Ukiweza kuishi na watu, Umekubali kuwa mtumwa

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
2,211
2,000
Hi everybody ....

Kumekuwa na kawaida ya

Watu wapole wanaokubali kila wanachoambiwa bila kupinga ...wanajua kuishi na watu

Watu wenye kutoa msaada muda wote pindi inavohitajika kufanya hvyo...wanajua kuishi na watu

Watu wanaofanya yale yanayowapendeza wengine machoni wanajua kuishi na watu

Watu wenye utii wa hali ya juu kwa kila wanachoambiwa ...wanajua kuishi na watu

Watu wanaojitoa sana ...wanajua kuishi na watu...n.k ..

Yani ukiweza kufanya yale yanayo wafurahisha wengine bila kujali yanakuumiza kwa namna gani , yatakuingizia hasara kiasi gani, Yanakuathiri kiasi gani
Jamii itakuchukulia kuwa unajua kuishi na watu , Ila ukienda kinyume nao basi hujui kuishi na watu

Hii mentality imejengeka kwenye Jamii na kupelekea watu kufanya hata yale yanayowaumiza ilimradi tuu aonekane kuwa ana roho nzuri ,ana Utu, anajali ,bila kuangalia anagharamika kiasi gani

Ukiishi kwa kufuata misingi yako ujiandae kukosolewa ,kutopendwa na hata kufanyiwa mambo mabaya kwa makusudi

Ukitaka kuridhisha kila mtu ..Ujue umekubali kuwa mtumwa
 
Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
2,211
2,000
Ukitazama mafunzo na maelekezo ya vitabu vya kiimani utaona matokeo ya tabia chanya au hasi ktk jamii.
Hizo hapo juu ni baadhi ya tabia chanya zinazochochea amani na upendo ktk jamii.

Tabia hasi nazo matokeo yake yanafahamika.
Ni kweli kabisa mkuu lakini ni muhimu kufanya vitu kwa kiasi na sio kwa msukumo wa Jamii ...coz ukiwaendekeza sana watu utageuka mtumwa ..na at the end vile unavojitoa n tofaut kabisa na return ...Ndo maana kuna msemo tenda wema uende zako lakini haina maana kwamba wema upitilize
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
25,575
2,000
ndio maana ya neno upendo wa agape mkuu.

mara nyingi watu wa hivi huwa hawahesabu mabaya ya wanaoishi nao,wao hujitoa kwa ajili yao hata iweje.

gues what,huwa ni watu wenye furaha zaidi na amani sana,maana wanajua binaadam hata afake vipi,kuna point lazina atazikumbuka fadhira anazomfanyia.

nami nikusihi,ili uwe na mafanikio zaidi hapa duniani,jitahidi kutendea mema wengine na si kujitizama wewe zaidi.
 
ukiishasema wema usizidi uwezo huo sio wema tena.

najua utashangaa,yess wema hauna mpaka.
kwenye haya maisha unawezakutana na rafiki au mtu tu halafu
ukashangaa anavyojitoa kwako,kiasi ukahisi labda anataka kukutoa kafara.

vipi ukajifunza kwake ukatendee wengine!!!dunia ingekuwaje???
 
Mkuu nakubaliana na ww lakini hata Vitabu vya dini vinatuhusia. Kufanya kila kitu kwa kiasi ... Too much of everything is harmful ...
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
25,575
2,000
Bado tuna mentality za kijamaa..mtu anaona sifa kusifiwa ana roho nzuri..kisa ndugu wamejazana nyumbani kwake wanakula bure,mbaya zaidi wanaharibu mpaka watoto wake.
hizo ndio gharama za kusifiwa una roho nzuri.

kuna watu hawatongozewi wake mtaani kutokana na siha hiyo tu.hata binti yake mzuri unamuogopa maana ni kama unahisii kuikosea nafsi yako kwa kumtendea baya asiye mbaya.
au huwa tuna kauli moja"baba yake au mume wake mtu poa sana namheshimu".
 
Cadinali

Member
Feb 13, 2020
10
45
Hi everybody ....

Kumekuwa na kawaida ya

Watu wapole wanaokubali kila wanachoambiwa bila kupinga ...wanajua kuishi na watu

Watu wenye kutoa msaada muda wote pindi inavohitajika kufanya hvyo...wanajua kuishi na watu

Watu wanaofanya yale yanayowapendeza wengine machoni wanajua kuishi na watu

Watu wenye utii wa hali ya juu kwa kila wanachoambiwa ...wanajua kuishi na watu

Watu wanaojitoa sana ...wanajua kuishi na watu...n.k ..

Yani ukiweza kufanya yale yanayo wafurahisha wengine bila kujali yanakuumiza kwa namna gani , yatakuingizia hasara kiasi gani, Yanakuathiri kiasi gani
Jamii itakuchukulia kuwa unajua kuishi na watu , Ila ukienda kinyume nao basi hujui kuishi na watu

Hii mentality imejengeka kwenye Jamii na kupelekea watu kufanya hata yale yanayowaumiza ilimradi tuu aonekane kuwa ana roho nzuri ,ana Utu, anajali ,bila kuangalia anagharamika kiasi gani

Ukiishi kwa kufuata misingi yako ujiandae kukosolewa ,kutopendwa na hata kufanyiwa mambo mabaya kwa makusudi

Ukitaka kuridhisha kila mtu ..Ujue umekubali kuwa mtumwa
Kiufupi ukiona unapendwa na kila mtu jua unashida
 
Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
2,211
2,000
hizo ndio gharama za kusifiwa una roho nzuri.

kuna watu hawatongozewi wake mtaani kutokana na siha hiyo tu.hata binti yake mzuri unamuogopa maana ni kama unahisii kuikosea nafsi yako kwa kumtendea baya asiye mbaya.
au huwa tuna kauli moja"baba yake au mume wake mtu poa sana namheshimu".
Mkuu tembea uone kuna watu wema mnoo na bado watu wanawafanyia yasiyostahili
 
Blood of Jesus

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
1,498
2,000
Maisha ya hapa duniani ni mafupi sana. Ukiwa na uwezo wa kuwasaidia wengine fanya hivyo kwa moyo mweupe. Aliyekupa wewe ndiye aliyewanyima wao. Duniani hatukuja na kitu na hatutoondoka na kitu. Wekeni hazina zenu mbinguni ambako hakuna kutu wala wevi. Uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. Heri kutoa kuliko kupokea. ...

Fanya hivi utaishi maisha ya raha sana.

JESUS IS LORD!
 
Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
7,319
2,000
ndio maana ya neno upendo wa agape mkuu.

mara nyingi watu wa hivi huwa hawahesabu mabaya ya wanaoishi nao,wao hujitoa kwa ajili yao hata iweje.

gues what,huwa ni watu wenye furaha zaidi na amani sana,maana wanajua binaadam hata afake vipi,kuna point lazina atazikumbuka fadhira anazomfanyia.

nami nikusihi,ili uwe na mafanikio zaidi hapa duniani,jitahidi kutendea mema wengine na si kujitizama wewe zaidi.
Points. Na hivi ndivo ninavoishi na majirani pamoja na watu wanaonizunguka.
Niko na Amani na maisha yanaenda
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom