za baba halisi akiwa na huyo mtoto, copy & paste kabisa.

All in all haya mambo yanahitaji utumie akili sana usikurupuke kabisa.

Tutazingatia
 
MWANAMKE NIMEMWAMBIA TUKUTANE AFRICANA AKAKUBALI .NIKAFIKA MAPEMA KUMSUBURI AFRICANA. BADALA YAKE ANANITAKA NIMFUATE MLIMANI CITY. NIKAKATAA, NILIYAKOGA MATUSI MPAKA BASI. SIJUI KAROGWA HUYU? TANGIA HAPO NIMEFUNGA VIOO JE KOSA LANGU NI NINI?
 
Back
Top Bottom