Ukizaa na mwenzio au wote ni wazazi usitengeneze mazingira ya chuki na uhasama mnapoachana

M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Messages
2,644
Points
2,000
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined Sep 12, 2017
2,644 2,000
Nishauri tu kwamba kama wewe ni msichana umezaa na mwanaume ikatokea amekukwaza hakutaka kulea mtoto na mvulana umempa msichana ujauzito usimkimbie na usimfanye ajione kama alikosea kuwa na wewe maana ulipomtongoza na ukamuomba muwe wote mlikuwa mmependana hata kama ni kwa lisaa, mwanamke hawezi kumvulia mwanaume chupi kama hampendi au hajaamua. tuache habari za kubaka na mengine ya shinikizo kuwa utapata chochote ndio maana unaamua kumvulia chupi hapana, hiyo ni story nyingine.

Mwanaume ukimpa mdada ujauzito hata kama umejikuta huna uwezo wa kulea mimba na kumlea mtoto uwe muwazi kwake na umuonyeshe upendo tu inatosha kabisa, kadri siku zinavyokwenda ataelewa na kujua au kupata uhakika kweli huna hela Mwenyezi Mungu atafanya yake. Mdada anapokwambia ana ujauzito wako take it easy usimtukane, usimjibu vibaya, usimrushie maneno makali na ya hovyo, mchukulie kama vile dada yako kakutana na hilo au ndio kapata huo ujauzito na umuheshimu. ukisema alikuwa malaya ana wanaume wengi mimba sio yakwako unakuwa umekosea sana tu, si ungeacha kuingiza mdudu wako ndani au ungeacha kukojoa ndani, kama alikwambia yeye ni mjamzito au hajaona siku zake kwa mwezi huo basi muite mkae myazungumze. mbeleni huko tunakokwenda yani maishani kuna mengi mengine huyajui, kwa hiyo mpe heshima yake na umthamini hata kama ana sura mbaya au ni mbovu wa namna gani mpe heshima yake tu inatosha.

Mwanamke anapobaini kuwa ni mjamzito wewe mwanaume uwe na uvuilivu flan ambao utakuzuia kutorusha maneno, mwanaume akikataa sio yakwake na hata akikurushia maneno usipanik kwa kuanza kumjibu au kumtukana take it easy, haya maneno ya hovyo machafu na mabaya huwa tunakutana nayo huko mbeleni mwisho wa siku tunakutana na matatizo mengi yatokanayo na maneno mabaya tuliyo yatoa. Wengine huomba msaamaa yakisha wakuta wengine huvumilia na kuwatafuta wanaume wengine na kuwapa mzigo kuwa ni wakwao hadi mwanaume atakapo stuka yote haya ni kujisaidia ili upate sehem ya msaada hadi hapo utakapo jifungua.

Ninachotaka kushauri tu ni kitu kimoja
1. Mwanaume mtoto wa mwenzio ni kama wakwako au kama dada yako, tusiwatendee hao tunaweza tukatendewa kwa mabinti zetu pia au dada zetu, je tutafurahi au tutakuwa tayari kuyapokea kwa mikono miwili?

2. Kina dada tuache tabia ya kurusha maneno makali na machafu kwa wanaume tunapobaini kuna tatizo, si tunajua hatukufanya tafiti na kujiridhisha kuwa huyu mwanaume hafai, tunajua hilo hayo ni makosa basi tutafute namna pasiwepo na bifu au uhasama maana mwisho wake ni mbaya na ni mateso ambayo yanaweza yakakurudisha kule kule kwa huyo mwanaume.

3. Wanaume tuache kuwazalisha watoto wa watu, wanawake tumieni kinga mara zote hadi hapo mtakapo jiridhisha kuwa huyu anafaa kuzaa naye, maisha yasiwafanye mkawa chip hadi ukamuachia.

4. Lazima ifike mhala tuheshimiane, kama tumezaa mtoto tusiwape watoto sumu kuwa mama yako mbaya au baba yako mbaya hafai.

