Ukizaa na mwenzio au wote ni wazazi usitengeneze mazingira ya chuki na uhasama mnapoachana

Kuna madhara flan mpaka tuyafuatilie kwa karibu ndio tunayajua kwa mfano:
1. Baba aikatae Mimba yakwake kabisa halafu mdada aamue tu kuzaa maana baba hakutaka azae badae mtoto akizaliwa na akikua ebu fuatilieni mtaona kuna kitu kinacho mfuatilia huyo baba, kwa wenye experience watujuze hapa

2. Baba amkubali mtoto hadi mtoto anazaliwa ila kwa umri flan mdogo baba amkimbie mama na akatae kabisa hata kwa machozi ya kumlilia baba ampe hela ya matumizi mwanaume akatae fuatilieni kinacho mtokea baba huko mbeleni mtoto akiwa ameshakuwa na huku hajalelewa na baba.

3. Mdada amsingizie mwanaume kuwa ni mwanaye halafu mwanaume akubali huku mtoto akiwa sio wakwake utaona kinachoendelea tabia za mtoto huwa zinakuwa ni za kushangaza kwa baba anayesemwa ni mwanaye
Mimi kuna mdada alipata ujauzito akaniambia ni ujauzito wangu,nikamwambia sawa,ila mtu anapokuwa mjamzito anahitaji kuishi katika utaratibu mzuri,sasa yeye ukimpa hela anaenda kwenye pombe mpaka saa nane usiku,alafu kipindi hicho hicho anachodai ujauzito,alishatembea na rafiki yangu tena nikagundua live,baada ya siku kama tatu nikamkuta amekumbatiana na mpangaji mwenzake,jee mtu kama huyo anastahili kupewa matunzo ya hiyo mimba aliyoibeba au ni wakumpotezea tuu?
 
Uyo ana tatizo, kwanini aonekane akiwakumbatia wengine maana yake anagawa penzi, huyo ni wa kumsubiri ajifungue ili uwe na uhakika
 
Upo sahihi mkuu.

Kuna siku nilikutana na mdada kaunta ya juu...tukaanza stori mbili tano.

Tulifika mbali....akaanza kunisimulia stori zake na kunionyesha picha ya mwanae(kike). Lahaula anafanana na mtu ninayemjua. Nikaanza mbali mwenye mtoto ni mtu wa wawapi akasema Mtanzania anaitwa nani akataja...

Kumbe mtu wangu wa karibu....

Walikutana binti akiwa mdogo (19) binti akampenda saana jamaa....jamaa hakuwahi kujaribu kufanya makosa akawa anatumia mpira...huku binti akitamani kupata mtoto nae...

Siku ya siku wakapita peku..binti akapata ujauzito kuja kumweleza jamaa akawa mbogo...akapewa pesa za kuitoa.

Binti akaniambia aliifanyia hiyo mimba maandalizi ya kila kitu hakutoa ujauzito....toka kipindi hicho hawajakutana na nadhani jamaa anaamini mimba ilishatolewa au ameshasahau. Ila mtoto anafanana na watoto wake. Nilijizuia nisivushe tafrani kueleza mtoto yu hai.

Asante kwa uzi.....tusikatae watoto fikiria ungekataliwa wewe.

Kwanini lakini unerejesha kumbukumbu yangu nyuma........ Huyo mdada namfahamu....

Tuweke mada pembeni, nimekumiss.....

Live it.... Love it....
 
Nitokako hakuna aliyekataa mtoto....wanaume waliwalea ila usije ukadai chako wakishakua.

Na hata ukiingia ndani bomani utakuta ambaye siku mzaa anaurithi wa n'gombe wengi kuwazidi wenzake.

Mna utu sana huko mtokako, sio kwa kutokataa mtoto ajaye bomani bali ni upendo uliotukuka unaoongozwa na hekima.

Kila mtenda, hutendwa....

Kila mtendea, hutendewa...

Kuna Mangi mmoja alichemka miaka hiyoo akakataa kiiumbe chake kabla hata hakijazaliwa dada wa watu akameza fundo akaondoka hakurudi tena kwa yule Mangi, baada ya mtoto kuzaliwa dada alimtafuta Mangi akawambia muone mwanao. Mangi alifurahi maana mtoto alikuwa bandika bandua sura yake ila bado akaona sio akapotezea hakuonesha kutaka kulea mtoto.

Dada akaondoka mazimaa, sasa hivi huyo kaka anatusumbuaje sisi ndugu za huyo dada kuwa wazazi wake wanataka wamuone mjukuu sie tunamwambia muongee na mama mtoto mambo yenu hatuwezi ingilia sasa hivi.... Na wakati anaonesha rangi zake kwa ndugu yetu tuliona sema tukawa tunampa moyo sister na kumfariji.

Kaka yuko mpolee kimyaa ameufyata hadi anatia huruma ila ndo hivo hatuwezi kumsaidia alilikoroga mwenyewe.

K' Matata.
 
Huyo mtoto ana umri gani sasa hivi
 
Kuna watu wananifahamu humu, nikisema tuu umri wa mtoto watajua namzungumzia dada yupi.

