Ukiweza kutofautisha haya basi umekomaa, njia kwako ni nyeupe

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,864
UKIWEZA TOFAUTISHA HAYA BASI UMEKOMAA NA UTAKUWA UMEFANIKIWA

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

1. UHAI Vs Uzima

Uhai independent Variable
Uzima ni dependent Variable
Unaweza ukawa hai lakini usiwe Mzima
Lakini huwezi kuwa Mzima bila uhai.

Uhai unahusu kuishi kwa ujumla, uzima ni mahususi kwa kuwa na afya njema.

2. PUMZI Vs HEWA

Pumzi ni Nishati ya kumfanya kiumbe awe Hai
Hewa ni Maada ya mkusanyiko wa gesi. Itembeapo huzalisha upepo.
Pumzi huhusishwa na gesi ya Oksijen, ni kusema nishati ya uhai iitwayo pumzi imehifadhiwa kwenye gesi ya Oksijeni

3. AKILI Vs ELIMU
Akili hukupa uhai
Elimu hukupa uzima
Yaani Akili ndio inakufanya uishi wakati elimu inakufanya uishi kwa namna ipi(nzuri)
Akili haina mipaka, elimu ina mipaka, ni mahususi.

4. UZURI Vs UREMBO

Uzuri upo akilini mwa mtu, huanzia ndani kwenda nje, na kamwe uzuri hauwezi anzia nje kwenda ndani..
Urembo upo mwilini, upo nje, hauwezi ingia ndani bali upo nje siku zote.
Uzuri upo siku zote, urembo unabadilika badilika kulingana na wakati na mazingira.

5. WEMA Vs MSAADA
Wema hauna malipo
Msaada una malipo huitwa Hisani/Fadhila.
Wema wenye malipo huitwa Msaada. Hii ni kusema wema unaweza kuwa msaada, ila msaada hauwezi kuwa wema.

Wema hauumi
Msaada unauma hasa pale usipolipwa Hisani.
Ukiona ulitenda jambo fulani kwa mtu alafu ukaumia kisa hakurudisha hisani iwe ya kukwambia Ahsante, jua wewe ni mtoa msaada, huna wema.

Yesu alisema hakuna aliyemwema isipokuwa MUNGU, hata hivyo hatujakatazwa kujitahidi kuwa wema. Ndio maana Vitabu vya dini vinatusihi tujitahidi kuwa wema.

6. GIZA Vs USIKU

Giza lipo akilini/fikarani
Usiku Upo machoni.
Panaweza kuwa usiku lakini mtu akaona Nuru kutokana na akili yake kuwa na Nuru.
Giza linamfanya mtu asione hata kama ni mchana
Usiku hamfanyi mtu asione.

7. NURU Vs MCHANA

Nuru ipo akilini/ Fikarani
Mchana upo machoni
Panaweza kukawa mchana lakini mtu asione kwa sababu akili yake haina Nuru.

8. THAMANI Vs GHARAMA
Thamani ni ulazima wa kitu au jambo
Gharama ni umuhimu wa kitu au jambo
Thamani hulenga watu wote kwa sababu ni jambo//kitu cha lazima.
Gharama hulenga watu wa wachache kwa sababu sio cha lazima.

Vitu vya thamani ni kama vile Ardhi, Hewa,, Mwanga wa jua, Maji kwani watu wote bila hivyo hatuwezi kuendeea kuishi

Vitu vya Gharama ni kama vile Majumba mazuri, Magari, Simu, Vito cha thamani kama dhahabu n.k.

Maisha huwa magumu pale ushindwapo kutofautisha thamani na gharama.

9. UPENDO Vs MAPENZI

Upendo upo Rohoni na moyoni
Mapenzi yapo mwilini na akilini.

Upendo hauishi kwa sababu umezaliwa rohoni, ni mtamu kwa sababu unaishi moyoni.
Mapenzi hayadumu kwa sababu yamezaliwa akilini, na yanatesa kwa sababu yanaishi mwilini..
Kadiri maumbile ya mwili yanavyobadilika ndivyo mapenzi yanavyobadilika, lakini mabadiliko hayo hayaathiri Upendo kwani Roho ya mtu haibadilikagi ni ile ile tangu amezaliwa mpaka atakapoondoka.

