Mchajikobez
JF-Expert Member
- May 25, 2018
- 371
- 536
Mimi kuna mdada alipata ujauzito akaniambia ni ujauzito wangu,nikamwambia sawa,ila mtu anapokuwa mjamzito anahitaji kuishi katika utaratibu mzuri,sasa yeye ukimpa hela anaenda kwenye pombe mpaka saa nane usiku,alafu kipindi hicho hicho anachodai ujauzito,alishatembea na rafiki yangu tena nikagundua live,baada ya siku kama tatu nikamkuta amekumbatiana na mpangaji mwenzake,jee mtu kama huyo anastahili kupewa matunzo ya hiyo mimba aliyoibeba au ni wakumpotezea tuu?Kuna madhara flan mpaka tuyafuatilie kwa karibu ndio tunayajua kwa mfano:
1. Baba aikatae Mimba yakwake kabisa halafu mdada aamue tu kuzaa maana baba hakutaka azae badae mtoto akizaliwa na akikua ebu fuatilieni mtaona kuna kitu kinacho mfuatilia huyo baba, kwa wenye experience watujuze hapa
2. Baba amkubali mtoto hadi mtoto anazaliwa ila kwa umri flan mdogo baba amkimbie mama na akatae kabisa hata kwa machozi ya kumlilia baba ampe hela ya matumizi mwanaume akatae fuatilieni kinacho mtokea baba huko mbeleni mtoto akiwa ameshakuwa na huku hajalelewa na baba.
3. Mdada amsingizie mwanaume kuwa ni mwanaye halafu mwanaume akubali huku mtoto akiwa sio wakwake utaona kinachoendelea tabia za mtoto huwa zinakuwa ni za kushangaza kwa baba anayesemwa ni mwanaye