Kuna mdada nimezaa naye aliwahi kunambia siku nitadai mtoto wangu hakuna rangi nitaacha kuiona, mdada alikuwa mkali sana, hayo yalitokea tu ghafla maana sijaona nilipo mkosea nilimuandikia email nyingi za kuomba msamaha huenda kuna sehem nilikosea bado aliendelea kusema achana na mimi, kuna mwanaume alimwambia atamuoa na atamlea mtoto wangu basi akanikana. Hekima niliyoitumia nilikaa kimya sikumsemesha nilienda kumlipia mtoto ada ya sh Mil 1. laki 5 kwa mwaka, nikampa namba ya simu nikampa na mtoto hela ya kula huko shuleni, mama mtoto alivyosikia hivyo akawaambia waalimu wasiruhusu mtu yeyote kuja kumuona mtoto tena akachukua namba akatupa ili mtoto asiwasiliane na mm.

Niseme tu kwamba yule mwanaume alimuacha anabaki anazunguka na mtoto, jinsi ya kurudi kwangu imekuwa ngumu maana anajua matusi makubwa aliyoyatoa na kwa ndugu zangu hatukumjibu. amejipendekeza kukaa na wanaume zaidi ya 3 sasa wote anawaita ni malaya haoni wa kuishi naye na kila mwanaume amekaa naye kwa zaidi ya miezi 4 kama mke na mume, akitoka kwa huyu anahamia kwa huyu akijua huenda kuna unafuu kumbe hamna kitu, mwisho wa siku sasa hivi alirudi kwa kaka yake ndipo anapoishi sasa.

Bado ni mkimya nasubiri mwisho wake niuone maana maneno yake sijui nisemeje ila yanamtesa kwa sasa.

Lazima sote tujifunze hapa yeye ajifunze kwa upande wake na mimi nijifunze kwa upande wangu tujue nani kakosea na nani kafanya vizuri.

Hayo ndio maisha.
 
Jeceel

Jeceel

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2018
Messages
538
Points
1,000
Jeceel

Jeceel

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2018
538 1,000
Watz wengi ni mabingwa wa kuwabamibikizia watu mimba sio zao
 
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
30,127
Points
2,000
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
30,127 2,000
Pole sana...

Kumbe maneno mengi hivi ni sababu unauchungu wa uliyofanyiwa na mwanamke wako...Cc: mahondaw
 
Daby

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Messages
30,189
Points
2,000
Daby

Daby

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2014
30,189 2,000
Upo sahihi mkuu.

Kuna siku nilikutana na mdada kaunta ya juu...tukaanza stori mbili tano.

Tulifika mbali....akaanza kunisimulia stori zake na kunionyesha picha ya mwanae(kike). Lahaula anafanana na mtu ninayemjua. Nikaanza mbali mwenye mtoto ni mtu wa wawapi akasema Mtanzania anaitwa nani akataja...

Kumbe mtu wangu wa karibu....

Walikutana binti akiwa mdogo (19) binti akampenda saana jamaa....jamaa hakuwahi kujaribu kufanya makosa akawa anatumia mpira...huku binti akitamani kupata mtoto nae...

Siku ya siku wakapita peku..binti akapata ujauzito kuja kumweleza jamaa akawa mbogo...akapewa pesa za kuitoa.

Binti akaniambia aliifanyia hiyo mimba maandalizi ya kila kitu hakutoa ujauzito....toka kipindi hicho hawajakutana na nadhani jamaa anaamini mimba ilishatolewa au ameshasahau. Ila mtoto anafanana na watoto wake. Nilijizuia nisivushe tafrani kueleza mtoto yu hai.

Asante kwa uzi.....tusikatae watoto fikiria ungekataliwa wewe.
 
Daby

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Messages
30,189
Points
2,000
Daby

Daby

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2014
30,189 2,000
Watz wengi ni mabingwa wa kuwabamibikizia watu mimba sio zao
Nitokako hakuna aliyekataa mtoto....wanaume waliwalea ila usije ukadai chako wakishakua.