10. WAKATI Vs MUDA

Wakati hauishi
Muda unaisha
Wakati hauna usiku wala mchana
Muda unao usiku na mchana

11. UTIMILIFU Vs UKAMILIFU

Utimilifu bila kuwa na kasoro, nyoofu iliyotimia.
Ukamilifu ina pande mbili kuwa na kasoro au kuwa nyoofu.

Kuna watu wanasema Hakuna mwanadamu Mkamilifu, sio kweli, Binadamu ni wakamilifu katika kukosea au katika kupatia. Wapo binadamu waliokuwa wakamilifu kwa kupatia yaani kutenda mema bila kutenda mabaya kama vile AYUBU.
Ayubu 1:1
1 Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu; alimcha Mungu na kuepukana na uovu.

Kwa leo niishie hapa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Iringa Mjini
 
MTIKISIKO VS MRINDIMO

Kutikisika ni kutetemeka mwili mzima hususani wembamba! Bali Mrindimo ni kutetemeka makalio tu! Hususan wenye nyungu
 
𝗞𝘂𝗰𝗵𝗼𝗸𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗸𝗮𝘁𝗮 𝘁𝗮𝗺𝗮𝗮 𝗷𝗲?
 
𝗞𝘂𝗰𝗵𝗼𝗸𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗸𝗮𝘁𝗮 𝘁𝗮𝗺𝗮𝗮 𝗷𝗲?

Kuchoka kiwango cha mwisho cha kushindwa kustahili/ kuvumilia iwe kwa uvivu kwa kwa uwezo wa mwisho.

Kukata tamaa, kukosa tumaini, uhakika, kushindwa au kukutana na jambo ambalo ushaona huliwezi.
 
Uvivu vs kujikimu
Ujinga vs Upumbavu
Kuswali vs kusali ???

Uvivu, utayari mdogo wa kusua sua, kutofanya jambo kwa moyo, kufanya jambo ilimradi
Kujikimu, kujipa mahitaji

Ujinga, kutokuwa na maarifa, elimu, ujuzi, na ufahamu wa mambo/jambo fulani
Upumbavu, Kujua jambo fulani na usilifuate, kutojua jambo fulani na hutaki kulijua

Kuswali ni ibada ya jumla kwa waislamu
Kusali ni kipengele cha ibada kwa Wakristo kinachohusu Kuomba, maombi
 
Kujisaidia ni kujipa nafuu katika jambo fulani, binadamu anapobanwa na Kinyesi/mavi, hujisaidia ili kujipa unafuu

Kunya ni kitendo cha kutoa kinyesi kwa binadamu
Kwahiyo mtu akiwa chooni Anajisaidia au anakunya?
Ni tukio gani sahihi kuita! Binadam anapotoa haja chooni ?
Neno lipi sahihi?
 
Kwahiyo mtu akiwa chooni Anajisaidia au anakunya?
Ni tukio gani sahihi kuita! Binadam anapotoa haja chooni ?
Neno lipi sahihi?

Yote ni sahihi inategemea na namna tukio linavyofanyika.

Kujisaidia kunahusu uungwana
Kunya kunahusu ushenzi

Mtu akitoa atoa haja kubwa chooni kiungwana huitwa kinyesi, na anajisaidia
Mtu akitoa haja kubwa maeneo yasiyo rasmi huitwa mavi, na tukio hilo huitwa Kunya.

Mtu akiingia chooni akatoa kinyesi na kuweka sehemu inayostahili na kusafisha huitwa kujisaidia
Mtu anayeingia chooni akaharibu mambo akaacha mavi yake sehemu isiyostahili huitwa kunya.

Heshima ya maneno apewayo mwanadamu inatokana na uungwana wake, akienda kinyume basi neno halisi hutumika
 
Back
Top Bottom