Itoshe tuu kusimulia habari kama ilivyo, Ila mtoto ni mkubwa.
Mtoto anafanya kazi au bado anasoma
 
Mtoto anafanya kazi au bado anasoma

Weeh achaa, sisemi ng'oo.

Iache iwe fundisho kwa wanaume wepesi kukataa mimba, bado akaoneshwa mtoto baadae ya kuzaliwa kafanana copyright bado akambwela mbwela hajielewi...... Sister Wala jana habari nae baba mtoto, hata akiwa jana hela hajigusi kuomba msaada kwa baba mtoto.

Na anafahamu iko siku mtoto atamtafuta tuu baba yake, hilo hana shida nalo.
 
Je atakuwa tayari kumuonyesha mtoto baba yake alipo maana wengine wagumu hawataki kabisa
 
Sijui kwa hilo maana sifahamu ya moyoni mwake ila nafahamu alishatuambia, huyu mtoto najua iko siku atamtafuta tuu baba yake amesema hatamzuia.

Mtu chake...

Sister hakuwa na kinyongo tangu mwanzo sema baba mtoto tuu kujiforogoa kumbe ligi haliwezi...
 
Mimi kuna mdada alipata ujauzito akaniambia ni ujauzito wangu,nikamwambia sawa,ila mtu anapokuwa mjamzito anahitaji kuishi katika utaratibu mzuri,sasa yeye ukimpa hela anaenda kwenye pombe mpaka saa nane usiku,alafu kipindi hicho hicho anachodai ujauzito,alishatembea na rafiki yangu tena nikagundua live,baada ya siku kama tatu nikamkuta amekumbatiana na mpangaji mwenzake,jee mtu kama huyo anastahili kupewa matunzo ya hiyo mimba aliyoibeba au ni wakumpotezea tuu?
Hapo mkuu umetimiza wajibu wako na umenawa mikono kuwa yy kaharibu na kuna siku atapolomosha matusi tu!
 
Kwanini lakini unerejesha kumbukumbu yangu nyuma........ Huyo mdada namfahamu....

Tuweke mada pembeni, nimekumiss.....

Live it.... Love it....
Miss you pia matata.

Tehtehteh...umeanza utata!!!
 
Mna utu sana huko mtokako, sio kwa kutokataa mtoto ajaye bomani bali ni upendo uliotukuka unaoongozwa na hekima.

Kila mtenda, hutendwa....

Kila mtendea, hutendewa...

Kuna Mangi mmoja alichemka miaka hiyoo akakataa kiiumbe chake kabla hata hakijazaliwa dada wa watu akameza fundo akaondoka hakurudi tena kwa yule Mangi, baada ya mtoto kuzaliwa dada alimtafuta Mangi akawambia muone mwanao. Mangi alifurahi maana mtoto alikuwa bandika bandua sura yake ila bado akaona sio akapotezea hakuonesha kutaka kulea mtoto.

Dada akaondoka mazimaa, sasa hivi huyo kaka anatusumbuaje sisi ndugu za huyo dada kuwa wazazi wake wanataka wamuone mjukuu sie tunamwambia muongee na mama mtoto mambo yenu hatuwezi ingilia sasa hivi.... Na wakati anaonesha rangi zake kwa ndugu yetu tuliona sema tukawa tunampa moyo sister na kumfariji.

Kaka yuko mpolee kimyaa ameufyata hadi anatia huruma ila ndo hivo hatuwezi kumsaidia alilikoroga mwenyewe.

K' Matata.
Ni mbaya saana...wengi wa watoto wanaokataliwa hupitia maisha magumu saana.

Imagine unaambiwa na mama baba yako alikukataa huku unaona marafiki zako wanachukuliwa na baba zao shule!!

Huyo mdada alifanya vizuri kurudi kwa mara pili kumwonyesha jamaa mtoto wake cha kusikitisha bado mwanaume hakuonyesha ushirikiano.

Unajua faida ya kurudi kwa mara ya pili??
Unaepuka kuwa mbinafsi. Kumbuka unaweza kugombana na mzazi mwenzako wewe binafsi lakini ni haki ya mtoto kumjua mama au baba yake. Hili huwa tunalisahau.

Wengi wanazilisha ego zao kwa kuwakomoa wazazi wenzao lakini literally anayekandamizwa ni mtoto...huu nauita ubinafsi.

Lingine..wanaume tunaokimbia watoto tunadhani wanawake wanahitaji vingiii. Wala sio wengi wenu kikubwa mnachohitaji hata kama hauhufumii asilimia 100 lakini unaonyesha kujali, upendo kwa mama na mtoto na kumweleza mwanamke tulichofanya hatukukosea...inatosha kabisa.

Umenifanya niandike saana.
 
Sio kufanyiwa swala ni kumhurumia yeye kwa alichokifanya maana sasa kinamtesa na kwangu hawezi tena kunambia lolote nikamuelewa, iyo ni miaka ya nyuma kidogo imekuwa ni fundisho kwangu kuwa kukaa kimya kunasaidia zaidi ya kurushiana maneno
mtoto ana umri gani mkuu?nmejikuta namuonea huruma sana dogo
 
Back
Top Bottom