Na hata ukiingia ndani bomani utakuta ambaye siku mzaa anaurithi wa n'gombe wengi kuwazidi wenzake.
 
Cole Williams

Cole Williams

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2016
Messages
31,697
Points
2,000
Cole Williams

Cole Williams

JF-Expert Member
Joined Jun 1, 2016
31,697 2,000
Upo sahihi mkuu.

Kuna siku nilikutana na mdada kaunta ya juu...tukaanza stori mbili tano.

Tulifika mbali....akaanza kunisimulia stori zake na kunionyesha picha ya mwanae(kike). Lahaula anafanana na mtu ninayemjua. Nikaanza mbali mwenye mtoto ni mtu wa wawapi akasema Mtanzania anaitwa nani akataja...

Kumbe mtu wangu wa karibu....

Walikutana binti akiwa mdogo (19) binti akampenda saana jamaa....jamaa hakuwahi kujaribu kufanya makosa akawa anatumia mpira...huku binti akitamani kupata mtoto nae...

Siku ya siku wakapita peku..binti akapata ujauzito kuja kumweleza jamaa akawa mbogo...akapewa pesa za kuitoa.

Binti akaniambia aliifanyia hiyo mimba maandalizi ya kila kitu hakutoa ujauzito....toka kipindi hicho hawajakutana na nadhani jamaa anaamini mimba ilishatolewa au ameshasahau. Ila mtoto anafanana na watoto wake. Nilijizuia nisivushe tafrani kueleza mtoto yu hai.

Asante kwa uzi.....tusikatae watoto fikiria ungekataliwa wewe.
Kila ulichoandika ni sawa Mkuu, lakini nani wa kusacrifice na anakutana na situation gani wakati anatakiwa akubali jukumu lake

TATIZO MFUMO MKUU
 
Daby

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Messages
30,189
Points
2,000
Daby

Daby

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2014
30,189 2,000
Kila ulichoandika ni sawa Mkuu, lakini nani wa kusacrifice na anakutana na situation gani wakati anatakiwa akubali jukumu lake

TATIZO MFUMO MKUU
Sijaweza kukupata vizuri mkuu...nidadavulie
 
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Messages
2,644
Points
2,000
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined Sep 12, 2017
2,644 2,000
Watz wengi ni mabingwa wa kuwabamibikizia watu mimba sio zao
Tarehe yakwake ya danger si utaijua na siku ulilala naye si utaijua hospitali si watapima wakwambie ina muda gani ikishindikana basi mtoto azaliwe tuone kiungo kipi cha kwako atakuwa nacho
 
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Messages
2,644
Points
2,000
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined Sep 12, 2017
2,644 2,000
Pole sana...

Kumbe maneno mengi hivi ni sababu unauchungu wa uliyofanyiwa na mwanamke wako...Cc: mahondaw
Sio kufanyiwa swala ni kumhurumia yeye kwa alichokifanya maana sasa kinamtesa na kwangu hawezi tena kunambia lolote nikamuelewa, iyo ni miaka ya nyuma kidogo imekuwa ni fundisho kwangu kuwa kukaa kimya kunasaidia zaidi ya kurushiana maneno
 
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Messages
2,644
Points
2,000
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined Sep 12, 2017
2,644 2,000
Upo sahihi mkuu.

Kuna siku nilikutana na mdada kaunta ya juu...tukaanza stori mbili tano.

Tulifika mbali....akaanza kunisimulia stori zake na kunionyesha picha ya mwanae(kike). Lahaula anafanana na mtu ninayemjua. Nikaanza mbali mwenye mtoto ni mtu wa wawapi akasema Mtanzania anaitwa nani akataja...

Kumbe mtu wangu wa karibu....

Walikutana binti akiwa mdogo (19) binti akampenda saana jamaa....jamaa hakuwahi kujaribu kufanya makosa akawa anatumia mpira...huku binti akitamani kupata mtoto nae...

Siku ya siku wakapita peku..binti akapata ujauzito kuja kumweleza jamaa akawa mbogo...akapewa pesa za kuitoa.

Binti akaniambia aliifanyia hiyo mimba maandalizi ya kila kitu hakutoa ujauzito....toka kipindi hicho hawajakutana na nadhani jamaa anaamini mimba ilishatolewa au ameshasahau. Ila mtoto anafanana na watoto wake. Nilijizuia nisivushe tafrani kueleza mtoto yu hai.

Asante kwa uzi.....tusikatae watoto fikiria ungekataliwa wewe.
Jaribu kufuatilia wanaume wengi wanao wakataa watoto wanao zaliwa huwa wanakutana na mambo flani hivi ambayo sijui huwa ni hasira ya yule mtoto kukataliwa au ni nini, fuatilia kwanza kuwaangalia watoto walio kataliwa na moja wa wazazi wao kuwa wasizaliwe au walizaliwa badae baba zao wakawakimbia fuatilia utatupa mrejesho kinachowakuta hao wanaume
 
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Messages
2,644
Points
2,000
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined Sep 12, 2017
2,644 2,000
Kuna madhara flan mpaka tuyafuatilie kwa karibu ndio tunayajua kwa mfano:
1. Baba aikatae Mimba yakwake kabisa halafu mdada aamue tu kuzaa maana baba hakutaka azae badae mtoto akizaliwa na akikua ebu fuatilieni mtaona kuna kitu kinacho mfuatilia huyo baba, kwa wenye experience watujuze hapa

2. Baba amkubali mtoto hadi mtoto anazaliwa ila kwa umri flan mdogo baba amkimbie mama na akatae kabisa hata kwa machozi ya kumlilia baba ampe hela ya matumizi mwanaume akatae fuatilieni kinacho mtokea baba huko mbeleni mtoto akiwa ameshakuwa na huku hajalelewa na baba.

3. Mdada amsingizie mwanaume kuwa ni mwanaye halafu mwanaume akubali huku mtoto akiwa sio wakwake utaona kinachoendelea tabia za mtoto huwa zinakuwa ni za kushangaza kwa baba anayesemwa ni mwanaye
 
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Messages
2,644
Points
2,000
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined Sep 12, 2017
2,644 2,000
Kila ulichoandika ni sawa Mkuu, lakini nani wa kusacrifice na anakutana na situation gani wakati anatakiwa akubali jukumu lake

TATIZO MFUMO MKUU
Mwanaume muulize mdada vizuri akanushe kama mtoto ni wako then mvumilie ajifungue tu basi utapata jibu na utachukua hatua
 
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Messages
2,644
Points
2,000
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined Sep 12, 2017
2,644 2,000
Kina dada wawe wakweli kuwataja waume sahihi waliowapa ujauzito hata kama hawana uwezo ni baraka na kulinda heshima zao
 
Kingsmann

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Messages
1,167
Points
2,000
Kingsmann

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2018
1,167 2,000
Mwanaume kukataa mimba wakati ulikojolea ndani ni ufala.

Mwanamke kumsingizia mtu mimba ni upumbavu wa hali ya juu.

...........................................................................................

Usikatae mimba kataa mtoto.

Niliwahi kataa mtoto hivihivi na jamii ilinielewa. Sababu bila hata ya DNA yule hakuwa damu yangu.
Bahati nzuri nilifuma picha za baba halisi akiwa na huyo mtoto, copy & paste kabisa.

All in all haya mambo yanahitaji utumie akili sana usikurupuke kabisa.
 
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Messages
2,644
Points
2,000
M

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined Sep 12, 2017
2,644 2,000
All in all haya mambo yanahitaji utumie akili sana usikurupuke kabisa.
watu wanakurupuka kuanza kurushiana maneno makali na matusi mwisho wa siku mtoto ni wake
 
Forum statistics

Threads 1,326,612
Members 509,543
Posts 32,228,388
Top